PASSOVER (Wayahudi) VS PASAKA (Wakristo) VS Kutokula Nyama

PASSOVER (Wayahudi) VS PASAKA (Wakristo) VS Kutokula Nyama

Castle_Lite

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2016
Posts
3,533
Reaction score
6,930
Mungu akubariki katika tafakari ya mateso ya Bwana wetu Yesu Kristo siku ya Leo.

- Yesu Kristo aliikuta Pasaka.
Tunaona kwenye Biblia kuwa Mipango ya kumkamata na Kumuua ilipangwa kipind cha majirio ya Passover.

Marko 14:1-2
"1 Baada ya siku mbili ilikuwa sikukuu ya Pasaka, na mikate isiyochachwa; wakuu wa makuhani na waandishi wakatafuta njia ya kumkamata kwa hila na kumwua.

2 Kwa maana walisema, Isiwe kwa wakati wa sikukuu, isije ikatokea ghasia katika watu. "

Passover inatokana na neno la Kiebrania, Pesach. ni sikukuu muhimu sana kwa Wayahudi inayokumbuka tukio la kihistoria la ukombozi wao kutoka utumwani Misri.

Wana wa Israeli walikuwa watumwa nchini Misri, Mungu alimtuma Musa awaokoe.Baada ya mapigo 10 kwa Wamisri, Farao aliwaruhusu waondoke

Ule Usiku wa pigo la mwisho, malaika wa mauti alipita Misri, Nyumba za Waisraeli zilipakwa damu ya kondoo mlangon, Malaika “alipita juu” ya nyumba hizo (ndiyo maana Passover = kupita juu), Akaziacha . Ila alikuwa anaua Wazaliwa wa Kwanza kwenye nyumba ambazo hazina Hiyo damu ya mwana Kondoo.

Pasaka ya Wakristo ilikuja baada ya Yesu. ni sikukuu inayoadhimisha kufufuka kwa Yesu Kristo baada ya kusulubiwa.

Yesu alisulubiwa siku ya Ijumaa, Alizikwa kaburin na Baada ya siku tatu (Jumapili),alifufuka kutoka kwa wafu.

Wakristo Duniani Kote wanasherehekea Pasaka na sio Passover. Na kipind hiki kiliongezewa na zile siku 40 alizofunga Yesu akiwa Jagwani.

Kwenye siku hizi 40 za Maandalizi kabla ya Pasaka. Wakristo hufunga na kujizuia baadhi ya vitu vya Anasa na starehe nyingne.

Kwanini Nyama Hailiwi siku ya Ijumaa?.
Nyama ilichukuliwa kama chakula cha anasa huko zamani na Kuacha kula nyama ni ishara ya unyenyekevu kwa Wakristo. kujinyima na kuonyesha mshikamano na mateso yake Bwana wetu Yesu Kristo aliyokutana nayo siku ya Ijumaa.

Madhehebu Mengne kama Wakatoliki Huruhusu samaki kwa madai kuwa sio Nyama ya Kuchinja wakisanikisha na tukio lile la Kuchinja mwana Kondoo kwenye siku ya Passover (nchini Misri).

Nikutakie tafakari njema ya siku ya Ijumaa Kuu.
 
Maana ya Pasaka
AGANO LA KALE: Pasaka ni kutolewa utumwani (Misri) kupelekwa kwenye ahadi (Kaanani).

AGANO JIPYA: Pasaka ni hali ya kutolewa kwenye mauti ya kiroho (Israeli ya kiroho/Ukristo wa kwanza) kwenda uzimani (Israeli mpya ya kiroho/ Ukristo wa pili/mpya).

Elimika sasa mpenzi.
 
nimefika kwenye huu msitari nikiwa na kipande cha nyama dah😥 sijui niteme tu,,,,

nimekumbuka mimi ni msabato wacha nizitafuneee

Usabato ni mgumu sana.

Mm napenda wanavyoimba na wanavyojiweka Natural. Hasa wanawake.

Na Ukikuta Pisi ya kisabato alaf awe mzur. Bas ni mzur kweli.
😂😂😂😂
 
Usabato ni mgumu sana.

Mm napenda wanavyoimba na wanavyojiweka Natural. Hasa wanawake.

Na Ukikuta Pisi ya kisabato alaf awe mzur. Bas ni mzur kweli.
😂😂😂😂
hata sio mgumu ila ukizoea utaona kila kitu kipo kawaida,, mim nimezaliwa na kukulia usabatoni kwahiyo sioni changamoto yyote

sisi ni timu naturally😆, maadili ya kisabato yamenifanya nishindwe kupaka makeup kabisa🤦‍♀️🤦‍♀️ ila lipstick huwa,najaribu mara moja moja na saivi ndo nimeanza na kusuka,, vipodozi vingine vinanishinda kabisa

mfano mzuri ni mimi👌😇 mama yangu alizaa hebu nimpe maua yake tu ( wanao nifahamu wasione hii comment🤣🤣),, olu ñ olu mimi ni kareembooo sema ndo vile bado najitafuta😆😆😆😆
 
Nakumbuka moja ya mahuburi ya father Babu marehemu namnukuu.
Kutokula nyama siku ya ijumaa ni ku shiriki mateso kwa kujinyima
Sasa kwa muafrika mateso anashiriki mwaka mzima, robo tatu ya watanzania kiuhalisia nyama kwao ni anasa na hailiwi ovyo au kila siku..... Kwa hiyo kwa muafrika kula nyama Leo si dhambi na hata kama ni dhambi basi familia zenye uwezo wa kupika samaki Leo kwa mbadala wa nyama ni chache mnooo.... Hii dhambi afrika haipo.
Mi leo kama nyama ipo nakula.
 
hata sio mgumu ila ukizoea utaona kila kitu kipo kawaida,, mim nimezaliwa na kukulia usabatoni kwahiyo sioni changamoto yyote

sisi ni timu naturally😆, maadili ya kisabato yamenifanya nishindwe kupaka makeup kabisa🤦‍♀️🤦‍♀️ ila lipstick huwa,najaribu mara moja moja na saivi ndo nimeanza na kusuka,, vipodozi vingine vinanishinda kabisa

mfano mzuri ni mimi👌😇 mama yangu alizaa hebu nimpe maua yake tu ( wanao nifahamu wasione hii comment🤣🤣),, olu ñ olu mimi ni kareembooo sema ndo vile bado najitafuta😆😆😆😆
Mjukuu hujasubiri kupewa maua, umeamua kujipa mwenyewe😅
Nakukaribisha Mbezi Luis kesho, nitasali hapo😅😅
 
sisi ni timu naturally😆, maadi ya kisabato yamenifanya nishindwe kupaka makeup kabisa🤦‍♀️🤦‍♀️ ila lipstick huwa,najaribu mara moja moja na saivi ndo nimeanza na kusuka,, vipodozi vingine vinanishinda kabisa

Lipshine inatosha.
Achana na Makeup na mavipodozi . Rang yako asil itapotea. Ila kusuka muhim ili unoge vizur. 😍😍😍

mfano mzuri ni mimi👌😇 mama yangu alizaa hebu nimpe maua yake tu ( wanao nifahamu wasione hii comment🤣🤣),, olu ñ olu mimi ni kareembooo sema ndo vile bado najitafuta😆😆

Hongera sana kwa kuwa mcute.
Its just matter of time. Utajipata.

nakushaur tu funga PM kwa leo 😂😂😂😂 vijana wa JF unawajua.
Wandan wandan na wa nje wa nje.
 
Mjukuu hujasubiri kupewa maua, umeamua kujipa mwenyewe😅
Nakukaribisha Mbezi Luis kesho, nitasali hapo😅😅
sijataka kusubiri kabisa babu😆😆 raha na maua najipa mwenyew, ila familia yangu huwa inanipa mara moja moja isipokua kaka yangu mmoja😪

asanteee siku nikija dar nitakutafuta tusali wote tena natamani iwe sabato ya wageni ili nisikupe tabu sanaa ya kunitambulisha kwenye familia mpya☺️🤗,,, asante babu 🙏
 
Back
Top Bottom