Paschal Mayalla simama upande wa haki au heri ukae kimya

Paschal Mayalla simama upande wa haki au heri ukae kimya

Hawa wazee wapumzike tu, mzee mwenzake Mohamed Said ameamua ku deal na historia ya uislamu katika mchango wa kupambania uhuru Tanganyika.

Mayalla nae atumie ujuzi wake wa uandishi kuandika mambo mengine yasiyohusu zaidi siasa, maana watu hawamuelewi.
Asipotambua nyakati atakua mtu aliyeshika mawili kisha yakamponyoka yote... Huyu jamaa alikua anaheshimika na watanzania wote kuanzia serikalini hadi mtaani, ila ile heshima aliyokua nayo imegeuka aibu hadi kwangu niliyeipenda jamiiforum kupitia yeye
 
Inasikitisha sana.
Tumsaidie aisee hata kwa ushauri, baadae akija hapa tumshauri mzee wetu Paskali.
 
mzee Pascal Mayalla hataki ukiherehere ulio mponza enzi za magu, Kumbuka ana uzi alisema kapata mtoto enzi za karibuni.

Kingine maisha yana badilika, hivyo nae ajaribu kubadili style ya kalamu yake ili kulinda heshima ya taaluma yake.
 
Moja ya tatizo kubwa la watanzania ni kukosa proper civil education. Of what it means to be a country man. Tumefundishwa kuabudu na kusujudu viongozi na si taifa. Ndio maana kuna utitiri wa wanasiasa wanaruka ruka tu kutoka chama hiki kwenda kingine. Hawana values wanasimamia.
 
Asipotambua nyakati atakua mtu aliyeshika mawili kisha yakamponyoka yote... Huyu jamaa alikua anaheshimika na watanzania wote kuanzia serikalini hadi mtaani, ila ile heshima aliyokua nayo imegeuka aibu hadi kwangu niliyeipenda jamiiforum kupitia yeye
Huyo ameshakula mtaji wake wa kitaaluma siku nyingi. He can no longer be counted on to perform to the professional standard!
 
Enzi za ujana wake alikuwa akiwakaanga vizuri vigogo wa serikali DTV, bila woga, kwenye kile kipindi chake cha kitimoto.
Ndio mkubali JK alikuwa na uungwana kwenye uhuru wa habari
Alitukanwa , Alibezwa na mpaka hata mtoto wake alizodolewa kwenye matokea, lakini Mzee alikuwa anacheka tu......
Mlivyompata Jiwe mkafurahi na mihemko yake, na huyo ndio alimfinya Pasco, na vyombo vyote habari, ndio uliokuawa mwanzo wa udikteta uchwara unaendelea sasa.....
 
Ndio mkubali JK alikuwa na uungwana kwenye uhuru wa habari
Alitukanwa , Alibezwa na mpaka hata mtoto wake alizodolewa kwenye matokea, lakini Mzee alikuwa anacheka tu......
Mlivyompata Jiwe mkafurahi na mihemko yake, na huyo ndio alimfinya Pasco, na vyombo vyote habari, ndio uliokuawa mwanzo wa udikteta uchwara unaendelea sasa....
Kitimoto ilikuwa enzi za Mkapa, 1995 kama sikosei.

Jk ndiyo mwanzishi wa haya mambo ya utekaji na siasa chafu, Magu hahusiki.

Unakumbuka walivyomchafua mzee wetu Dr Salim? Unakumbuka Dr Ulimboka alivyotupwa Mwabepande na Mwangosi alivyotolewa utumbo kila mtu anaona?

Sasa Magu hayupo, haya yanaendela, kwa nini? Huoni "the common factor" hapo ni huyo JK, tunayeambiwa ni boss.
 
Paschal Mayalla,wewe ni mzee,lakini tumia Hekima na busara uliyonayo,damu ya watanzania iliyomwagika itakulaani kizazi chako chote,kwa kusimama na wadhalimu,heri kuwa kimya kuliko kuongea na kusimama upande wa wadhalimu,

Nakuomba mzee wangu malizia uzee wako kwa hekima,Duniani hakuna kilicho chenye pumzi kitadumu milele maana sote tutakufa,japo vifo vyetu vitatukumba kwa Mikasa tofauti tofauti,lakini heri kusimama katika haki maana ni heshima ya milele na utatengeneza kitabu cha historia nzuri na ya hekima pia utaishi mioyoni mwa watu waliyo Hai milele na milele ijapokuwa katika kipindi hicho ni mfu wa millenia.
Shida yenu kubwa nyinyi hamtaki mtu awe na misimamo tofauti lazima wakubaliane na nyinyi, nani kaamua kama upande wako ndio wa haki? Nyinyi mtakuwa worse than CCM mkipata power. Yoyote mwenye mawazo different ni adui, nini tofauti yenu na CCM?
 
Ndio mkubali JK alikuwa na uungwana kwenye uhuru wa habari
Alitukanwa , Alibezwa na mpaka hata mtoto wake alizodolewa kwenye matokea, lakini Mzee alikuwa anacheka tu......
Mlivyompata Jiwe mkafurahi na mihemko yake, na huyo ndio alimfinya Pasco, na vyombo vyote habari, ndio uliokuawa mwanzo wa udikteta uchwara unaendelea sasa.....
Na wanamlilia JPM leo ndio ujue unafiki wa watu. Wakati Pasco anaadhibiwa bila kosa hawa watu wanajiita upande wa haki walikuwa kimyaa wanacheka tu. Kiuhalisia Pasco lile swali likuwa halina shida yoyote na alikuwa anawasemea hawa wapenda haku wa leo lakini walikuwa wanacheka. Nani alitoka hadharani kumtetea Pasco?
 
Back
Top Bottom