Pascal Mayalla anafaa kuwa Msemaji wa Serikali

Abeto Malakoti

Senior Member
Feb 7, 2018
122
234
Kwa kuwa Dkt. Hassan Abbas ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ni ambayo ni nafasi yenye majukumu mengi na mazito ya kiutawala huku akiendelea kuwa Msemaji Mkuu wa Serikali, ni rai yangu kuwa Rais amteue Msemaji Mkuu wa Serikali mpya ili Dkt. Abbas apate muda wa kutosha wa kujikita katika nafasi yake ya Ukatibu Mkuu kikamilifu.

Kwa sasa Mitandao ya kijamii ina nguvu na ushawishi mkubwa sana kijamii, kisiasa na kiuchumi kuliko magazeti magazeti, online newspaper, online TV, radio and television Television Stations.

Nguvu na ushawishi wa mitandao ya kijamii kama vile WhatsApp, Facebook, Twitter, na Instagram katika nyanja za siasa, uchumi na kijamii unazidi kuongezeka kwa kasi kubwa kila siku.

Mara kadhaa Serikali, taasisi za Serikali, vyama vya siasa, taasisi za kidini, asasi za kiraia n.k zimejitokeza kujibu tuhuma, hoja, masuala na maswali ambayo yameibuliwa na mitandao ya kijamii na hiki ni kielelezo tosha cha nguvu ya mitandao ya kijamii.

Pia, tasnia ya habari imechangamana sana na teknolojia ya habari na mchangamano huu umeleta changamoto kadhaa za kisheria na za kiteknolojia kwenye sekta ya habari, hivyo, Msemaji Mkuu wa Serikali ambaye pia kwa mujibu wa sheria ni Mkurugenzi wa Idara ya Huduma ya Habari na Mshauri Mkuu wa Serikali wa Masuala ya Habari na Mawasiliano ya Kimkakati na Uchapishaji wa Habari anapashwa kuwa na ABCs za sheria na teknolojia ya habari na mawasiliano.

Hivyo basi, moja wapo ya sifa kubwa na muhimu ambaye Rais na washauri wake wanapashwa kuzingatia katika uteuzi wa Msemaji Mkuu wa Serikali ni uelewa na uzoefu wa kutosha katika nyanja ya mitandao ya kijamii na uelewa wa kiasi fulani sheria na teknolojia ya habari na hata mawasiliano.

Hivyo basi, kwa maoni yangu ninaona Paschal Mayalla wa JamiiForums anafaa kuvaa viatu vya Dkt. Hassan Abbas kwa kuwa ana uzoefu wa kutosha kwenye tasnia ya habari na ana added advantages kadhaa ikiwemo ya kuwa mwanasheria na kuwa uelewa na uzoefu mkubwa wa mitandao ya kijamii na ana ABCs za teknolojia ya habari na ni multi-knowledge au polymanth kwa maana ya kwamba ana maarifa na uelewa wa kiasi fulani ambao sio wa formal training karibu kila taaluma au tasnia kama vile siasa, historia, sheria, theolojia, lugha, soshiolojia, falsafa na kadhalika.

Watu ambao ni Polymanth au multi-knowledge ni viumbe adimu sana hapa duniani na hususani Tanzania na kwenye baraza la mawaziri Polymanth au multi-knowledge ni yuko mmoja tu Prof. Kabudi pekee.

Hivyo, Mhe. Rais ninakushauli kutumia mamlaka yako chaini ya Kifungu cha 4 (1) cha Sheria ya Huduma ya Habari, 2016, kumteua Ndugu Paschal Mayala kuwa Msemaji Mkuu wa Serikali, Mkurugenzi wa Idara ya Huduma ya Habari na Mshauri Mkuu wa Serikali wa Maswala ya Habari na Mawasiliano ya Kimkakati na Uchapishaji wa Habari.

Naomba kuwasilisha.
 
Hiyo Post unayo mpigia chapuo ni ya kiserekali na ina ukomo wa umri. Nadhani itaikosti serekali sana kumteua mtu akakae pale miezi kadhaa tu halafu astaafu kwa mujibu wa sheria. Kumbuka tunaheshimu utawala bora.
 
Apana ndugu Abeto, Pascal apewe nafasi ya Polepole, na pole apelekwe ikulu, maanake PP akiwa ikulu, atawacha kuropoka kipumbavu ama sivyo atachapwa vibao na bosi wake.
 
Back
Top Bottom