Slim5
JF-Expert Member
- Jan 7, 2014
- 28,374
- 38,248
Mungu wangu. Dada ako akabadili mtindo wa ukaaji pale mgahawani. Mwanzo tulikaa kama vile watu wakaavyo katika siti ya dala dala, ile siti ya watu wawili, lakini sasa amekaa tunatizamana. Nikaona ile min skirt ya gold ikipanda juu. Wakati akikaa huku akiilazimisha kuishusha chini, ni kama vile alitaka nijue anajisitiri na maungo yake, ana heshima, japo ukweli wa moyoni mwake alikuwa anasema weeee …….., angalia huku basi, lugha ngumu, basi hata picha huoni!

Sijui kama nina bahati ama nina mkosi. Mungu anajua. Tuliachana mwenge. ukanisifu kwa kuwa na kibarua, ukanipa hongera. Ukaahidi utanpitia mchana wakati ukienda Muhimbili kumuangalia manusra wangu wa ajali. Nikakuitikia sawa. Nilipiga kazi mpaka jioni, sikukuona tena kwa siku ile, ni kwamba hukuja kunipitia.
Hali yako mgonjwa wangu iliendelea vizuri. Nilijitahidi walau nisimalize siku 3 bila kuja kukuona pale Muhimbili. Niliweza. Mara ya mwisho kuja kukuona Muhimbili, ulinipa taarifa kuwa kesho yake ungetoka Hospitali na kurudi nyumbani. Watu wa Muhimbili, wamesema kikubwa kilichobaki ni mazoezi ya viungo. Wakakupa ratiba ya kuhudhuria vipindi vya mazoezi hospitali na wakakusisitiza pia mazoezi yako binafsi nyumbani.
Sasa ratiba ikageuka. Safari za Muhimbili zikafa. Sasa hivi kuna ratiba mpya. Ratiba ya kuja kukuona Manusra wangu wa ajali, unapoishi pale ubungo, si mbali na eneo ambalo kisanga kizima kilikupata hapo. Hili la kuja kukuona ubungo halikuwaa gumu, si ndio njia ya kurudi uswahilini kwetu. Ratiba ya kuja kukuona muhimbili kipindi kile ndio ilikuwa ngumu sana kwa upande wangu, lakini sio hii ya kuja hapo unapoishi, ubungo.
Kutokana na majukumu ya kibarua changu, nilijiwekea utaratibu wa kuja kukujulia hali nyakati za jioni baada ya kufunga kibarua changu. Hili nililiweza. Lilikuwa ndani ya uwezo wangu, nilichofanya ni kushuka, nakucheck then narudi tena barabarani, nadandia gari zangu za nyumbani. Ilikuwa rahi sana.
Nilikuja kukuona pale unapoishi. Mara kadhaa nilikukuta ukifanya mazoezi ya kutembea. Ulikuwa unatembea kwa kutumia fimbo maalumu uliyorudi nayo kutoka Muhimbili. Maendeleo ya mguu wako yalionyesha dalili ya kuwa ungepona ndani ya muda mfupi. Uliweza kupanda na kushuka ngazi. Ilikuwa inanifurahisha kila ninapokuja ukinionyesha mabadiliko ktk mguu wako, wakati mwingine ukinitaka niushike, hasa maeneo ya juu karibu na kiuno, mh sikuweza.
Kumbe matukio hayajaisha bado.
Ukiwa na dalili zote za kupata nafuu, ilitokea siku ya siku nikaja nikakukuta pekee yako. Mara zote ninazokuja kukujulia hali huwa nakukuta na ndugu na jamaa zako, wakati mwingine akiwemo na Yule "mtu wako". Na mara zote dadako alikuwa akinisindikiza, mara tu ninapoaga, huwa ananisindikiza na kuhakikisha nimepanda dala dala ndio na yeye hurudi. Wakati mwingine hunilazimisha nile nae chakula!
Kuna wakati walaji hula tamu chungu, hii ilikuwa kwako sasa hivi. Ulifurahi kuniona. Ulichukia kwa nini sikukuti peke yako, yaani ulitamani siku ije tuwe wawili tu. Leo ndio leo. Nimekukuta peke yako, tena nimekukuta unajiandalia msosi, ulikuwa unapika viazi nyama. Sijawahi kukuona una furaha kama furaha uliyokuwa nayo siku ya leo.
Sikuweza kung'amua nini hasa uhalisia wa furaha yako. Ulilisisitiza kuwa umefurahi nimekukuta ukiwa free. Bado sikukuelewa, kwa macho yangu nilikuona uko busy na mapishi, lakini mwenyewwe unadai u free. Nakumbuka ulianza na maswali. Uliuliza maswali mengi. Yapo maswali yaliyofanana na yale alokuwa akiniuliza "dada", na pia kuna maswali yalikuwa mapya kabisa.
Ukaniomba ruhusa uniache ukaoge, ukaenda. Sijawahi kumuona mtoto wa kike maishani mwangu, akiwa na matatizo ya mguu yaliopelekea avalishwe P.O.P na mwilini anapiga min – skirt. Hii ndio kwa mara ya kwanza naiona. Kuishi kwingi kuona mengi. Moyoni nilijua kuwa, kama nilidhani ile ya dada ilikuwa cinema, basi nilikosea, ile ni picha utanguliza, sinema ipo hapa leo. Chumbani. Watu wawili tu. Hamna muuza supu wala muuza chapati. Hapa hamna wapita njia kama wale wa Muhimbili. Hapa ni mimi na wewe tu.
Najua kuwa tembea yako ni ya kuchecheme kutokana na hili P.O.P, sawa, ila hii chechemea ya leo, mungu wangu, imezidi, acha niseme. Nishawaona watu wengi wenye majeruhi ya mguu, huwa wanachechemea lakini si kama unavochechemea wewe leo hii hapa chumbani kwako. Ni kama vile kuna sumaku, sikujua kwa nini macho yangu hayakuweza kuangalia sehemu nyingine, bali ni kwako tu, ukichechemea!
Ukapakua chakula. Kwa mara ya kwanza nakula chakula ulichopika mgonjwa wangu. Nilikusisitiza uniwekee chakula kidogo tu (nikijua si muda mrefu kutaongezeka wageni ndani mle), hukujali, ulijaza cha kutosha kwa madai kuwa niache kujivunga. Wanaume hula kwa maana ya kula. Kama ulijua kuwa napenda nyama, ulijaza za kutosha. Ukaleta ktk kochi nililokaa. Nikapokea na bila kupoteza muda nikaanza kula. Ukaenda kuchukua sahani yako, kwa mwendo wako ule ule wa kuchechemea, ambao mgeni mpya asingejua kama ni kuumwa ama kashdah zimekujaa mtoto wa kike.
Ukaleta chakula chako. Haaaaa! Katika kile ambacho macho na akili yangu havikuamini kinachotokea hapa, tena kwa watu sisi wawili, yaani mgonjwa na msamariamwema wake, chumbani, juu ya kochi la mtu mmoja, sisi tumekaa wawili! Tena na sahani zetu za chakula mikononi. Nilishindwa kutoa neno. Nilishindwa kunyanyuka. Nilishindwa kupeleka kijiko mdomoni. Nilichoweza kufanya ni kusogea ili kupisha eneo lako la kiuno litoshee pale ktk lile kochi.
Mapigo ya moyo. Nikauskia moyo ukipiga tofauti na mapigo yale ya kila siku nilioyazoea. Hapa moyo unapiga tofauti. Nimekosa maelezo yake vizuri.
Hukujua tu. Sikuwepo pale. Kilikuwepo kiwiliwili, akili ilishahama zamani sana. Akili haikuhamia Mwenge, hapana. Mungu wangu. Kuna taswira zinanijia. Kuna watu nawaona. Wa kwanza namuona dada ako, namuona ndani ya min- skirt ya gold. Kuna mtu mwingine namuona. Namuona jamaa yako. Picha inanijia jinsi alivonikunja siku ile pale nje Muhimbili, siku ya kwanza kumjua. Namuona anavotokwa na mishipa ya shingo akihoji kuwa mimi na wewe tunafahamiana, na eti tulikuwa guest, eti katika haraka haraka zetu ndio wewe ukagongwa.
Nilihisi kuwa nimeipa akili kazi ya ziada leo. Akili inafanya kazi tofauti na uwezo wake. Chakula kimekuwa kichungu. Uroho wa nyama kwisha. Simezi. Sitemi. Watu watatu wananipa wakati mgumu kwa mara nyingine. Kichwani taswira ya matukio yote yatuhusuyo mimi na wewe inanijia. Kila tukio linakuja na dakika zake, na kuondoka. Kuna maneno ulianza kuyaongea. Uliongea kwa pozi sana. Uliongea mithili ya mwanasheria anaemsihi mtuhumiwa akiri kutenda makosa, kwa ahadi kuwa atamsaidi kuimaliza kesi. Yalipita sikio la kushoto, yakatokea lile la kulia! Sijui cha kufanya. Nikawaza. Kati kati ya kuwaza, nauona mlango wa kuingilia kwako unafunguliwa. Kuna mtu anaingia.
[FONT=" [B]Munkari[/B] miss neddy watu8 Blessed g click prospa michepuko naan ngik-kundie Foundation terasy Tarime one MJINI CHAI ZAMBI YANGU Mwana RR Lipa Kwanza Pritty wa joseph Freeland Mentor kashesho beb v Kanigini lin ram miss ngatara Kan'tangaze monanja Munkari Drama queen JEKI wisu tamuuuuu City hunter j 64gb The Boss muuza ubuyu mtvbase Honey Faith ICHANA sauti imenikauka, naomba niitieni na muwapendao![/FONT]