SHIEKA
JF-Expert Member
- Dec 20, 2011
- 8,240
- 4,280
Wandugu, Hamjambo wote?
Sikukusudia kuwa na kitu kiitwacho part ii ila imebidi iwe hivyo kwa sababu
nilipoanza, umeme ulinikatikia katikati kabla ya kumalizia thread.Nikamalizia
kwa kusema kwamba ntaendelea. Ntaendelea yenyewe ndo leo, ijumaa 27/3/2015
hivyo nafanya haraka nisikatikiwe tena ifikapo saa nne u nusu ambao ndo muda
umeme huku majumba kuinama hukatika.
Watu wangu leo ni FaizaFoxy, lara 1, kabanga, The Boss, Shyland
na Madame B.
Haya, tuanze.
FaizaFoxy - Mama Mtata/Mama Bodogadi wa J.Kikwete.WanaJF wengi wana jina jingine ila sipendi kulitaja hapa.
Usije ukafanya kosa la kumsema vibaya Rais J.Kikwete au ccm hapa JF.Faizafoxy atakuchanachana vipande kama mshikaki. Ila ukileta thread ya kuuponda utawala wa marehemu Nyerere au thread inayohusu kanisa fulani kuungua,
Faizafoxy atakupigia saluti na avatar yake hunenepa na kutabasamu.
JF ingekuwa ni mahali tunaonana uso kwa uso,kungekuwa na kesi nyingi sana za ama Faizafoxy kuzaba baadhi ya wana jf vibao, au baadhi ya wanajf kumkata mtama Faizafoxy!
CCM ingekuwa ni kitambaa cha nguo, basi Faizafoxy angekuwa uzi ulotumika kufuma kitambaa hicho.She is a dyed in the wool fanatic of ccm. Na hii imemfanya ashindwe kabisa kuvumilia upinzani. Haya, huyo ni faizafoxy, twende sasa kwa Lara 1
lara 1 - Dada Msomi wa Mujini/Mama Igweee.Elimu ya chuo kikuu ya huyu dada pamoia na mikasa ya maisha (lara 1 is 30+)vimemfanya lara 1 kuwa mtaalamu wa kusoma watu kama asomavyo kitabu. Lara 1 akizungumza nawe kwa muda wa dakika 5 tano tu, dakika mbili za mwanzo ameshafahamu wewe (hasa kwa wanaume) una kurasa ngapi, chapter zako ni refu au fupi kiasi gani nk.
Lara1 kwa sababu ya uwezo wa kusoma tabia za wanaume, anayamudu vyema maisha ya mjini ambayo yanatatiza wasichana wengi. Lara 1 anatamani sana kukusanya wasichana wote wa nchi hii kwenye semina moja kubwa kuwaelekeza jinsi yakutembea kwenye vichochoro vya maisha, wapi pa kukanyaga wapi pa kuruka nk.
(umeme umekatika lakini hii laptop niliyoazima ina backup ya battery)
The Boss -Mr. Interesting.Kuna wanajf wanajipinda mgongo kuandika koment ndeeefu! Si The Boss bwana. Atasoma thread yako vizuri na ili usimlaumu kwa kutochangia, anaingia kwenye keyboard yake na kukuzawadia herufi 11-interesting
Samahani waliobaki nawaweka pending mpaka umeme utakaporudi maana naona laptop inakoroma kinamna.