Part 2: Ujasusi ndani ya Boeing

Part 2: Ujasusi ndani ya Boeing

My Son drink water

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2016
Posts
4,930
Reaction score
13,333
Mara baada ya mashambulizi ya kigaidi ya Sept 11, Rais wa Marekani wa wakati huo George W Bush, alitoa hotuba fupi akiwa na hasira na macho yake yakiwa mekundu, akiwa ametoka kujificha kwenye handaki la kambi kubwa ya kijeshi iliyopo ktk jimbo la Louisiana.
"You're either with us or not with us "
Alikuwa akiiambia Dunia ichague upande wa kukaa, aidha iwe upande wa Marekani au wa adui.
Maana yake ni kwamba Marekani ina maadui wengi mno kuliko marafiki halisi, Kwa hiyo ilikuwa ni furaha kubwa mno kwa US kupigwa siku hiyo kwa adui zake.
Nakumbuka nilikuwa Khartoum Sudan siku hiyo Marekani inapigwa, hata kabla sijajua Kama imepigwa niliona watu mitaani wakishangilia Kwa furaha huku magari yakipita Kwa msululu yakipiga honi za furaha.
Kuna watu wamesema kuwa sijaandika sahihi juu ya ajali ya Boeing 737 kwamba engine haikusababisha ajali bali ni mfumo wa Computer, na kwamba ni ngumu Boeing kuhujumiwa eti kwa sababu engine za Boeing zinanunuliwa UK kutoka kampuni ya Rolls Royce.
Nataka kuwafafanulia kidogo hapo ili kuwaweka sawa, iko hivi, ndege huendeshwa kwa mfumo wa Computer ikiongozwa na watu walio chini ya ardhi na si rubani, waongoza ndege wana uwezo wa kupoteza ndege au kumpoteza rubani asijue analofanya.
Kazi ya Computer kwenye ndege ni kusoma na kuweka Taarifa ya kila kitu kwenye ndege, kuanzia engine zinavyofanya kazi, hali ya hewa na mengine mengi, engine ikiwa imara na Computer ikagoma kusoma mwenendo wa ndege, ndege itapata ajali Kwa kupotea na hii inachukua masaa mengi hadi ije kupata ajali na siyo prompt accident ambayo husababishwa na hitilafu kwenye engine Kama ilivyokuwa Kwa Ethiopian Airway.
Computer haiwezi kuishusha ndege, kazi yake ni ku record na ku monitor movements za kila device kwenye ndege.
Boeing 737 imehuhujumiwa, na ndo toleo jipya kabisa kwa Boeing, Kwa kampuni iliyo na uzoefu sokoni Kwa miaka zaidi ya 100, haiwezi kupata hitilafu ya engine wala Computer system software, Kwa sababu kabla ya kuruhusu ndege ziingie sokoni ni lazima ziwe verified, Kwa hiyo wataalamu wa Boeing wali verify na kujiridhisha kwamba zinafaa?
Jibu ni ndiyo, wali verify, lakini kwa sababu ya hujuma ndo maana zimeanguka.
Mission accomplished, tayari majuzi Rais wa China alikuwa Ufaransa, ameingia mkataba wa kununua ndege zaidi ya 60 na Airbus badala ya Boeing.
Ujasusi ni ujasusi tu, huwezi kuidharau nchi eti kwa sababu ni ndogo, an enemy you despise is always a powerful enemy.
Hakuna urafiki wala huruma kwenye maslahi, Marekani ni rafiki mkubwa wa Israel, lakini pamoja na urafiki wao kila mmoja anamwinda mwenzake Kwa staili yake.
Jonathan Pollard, alizaliwa na kukulia Marekani ktk familia ya kiyahudi, Kumbe wazazi wake waliohamia Marekani walikuwa majasusi Hatari sana, Pollard alipokua alianza kazi ya kuipeleleza US na kutuma Taarifa Israel, Hiki ni kisa cha kusisimua kinachohitaji makala yake maalumu.
Na kila mwezi alipokea mshahara kutoka serikali ya Israel .
Baadaye alishtukiwa na kukamatwa, alihukumiwa jela maisha,mwaka 2015,aliachiwa huru baada ya waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu kuipigia magoti Marekani.
Hebu fikiria, Marekani haili Chakula kikapita bila kuisaidia Israel, kipesa na silaha, lakini jamaa bado wanawachungulia.
Trump hana maslahi na Russia ila Israel pekee, na kuna Taarifa Mossad walicheza mchezo ili Trump awe Rais wa US, na si Russia ambayo wengi wanaamini, hebu tazama baada ya Trump kuwa Rais ndo aliyeitangaza officially Jerusalem kuwa capital city ya Israel,kwanini marais wengine waliogopa kutangaza?
Aliyemuoa Binti wa Trump ni myahudi anayedaiwa kuwa agent wa Mossad, connect dots hapo.
Unapohujumiwa kijasusi huwezi kujua,utakuja kujua umeshamalizwa. China hakuwa na technology,waliunda kitengo cha ujasusi wa kiuchumi Kwa ajili ya kuiba technology na kweli wakafanikiwa.
Ununuzi wa engine za Rolls Royce Kwa ajili ya Boeing kutoka UK hakuifanyi Boeing kuwa salama eti kwa sababu UK ni rafiki mkubwa wa US.
kenya imehangaika na ujasusi wa kiuchumi hadi imefanikiwa hatua Kwa hatua.
Viwanda vingi vilivyokuwa Tanzania vimekufa na kufufukia Kenya, tumebakia kuwabeza huku wakisonga mbele, ooh hicho ni kiwanda cha ku assemble magari na siyo kutengeneza, ok fine, nyie mnacho? Kiko wapi cha kwenu cha nyumbu??
Ni nani kaihujumu Boeing?
Tukutane part 3 sehemu ya mwisho


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii ni kweli..fitna muhimu ili wengine wa survive..linatengenezwa zengwe mnaaminishwa kisha watu wanapiga pesa..
 
kuna mchezo huwa nikiuangalia siulewi kabisa, unaitwa criket. huo naufananisha na hii thread maana mwandishi hajandika kwa mpanglio vitu vieleweke anyway nipo "chini ya ardhi" nackilizia.

Huwezi kuelewa kitu ambacho hujakitilia maanani...binafsi naelewa cricket japo sio mchezo ninaoupenda.
 
Nimejifunza kitu, big up mkuu; naisubiria part 3 ili nianze ku-connect dots.
 
Na hii ni hujuma au own opinion
Screenshot_2019-03-29-15-42-36.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom