Paroko akemea siasa za matope | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Paroko akemea siasa za matope

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mshume Kiyate, Apr 20, 2011.

 1. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #1
  Apr 20, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Imeelezwa kuwa siasa nchini inaendeshwa katika mfumo ambao ni wakupakana matope baina ya kundi fulani la viongozi kwa lengo la kuchafua sifa za viongozi wa kundi jingine ili kulifanya lionekane baya miongoni mwa wanajamii hata kama lina viongozi wenye sifa nzuri za za uongozi.
  Hayo yalisemwa na Paroko wa Parokia ya Sinza, Padri Cathbeth Maganga wakati wa mahubiri yake katika Ibada ya misa ya Dominika ya matawi iliyofanyika Parokiani hapo, Padri Maganga alisema kuwa baadhi ya watu wasio na nia njema wamekuwa wakiwazushia wenzao mambo yasiyo ya kweli kwa lengo la kuharibia sifa nzuri walizonazo jambo ambalo husababisha taifa kuwa na viongozi wenye hila mbaya na ufisadi mkubwa. kuwabebesha sifa mbaya watu wema hakipishani na kitendo kilichofanywa na Wayaudi cha kumtesa Yesu Kiristo mpaka kufa msalabani, pamoja na kwamba kauli ya Padri Maganga haikutaja ni kundi gani la viongozi au chama kinachofanya mchezo huo, lakini kauli hiyo imekuwa ni jibu baada ya Katibu Mkuu wa Chadema, DK Willibrod Slaa kutaja orodha mpya ya majina ya watu aliyodaiwa kuwa ni mafisadi.
  SOURCE: MWANANCHI APRILI 20, 2011
   
 2. koo

  koo JF-Expert Member

  #2
  Apr 20, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 258
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kwanini unakua mwepesi kwa mambo mazito huwezi kujua kwamba kundi linalodhaniwa kama ndio gamba ndani ya ccm ndilo limepakwa matope na linapenyezqa pesa ili kutafuta uungwaji mkiono kwa jamii slaa hapaki matope anatoa ushahidi nahivyo kuwaachia wananch waamue kama nikweri au la lakini ccm imewafukuza wenzao pasipo kutoa ushahidi na hicho kimepelekea paroko akemee usipende kumtaja dkt kama huna chakusema
   
 3. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #3
  Apr 20, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  kazi kweli kweli
   
 4. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #4
  Apr 20, 2011
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,638
  Likes Received: 1,427
  Trophy Points: 280
  okaaaaaaaaaaay!
   
 5. CHIMPANZEE

  CHIMPANZEE Member

  #5
  Apr 20, 2011
  Joined: Mar 30, 2011
  Messages: 98
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  Huyu paroko hajui kama siasa ni propaganda?
   
 6. The Prophet

  The Prophet JF-Expert Member

  #6
  Apr 20, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 682
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  huyo paroko atakuwa alibadilisha dini ikiwa kama unachokiwaza wewe ndicho anakiwaza yeye.
   
 7. Mlangaja

  Mlangaja JF-Expert Member

  #7
  Apr 20, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 541
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Maelezo ya padre Maganga ni mazuri sana, lakini hitimisho lako ni bovu zaidi ya mahitimisho niliwahi ona tangu mwaka huu uanze. Kupakana matope ni tamathali ya usemi maana yake ni kusema mambo mabaya ambayo yanachafua sifa nzuri ya mtu mwingine. Mzabitu hazaa zabibu, na mwiba huzaa miiba. Mtu mbaya huzaa mabaya, na mtu mzuri huzaa mazuri. Ufisadi ni matunda ya tabia mbaya ya kufisadi mali za wananchi. Kutoa taarifa za ufisadi ni tambia nzuri. Slaa ametoa taarifa za mafisadi, kwa hiyo Slaa ni mtu mzuri.
  Mtu anayemhukumu mtu bila kueleza makosa yake huyo ni hakimi mbaya. Thithiem wamewahukumu wajumbe wa secretarieti bila kutoa taarifa za makosa yao. Kwa hiyo thithiem ni mahakimu...........
  Naamini utakuwa umemwelewa Maganga sasa.
   
 8. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #8
  Apr 20, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Mkuu naona utaki kuamini kama Paroko kasema hayo maneno kwa kukusaidia tu tafuta Gazeti la Mwanachi la tarehe 20, 2011, ukurasa wa nane usome, mimi tena nime-Quote kwa ufupi tu sijaongeza neno lolote wala kupunguza neno lolote ndio maana chini kuna Source nimeweka
   
Loading...