Papick kutimkia kwao Serbia

Kijamani

Senior Member
Nov 10, 2009
159
9
Upo uwezekano mkubwa kwa kocha wa sasa wa klabu ya Yanga Kostadin Papick kutimkia kwao Serbia.Hizi ni habari za ndani mno na siri kubwa ambayo imetolewa na mtu wa karibu sana wa Papick ambaye yupo Afrika ya kusini.

Hii ni kufuatia kocha huyo kutakiwa na klabu moja ya daraja la kwanza nchini kwao. Chanzo hicho kiliendelea kutanabaisha kwamba anachosubiri kwa sasa mwalimu huyo ni makubliano ya malipo na timu hiyo.

Kocha huyo ambaye ameingia yanga ambayo kwa sasa ipo katika wakati mgumu wa matokeo yasiyo ya kuridhisha amekatishwa tamaa na mfumo ambao ameukuta klabunui hapo. Hata hivyo bado Papick ana kazi kubwa ya kusitisha mkataba wake mpya na klabu yake ya Yanga.
 
Chanzo hicho cha siri cha ndani ndo kipi?...Ni siri gani hii hapa tena?
 
Wewe utakuwa mtu wa simba,unataka kutuvuruga sasa,kama kutufunga tayari sasa subiri round ya pili upate kipigo.5-1
 
Back
Top Bottom