Tipstipstor
JF-Expert Member
- Nov 29, 2021
- 1,531
- 3,331
Ahlanbik kutoka Lombardia ndani ya jiji la Bergamo kaskazini mwa nchi ya Italy:
Jana nlifanikiwa kuitazama mechi ya miamba ya soka nchini Tanzania ,Simba dhidi ya timu ya Geita Gold nikiwa hapa Italy kupitia Azam max, niseme tu pongezi ziwaendee Azam kwa kutuwezesha diasporas tulioko huku ughaibuni kuweza kuburudika na soka la nyumbani kwetu Tanzania. Ukiacha kuwa mshabiki mkubwa wa timu kubwa ya hapa jijini kwetu Bergamo, Atalanta Bergamasca Calcio (Atalanta B.C), bado nimeendelea kuwa mshabiki kindakindaki (die hard fan) wa Simba Sc. Naamini simba ina potential ya kuja kuwa timu kubwa kabisa Africa na duniani kwa ujumla.
Katika kuicheki hii mechi ya simba dhidi ya geita gold, nimegundua jambo moja kumhusu bwana mdogo Sakho, raia kutoka Senegal. Sakho ni mchezaji mzuri na ikiwa atatuliza akili na kuwekeza juhudi uwanjani basi anauwezo wa kufika mbali sana. Ila nilichokiona toka mwisho wa msimu uliopita ni kuwa bwana mdogo huyu ameanza kulewa sifa , simuoni yule Sakho aliyekuwa na uchu kutokea timu ya teungueth ya pale Senegal.
Sakho siku hizi amekuwa haeleweki anachokicheza uwanjani, amekuwa anajali zaidi kelele za wakaanga chips jukwaani (mashabiki) wanavyomshangilia pale anavyopigapiga chenga huku akisahau majukumu yake kiwanjani. Kwa wanaomfahamu kocha Zoran Maki wanajua kuwa huwa hana ujamaa na mchezaji yeyote hata kama unasifiwa au kukubalika na mashabiki.Mtakuwa mashahidi pale alipomtoa Jonas Mkude kabla ya hata kuisha kipindi cha kwanza. Zoran hahitaji mbwembwe nyingi kiwanjani.Falsafa yale inahitaji mchezaji awe na kasi akiwa na mpira au hana mpira, pia kucheza direct football basi.
Kwa sakho ,mafanikio ya kupewa tuzo ya goli bora yameanza kumdanganya na kujiona kuwa ameshakuwa mchezaji mwenye uhakika wa namba pale simba, nimwambie tu kuwa kwa kocha huyu hakuna mwenye uhakika wa namba pale simba , ukimzingua tu anakuzingua.Game kadhaa sasa zinlmepita sioni successful dribbles (take-ons) kutoka kwa sakho, sioni assists na kiwango chake cha complete passes kimeshuka pia. Anaingiza mambo mengi kwenye aspect of his game badala ya kucheza basic football tu. Akumbuke kuwa benchi la simba lina wachezaji wengi wazuri kama kina Okwa ambao wanafanya juu chini kumshawishi kocha ili wawe sehemu ya first eleven. Waliokaribu na kijana Sakho wamwambie tu kuwa abadilike aache ubinafsi wa mafanikio yake binafsi na badala yake acheze kwa ajili ya timu. Pia apunguze kila muda kutaka kuwa na mpira kitendo kinachomfanya kushuka sana chini kuja kufata mpira na kuanza kupiga chenga kijiji cha wachezaji wa timu pinzani. Atulie juu eneo la umbali wa 40yard kutoka katika goli la timu pinzani ili mipira imfate yeye na si kazi yake kuja kuifuata mipira nyuma.