Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,276
View attachment 381365Papa Francis kiongozi mkuu wa kanisa katoliki duniani amekaa kwa zaidi ya saa moja na makahaba waishio nchini Italia ambao walisafiri kutoka nchi mbalimbali duniani.
Papa mwenye umri wa miaka 79 amekuwa akikemea vitendo vya kutoka taifa moja kwenda lingine ili kuwatumikisha katika biashara za ngono.
Akiwa na wanawake 20 waishio katika moja ya jengo linalomilikiwa na kanisa katoliki katika mji mkuu wa Italia, kiongozi huyo akizungumza na wanawake hao akitaka kujua namna walivyoingia biashara hiyo haramu.
Wanawake hao wenye umri unaokadiriwa kuwa kati ya miaka 30 walitekwa na mwanamme mmoja, miongoni mwao wapo wanaigeria saba, waromania sita, na wengine wanne kutoka Albania, huku watatu wakitoka Italia, Tunisia na Ukraine.
Aidha, wamekiri sababu ya kubwa inayopelekea kwenda huko ni ajira ambapo wafanyabiashara Italia na nchi nyingine kutoka mataifa ya ulaya huwachukua kwa kuwaahidi kuwapa kazi na wakifika huko hulazimishwa kufanya ukahaba.
Papa Francis amewatia moyo makahaba hao wenye nia ya kuachana na biashara hiyo, wanapoanza maisha mapya kwa usaidizi wa kituo cha Papa Yohana wa pili.
Chanzo :Mpekuzi blog.