Papa Francis aosha miguu ya Waislam

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
52,816
117,356
Mkuu wa kanisa katoliki duniani Papa Francis ameosha miguu ya wahamiaji waislamu
mjini Rome katika tukio la unyenyekevu linaloambatana na itikadi ya kuanza kwa msimu wa Pasaka.

Papa Francis alitembela makao ya wahamiaji, mjini Roma na kuendesha misa ya kuanza kwa
msimu wa pasaka. Ziara yake katika kituo hicho cha kutathmini uhalali wa wahamiaji cha (Castelnuovo di Porto), inawadia huku uhasama na taharuki ikienea kote barani ulaya kuhusiana na kuwepo kwa wahamiaji waislamu hususani kufuatia mauaji ya Paris mwezi Novemba na ya hivi punde huko Brussels Ubelgiji. Papa Francis alikashifu mauaji yaliyotokea Ufaransa na Ubelgiji akisema kuwa hizo ni njama za watu wenye kiu cha kumwaga damu ya binadamu.

Kiongozi huyo wa kanisa katoliki duniani alilaumu mtazamo wa watuhumiwa hao kuhusu maafa waliyosababisha.

Aidha papa mtakatifu aliwashauri watu wa dini tofauti duniani kuishi kwa amani.
''Haijalishi iwapo tunaimani tofauti la muhimu kwetu sote ni tuishi kwa amani sisi ni ndugu
alisema papa mtakatifu.
 
Papa aonyesha unyenyekevu na kujishusha km alivyofanya kristo mwenyewe!
pasaka njema

1458886359823.jpg
 
Asante kwa ujumbe murua kabisa huu,Hakika Papa Francis ni Kiongozi wa mfano tena wa kuigwa kutokana na Unyenyekevu wake,pia juu ya Mtazamo wake wa Huruma ya Mungu;Mungu azidi kumjalia Hekima,Busara na Unyenyekevu na Maisha Marefu.

Hamna cha unyenyekevu hiyo ni PR 101....jamani sometimes we should see things beyond surface value...
 
Abarikiwe papa francis kwa kuwaosha miguu watu wa imani tofauti,ni jambo jema kabisa.

Kuosha miguu ndio kutatua matatizo ya kibinadamu au ni maigizo?

Baba Mtakatifu nani kasema?Ni wanadamu wenzake wamemwita "baba mtakatifu",basi hilo jina naweza nisikitambue na nikawa sahihi
 
Kama inasaidia kuleta amani mbona watu wote tutawaosha miguu hata mimi wakija kwangu nitawaosha tu ili kulinda amani
 
Naona maandalizi yanakwenda vizuri. Kiongozi pekee wa dini, ambaye anajulikana hata kwa wasio wa imani yake, wakati huo, unakuta mtu hamjui kiongozi wa imani yake ila wa ukatoloki anamjua. Kweli Mungu(kupitia biblia), hakukosea.
 
Maigizo yanaendelea, c naskia huyu jamaa, ni mmojawapo ya members of secret society???
Nauliza tuu
 
Kuosha miguu ndio kutatua matatizo ya kibinadamu au ni maigizo?

Baba Mtakatifu nani kasema?Ni wanadamu wenzake wamemwita "baba mtakatifu",basi hilo jina naweza nisikitambue na nikawa sahihi

Mbona unapanick... Endelea na shughuli zako nyingine...
Ukiona kitu hujakielewa jua hakikuhusu...potezea tu kaka
Ya Waroma waachie waroma...
 
Back
Top Bottom