Papa Francis amesema Trump sio Mkristo

hazole1

JF-Expert Member
Jan 3, 2015
4,319
3,916
Mkuu wa kanisa katoliki duniani Papa Francis amesema kuwa wazo la mgombea wa kiti wa chama cha Republican nchini Marekani, Donald Trump la kujenga ukuta kati ya Mexico na Marekani si la kikristo.

Papa Francis alisema kuwa kwa mtu yeyote ambaye katika karne hii ya 21 anayetaka kujenga ukuta badala ya kujenga daraja huyo si Mkristo.
Kiongozi huyo wa kanisa katoliki aliyasema hayo katika siku yake ya mwisho ya ziara nchini Mexico.

Trump ambaye anapigiwa upatu kutwaa tiketi ya chama cha Republicans katika uchaguzi mkuu ujao amependekeza kujenga ukuta na ua katika mpaka kati ya nchi yake na mexico ilikuwazuia wahamiaji kuingia nchini Marekani

Trump amesema kuwa papa Francis hana haki yeyote kumhukumu iwapo ni muumini au la.

Na suala la kujenga ukuta sio la kikristo
 
..sioni kama huyo Trump anaweza kuwa Rais wa marekani,amekosa hekima inayotakiwa kwa kiongozi mkubwa wa taifa km la marekani.
 
Mkuu wa kanisa katoliki duniani Papa Francis amesema kuwa wazo la mgombea wa kiti wa chama cha Republican nchini Marekani, Donald Trump la kujenga ukuta kati ya Mexico na Marekani si la kikristo
Papa Francis alisema kuwa kwa mtu yeyote ambaye katika karne hii ya 21 anayetaka kujenga ukuta badala ya kujenga daraja huyo si Mkristo.
Kiongozi huyo wa kanisa katoliki aliyasema hayo katika siku yake ya mwisho ya ziara nchini Mexico.
Trump ambaye anapigiwa upatu kutwaa tiketi ya chama cha Republicans katika uchaguzi mkuu ujao amependekeza kujenga ukuta na ua katika mpaka kati ya nchi yake na mexico ilikuwazuia wahamiaji kuingia nchini Marekani

Trump amesema kuwa papa Francis hana haki yeyote kumhukumu iwapo ni muumini au la
Na swala la kujenga ukuta sio la kikristo
Trump amejibu kwa logic
 
Unamaanisha nini wakati rais wa marekani anajulikana kama "the most powerful man in the world"?
Mimi nimeelewa kwamba, America sauti ya Umma wanaipa kipaumbele, ili kuepusha machafuko nchini mwao yatakayo wapelekea kuporomoka kiuchumi nao swala hili hawalitaki.Lakini mambo ya nchi ya wenzao wanakiherere nayo ili wawaharibie ili wao waendelee kua na sauti.Lakini naamin hawa dawa yao inachemka.
 
trump kwangu nimeona ni mtu mkweli na muwazi ,mm ni mkatoliki kihistoria ila trump kasema hivyo kua siku iss wakipiga Vatican ndio papa ataelewa,pili nasikia Vatican nayo imezungushiwa ukuta ndani ya italy japo sina hakika
 
kwa tatizo la madawa ya kulevya Trump yuko sahihi kujenga ukuta tatizo Trump sio mnafiki anayesema maneno mazuri ili achaguliwe yeye anasema kile anachoamini kusudi kama mkimchagua mjue ni mtu wa namna gani
 
Back
Top Bottom