Panya wanamaliza mazao yangu, msaada tafadhali

Crocodiletooth

JF-Expert Member
Oct 28, 2012
20,057
23,510
Nimejitahidi kumaliza panya hawa lakini naona inakuwa KAZI ngumu sana,
kwani wanakula mazao chini kwa chini unachokuja shtuka ni mmea unadondo tu.
Ufumbuzi tafadhali.

Natamani nipate mlinzi wa shamba toka kusini kwa nimepata fufunu kuwa wanyama huweza kuwa kitoweo murua.
 
Kuna wataalamu wa kukamata panya na fuko.. Yawezekana hao ni fuko aisee ni wasumbugu balaaa
 
Ni mazao gani mkuu uliyokuwanayo? Vipi kuhusu madawa ya kuua panya wanaita"bait" ulishafuatilia katika maduka ya kilimo Na mifugo!
 
Ni vema ungesema umelima nini lakini chimbia ndoo za plastic mpaka ziwe flat na ardhi kisha weka pumba kidogo kabisa ndani yake ili usijepandisha level ya ndoo panya akiingia kwakufuata pumba hawezi kutoka hivyo itakusaidia kuwapunguza pia.
Hivyo endelea kutumia Suma pamoja,mitego pamoja na hizo ndoo
 
hiyo yandoo za Plastc ni muafaka weka pumba changanya na dagaa utaona ukweli inafaa sana
 
chukua mabak ya chakula yawekee ile dawa ya mifupa inaitwa endosid( mtanisahihisha kama nimekosea spelling) hao panya week tuu hakuna hata mmoja na hua wanahama
 
chukua mabak ya chakula yawekee ile dawa ya mifupa inaitwa endosid( mtanisahihisha kama nimekosea spelling) hao panya week tuu hakuna hata mmoja na hua wanahama
Duuh! Mpaka kufikia kutumia sawa ya mifupa ilikuaje mkuu... Na ukishawawekea huwa wa Wanakufa au vipi
 
mleta mada,mkuu biological control ya nyoka ni nzuri sana niliona wanaitumia wazungu kule nachingwea, mtwara sababu panya walikua wanakula sana karanga wale wazungu wakafunga nyoka hakuna panya aliyekatiza, ni nyoka wapole wasiodhuru binadamu hata ukiwachokoza
 
Back
Top Bottom