Panya wa Sokoine kutumiwa Ethiopia

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,807
34,193
130226041317_landmines_rat_apopo_624x351_bbc_nocredit.jpg

Panya wa Apopo walifanikiwa kugundua mabomu yaliyotegwa ardhini Msumbiji na Angola

Wanasayansi katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine nchini Tanzania wanapanga kuwatuma panya waliopokea mafunzo kwenda kutumiwa kugundua kifua kikuu nchi za nje.

Panya hao, ambao awali walitumiwa kugundua mabomu yaliyoachwa chini ya ardhi, kwa miaka kadha sasa wamekuwa wakitumiwa kugundua watu wanaougua kifua kikuu sana katika magereza na viwandani.

Panya hao, ambao kiteknolojia hujulikana kama panya wa SUA-APOPO, wamebainika kuwa hugundua visa vya maambukizi ya kifua kikuu haraka na kwa ufasaha.

Panya hao hudaiwa kuwa na uwezo wa kupima sampuli 140 za makohozi kwa dakika 15 tu, wakati mtaalamu wa maabara aliyebobea huweza kupima wagonjwa 25 kwa siku.

Awali, walitumiwa Tanzania na Msumbiji pekee.

Lakini sasa chuo kikuu hicho kinapanga kuwapeleka Ethiopia na Bangladesh wakatumiwe huko.

Ethiopia ni moja ya nchi zilizotatizwa zaidi na aina ya vijidudu vya kifua kikuu visivyosikia dawa.

Bi Mariam Juma, mmoja wa wanasayansi katika chuo hicho, amenukuliwa na gazeti la Daily News la Tanzania akisema kwamba kutafunguliwa pia kituo jijini Dar es Salaam.

Akihutubia wanahabari katika maonesho ya biashara ya Dar es Salaam, Bi Juma alisema maafisa pia watawahimiza watu kujipima kujua hali yao.


Chanzo: BBC Swahili
 
Hichi ndicho chuo bora kabisa Tanzania. Serikali ikiwekeza kwenye Research basi hichi ndani ya miaka 10 tutakuja ongea mengine.

Tatizo UDSM umeharibu sana elimu hapa nchini. Lichuo lile bwana!
 
udsm usharobaro mwing umarekani tele bata za maana hakuna ata any innovation ya nguvu...congltion SUA
 
Back
Top Bottom