Panya Road, tunahitaji kufumua Jeshi la polisi?

Panya Road, tunahitaji kufumua Jeshi la polisi?

Nyie kama wananchi wa eneo hilo mnafanyeje kudhibiti wasirudi tena.

Polisi hawatoshi kulinda kila sehemu.
 
Sungusungu walikuwa wapi huo muda? Halafu mtu aje kwangu aniambie hela ya sungusungu aki atanitambua hyo siku
 
Wabongo mtu unajenga nyumba unashindwa kujiongeza kuwa na chumba cha siri a.k.a panic room au hata bunker?tahadhari ni muhimu maana serekali imeshindwa kulinda raia na mali zake.
Niliona movie ya panic room mama alijifungia na mwanae. Majambaz yalikuja yamekaa mle ndani masaa mengi yanahitaji kufungua safe wachukue milions za dollar.
 
Daah nikikumbuka jamaa yetu alivyoambiwa achague bokoboko au pilau.Na kwa kuwa alikuwa vyombo akachagua pilau tena lenye kachumbari nyingi.Nasema panya road wote walazwe chini.
 
Hao panya sijui upupu.. Nadhan bora wangekufa kifo kingine sio kukamatwa.

Hamtaamini kama mpo Tanzania. Waambieni vijana wale viduku wajichunge.

Juzi kulikuwa na wito wa mafunzo ya kilimo dodoma mbona sijasikia hata kijana mmoja akizungumzia?

Ukiwakuta kijiweni ukawauliza wanakwambia ndio kwanza wamesikia. Heee! Barua iko mtandaoni mwezi mzima wanashangaa. Wanataka wakimbize boda tu. Na kunywa energy. Wakimalza wakajaze wanafunzi mimba. Ndio life cycle yao.

Mm nina mzigo mkubwa na vijana ila bas tu. [emoji26]
 
Hizo siyo level za wanaovamiwa na Panya road,mnaangalia sana movie,panic room ni akina Mo Dewji na marehemu Mengi.Wewe ulipokulia kulikuwa na panic room na bunker?
Huyo ni mjinga sana anaongea haya akiwa amekulia kwenye nyumba ya vyumba vitatu kimoja Cha baba na mama, kimoja cha wanaume wote na kimoja Cha wanawake wote hiyo bunker ni stop ya kuni ipo nje huko halafu anakuja analeta ujuaji humu ingali kwa sasa amepanga rum moja buza.
 
Wabongo mtu unajenga nyumba unashindwa kujiongeza kuwa na chumba cha siri a.k.a panic room au hata bunker?tahadhari ni muhimu maana serekali imeshindwa kulinda raia na mali zake.
Panic room kwaajili ya kujificha na familia yake, sivyo?
 
Hawa watu adhabu yao ingekuwa moja tu, shaba...
 
Panic room kwaajili ya kujificha na familia yake, sivyo?
Ndio,mlango unakuwa wa siri kama kabati hivi,au bunker mnaingia underground,wao wakija wachukue wanachotaka ila nyie mbaki salama!
 
Back
Top Bottom