Panya road tiba ya ndoa Dar.

Panya road tiba ya ndoa Dar.

Molembe

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2012
Posts
9,933
Reaction score
11,865
Kati ya vitu ambavyo wanawake hawapendi ni mwanaume kurudi nyumbani usiku mawazo yao hufikria mwanaume alikuwa anachepuka, sasa jana wanaume wamerudi mapema kabisa nyumbani kitendo ambacho kimewafurahisha wanawake wengi.
 
basi mapanya road wapewe katangazo kama wapambanaj wa michepuko
 
Hii si habari njema kwa wanausalama wetu ( police & Usalama wa Taifa), Hizi ni dalili za Kushindwa kulinda raia na mali zao.

Haiwezi ingia hakilini kama Watu wataunda vikundi vya uporaji na kufanya watakavyo kila kukicha, leo wamekatisha shughuli za Kiuchumi, wamepora mali za walipa kodi na wameumiza na Kuuwa watu.

Hata Nigeria lile kundi la Boko Haram lilianza kwa style hii tunayoiona kwa kundi la Panya road; Kimsingi wanausalama wetu wamelala lakini siyo siri watajikuta wamechelewa kwa maana kundi hili lilikuwa ndogo tu hapa maeneo ya kipawa na vingunguti lakini kwa sasa linaonekana kutamalaki na kuwa na nguvu kubwa.

Panya roads kinachowasukuma kufanya vitendo vya uporaji na ukabaji si tofauti na kilichosababisha kuibuka kundi la Boko Haram na lile na al-shabaab. Kundi fulani likisaulika madhara yake ni makubwa" The marginalised group kwa sasa ni Vijana wasio na kazi wakati wanaujuzi.

Tatizo si kitu kingine bali ni Kundi la vijana waliosoma secondary za kata wamesahulika katika furusa za kiuchumi na Kipato cha kujikimu maisha ya Kawaida.
Serikali ya nigeria ilipowapa kisogo Vijana wa kasikazini kundi la Boko haram liliibuka.Pia serikali isipowapa kipaombele vijana wanaomaliza form four shule za kata madhala yake ni makubwa.

Serikali inayowapa Vijana wake mafunzo ya Kijeshi (JKT) na baadae inawaambie wakajiajiri mtaani, je unategemea nini hapo?, Vijana hao wengi wao nadhani wanakuwa wamepitia mafunzo ya JKT na wanachokikosa ni Salaha tu, madhara yake yangekuwa na wakizipata yatakuwa makubwa.

Mwaka jana November'2014, wote tuliona kundi la vijana waliohitimu mafunzo ya JKT, wakijaribu Kuandamana huku wakidai ajira. Hii ni hatari sana kama mwanajeshi anapata ujasiri wa kuandamana wakati amekula kiapo. Wanausalama wawe makini.

Vijana wapewe kipaumbele ktk Taifa hili vinginevyo akatokea kundi kupata wafadhili wenye kuwapa support ya Kutosha, basi khali ya Kiusalama itakuwa ni tete.

Ni kazi ya wanausalama watu wanaolipwa kwa Kodi zetu kutuakikishia usalama wetu, lakini pia mali zetu ; Vinginevyo hali hii haiwezi kuvumilka tutawataka wahusika wakuu Wajipime na Kuachia ngazi B4 is too late.

Hili Kundi la "PANYA ROAD" Ni kama limewazidia nguvu Wanausalama wetu, ambao muda wao mwingi wamekuwa wakifikiria Kupambana na wanasiasa wa Upinzani.

Kimsingi Wanausalama wetu wamesahau/ wameacha kazi yao ya kimsingi na Kujiongezea za kisiasa ambazo ni changamoto kubwa kwao.

Kundi Hili lisiposhughulikiwa kwa sense of Urgency na Umakini Madhara yake ni Makubwa .
 
Hii si habari njema kwa wanausalama wetu, Hizi ni dalili za Kushindwa kulinda raia na mali zao. Haiwezi ingia hakilini kama Watu wataunda vikundi vya uporaji na wakaendelea kukatisha shughuli za Kiuchumi huku wanausalama wakijinasibu wamewadhibiti vibaka hao.

Hata raia wa kawaida wanapaswa kulaumiwa hao panya road wanakaa nao kwanini wasiwashughulikie.
 
Sidhani kama watu wamerudi mapema jana. kwa sababu utapitia wapi kurudi hiyo mapema. Sema labda watu wamejivutia kiulani kwa wale waliokimbilia kwenye nyumba za watu kuomba hifadhi mpaka upepo upite.
 
Back
Top Bottom