Panya Dume

Pilipilihoho

JF-Expert Member
Jan 29, 2016
202
145
Profesa mmoja alikuwa anafanya utafiti wa kisayansi juu ya nguvu ya chakula dhidi ya ngono. Akaanza kwa kufanya majaribio ya panya. Alimfungia panya dume katika kibanda chake kwa muda bila kumpa chakula kizuri. Siku hiyo akawaita wanafunzi wake ili awaoneshe uvumbuzi wake.

Mara ya kwanza alichukua kipande cha keki akakiweka upande wa kulia na upande wa kushoto akamweka panya jike lakini yule dume alikimbilia kipande cha keki kukila.

Akarudia kwa mara ya pili na kuweka kipande cha mkate upande mmoja na mwingine akamweka yule panya jike pia dume yule alikimbilia kipande cha mkate.

Maya tatu, profesa akaweka vipande vya dagaa upande mmoja na mwingine akamweka yule panya pia dume akakimbilia vipande vya dagaa.

Baada ya majaribio hayo akawaambia wanafunzi wake, “mnaona sasa? Chakula ni bora kuliko ngono ndiyo maana huyu panya mara zote kakimbilia chakula.”

Mwanafunzi mmoja akasema, “profesa, unaonaje tukimbadili panya, pengine huyu ni mke wake!”
 
Back
Top Bottom