Panone hali ni mbaya.....

Panone hali ni mbaya.....

M4C ARUSHA

Member
Joined
Apr 27, 2012
Posts
38
Reaction score
4
HATIMAYE wafanyakazi wa kampuni ya kusafirisha na kuuza mafuta ya jumla na reja reja Panone and company limited wamejikuta wakiumaliza vibaya mwaka 2012 na kuukaribisha mwaka mpya 2013 wakiwa katika hali mbaya ya kiuchumi huku mmiliki wa kampuni hiyo akijenga maghorofa mithili ya uyoga jicho la m4c linakutiririshia habari kamili.


Kwa mujibu wa vyanzo vya habari vyenye kuaminika vimeeleza kuwa ndani ya uongozi wa kampuni hiyo yaani panone and company limited kumekuwa na madaraja ya watumishi ambao ni wakenya na wazawa yaani watanzania huku malipo ya mishahara ikiwa ni tofauti tofauti huku mishahara ikizidi kushuka kila kukicha hususani kwa wazawa.


Wafanyakazi kutoka vituo vya Tunduma mkoani mbeya dar es salaam ARUSHA manyara kiteto na Kilimanjaro wamekumbwa na dhahma hiyo ya kushushwa kiwango cha mishahara huku ya wageni ikibaki pale pale kwa kigezo kuwa kampuni haina hela.


Vyanzo hivyo vya habari vinafafanua kuwa mmiliki wa kampuni hiyo (jina tunalo)amekuwa jeuri sana hataki kusikiliza wafanyakazi kila wanapotaka kukutana nae na amekuwa akiwataka waache kazi na badala yake aajiri wafanyakazi kutoka nje kwani wazawa wao ni maneno maneno.


Chakusikitisha zaidi ni kuwa pale wafanyakazi walipoenda ofisi ya utumishi kitengo cha idara ya kazi katika mikoa tofauti tofauti lakini inasemekana mmiliki wa panone tayari alishapita huko na kumalizana na wakubwa hivyo ni sawa na kazi bure


Katika kudhihirisha hilo baadhi ya wafanyakazi wamekuwa wakilipwa bila kufuatwa kwa taratibu za ulipwaji wa fedha ikiwa ni pamoja na kuzipitisha benki ili mapato ya nchi yapatikane ambapo taarifa za ndani meneja mkuu Genestio Sombemshahara wake ni zaidi ya milioni tano mkaguzi wa ndani bwana J KIRAI mshahara wake ni milioni nne na laki nane.


Watumishi wa kitanzania ambao wamefanya kazi zaidi ya miaka mitano wamekuwa wakilipwa kima cha chini cha shilingi 80000 hadi 120000 kitendo ambacho ni kinyume na sheria ya shirikisho la vyama vya wafanyakazi nchini tucta.
Kwa mujibu wa meneja mkuu baada ya m4c kumdodosa amekiri na kuomba habari hizi zisifike sehemu yoyote kwani anamwonea huruma bosi wake kutokana na biashara anayoifanya anakwepa ushuru mkubwa sana wa serikali kwa kisingizio kuwa kampuni ni ya wakubwa huku akijidai anasambza mafuta nchini kumbe yanapelekwa nje ya nchi kama Rwanda,Kenya na drc hali kadhalika Zambia


“najua mna nia kweli ya kuwatetea watazania wenzenu ila oneni hayo maghorofa yanavyoota mtafuteni mmalizane nchi yenu si ya kitu kidogo?’alisema bwana Sombe Meneja mkuu
Kwa mujibu wa taarifa za ndani zaidi zinaonyesha kwamba ana mkopo katika benki mbali mbali lakini utajiri wake una mashaka kwani mikopo hiyo haiendani na uatajiri alio nao wakutisha hapa naomba vyombo husika viingilie kati yaani usalama wa taifa takukuru na tra .
 
Kiwango cha mshahara hufikiwa kwa makubaliano baina ya mwajiri na mwajiriwa. Hata ndani ya CHADEMA makao makuu kuna tofauti kubwa ya mishahara; Dr. Slaa analamba milioni 12 kwa mwezi wakati dereva wake analamba elfu 80 kwa mwezi
 
Hii Kampuni inatia shaka kwani ukianzia Shangarai, Kingori , mailisita na maeneo mengine tusiyoyajua PANONE inapandisha mighorofa ya kufa mtu sijui anapata wapi hela ya mteremko kiasi hicho. Kiukweli inasemekana yuko na RIZ-1 na wana malori ya kufuru ya kubeba mafuta
 
Kama hali ni mbaya mbona tukiomba kazi panone anatujibu nafasi hakuna, kama kuna magari yamepaki tuchangamkie?
 
Ngiloiiiiiiiiiiiiiii .... Si wanasema na Prince naye yumo
 
Ukiacha hilo la kuwa na mishahara iliyo chini ya kima cha chini..nadhani hayo mengine ni makubaliano kati ya mwajiri na mwajiriwa..

Wakati mwingine
Wakati mwingine watanzania tunalalamika sana bila kuangalia kama tunatekeleza wajibu wetu wa kazi pia..hata mimi ningekuwa mmiliki wa hiyo kampuni nisingeajiri watanzanaia kwa sababu ya utanzanaia wao, bali kwa sababu ya uwezo wao wa kuchangia maendeleo ya kampuni..tuonyeshe uwezo wetu watanzania..tuache kulalamika.
 
Kiwango cha mshahara hufikiwa kwa makubaliano baina ya mwajiri na mwajiriwa. Hata ndani ya CHADEMA makao makuu kuna tofauti kubwa ya mishahara; Dr. Slaa analamba milioni 12 kwa mwezi wakati dereva wake analamba elfu 80 kwa mwezi

Everything now is about CHADEMA..........what a benchmark to use!
 
Huyu jamaa kaanza biashara ya mafuta karibia miaka 20 iliyopita labda Riz 1 akiwa darasa la nne.Kwanini ashindwe kufanya hayo anayofanya mpaka hasubiri msaada wa Riz one?
 
[/SIZE]]Kiwango cha mshahara hufikiwa kwa makubaliano baina ya mwajiri na mwajiriwa. Hata ndani ya CHADEMA makao makuu kuna tofauti kubwa ya mishahara; Dr. Slaa analamba milioni 12 kwa mwezi wakati dereva wake analamba elfu 80 kwa mwezi


Sasa shida ni nini ?
 
kwanza hayo siyo malalamiko ni taarifa tu au kwa kuwa first born wa mh yupo hapo kazi ya utafiti kupitia vyombo husika haitafanyika hata hivyo taarifa ni mchangiaji mkubwa kwa kile chama cha gamba ila kwa sasa amehamia upande wa pili wa shilingi baada ya kuona free 1961 ambaye ni kaka yake anaongoza kile chama kiumakini ameamua kumsaidia baada ya kuambiwa na 1riz ambaye ndiye mshirika namba moja katika kuuibia hii serikali iliyopo katika himaya yao kwa kushirikiana na kampuni ndogo ndogo kama iliyopo kifaru kule mwanga ambayo ni ya mchumi wa ccm wilaya ya mwanga
 
Back
Top Bottom