Ngwananzengo
JF-Expert Member
- Jul 28, 2012
- 1,911
- 1,314
Kheri ya Noeli kwa wana familia wa jamiiforums. Tuombeane kheri ili panapo Majaliwa ya Mwenyezi Mungu tuone mwaka ujao.
Kama wahenga walivyosema, "ukubwa dawa". Kuna ndugu na rafiki yangu kaja kwangu akihitaji ushauri. Alilikoroga akalinywa lakini sasa tumbo linamvuruga. Naomba niwafahamishe kisa mkasa hiki ili tuone jinsi gani tunaweza msaidia.
Ndugu yangu huyu ambae ni mume wa mtu tena mwenye ndoa Takatifu na watoto juu aliteleza akaanguka. Kuna wakati alianzisha mahusiano na mchepuko. Kama ilivyo Ada penzi ni upofu akajikuta kazama mzima mzima. Penzi likanoga na kukolea, alipokuja kutahamaki tayari mchepuko ulikuwa na ujauzito.
Hapo ndipo akili ikamrudia na kukumbuka yeye ni mume wa mtu na baba wa watoto. Kama ilivyo Ada hakuna jambo lenye kukera ndani ya ndoa kama mume kuzaa nje ya ndoa. Akaanza kuhaha ili kuona ni kwa kiasi gani analitafutia ufumbuzi suala hili.
Hakuchi Hakuchi mwisho kunakucha, mchepuko Mungu akaujalia ukajifungua salama. Baada ya kujifungua jamaa akakaa kikao na mchepuko ili kuona nini kinafanyika. Maazimio ya kikao yakaamua ni wakati muafaka wa kufikia tamati kwenye uhusiano wao. Pili, jamaa aone nini kifanyike ili kuona mtoto analelewa.
Jamaa akahangaika huku na kule na kumpatia mzazi mwenzie millioni kumi na tano ili afungue shughuli yenye kumwongezea kipato kwa ajili ya malezi ya mtoto. Miaka mitatu tayari imepita tangu jamaa atoe hela, kinyume na matarajio yake mzazi mwenzake hana alichofanya. Sasa anapita kwa marafiki, ndugu na jamaa akilalama katelekezwa. Hapewi hela ya matumizi kwa ajili ya mtoto.
Jamaa yangu kichwa kinamuuma, alijua Tanzania ni kama ulaya ukiingia makubaliano na mtu basi makubaliano hayo hudumu. Binafsi nimemwomba anipe nafasi nitafakari kwanza na baada ya sikukuu hizi kupita nitampa ushauri wa ni kifanyike. Nawaomba ushauri wandugu juu ya mkasa huu.