Pamoja na siasa zetu tujue Corona ipo

eddy

JF-Expert Member
Dec 26, 2007
15,051
9,975
Mungu ametunusuru na hili gonjwa la ajabu, sio tu korona kipindupindu surua tetekuwanga kaswende na mafua navyo vimetokomea. Sasa hivi ni adimu kumwona hata mtoto anamafua, ukipiga chafya watu wanaweza pitia madirishani kukukimbia.

Sasa hawa jamaa zetu wasaka kura sijui udhamini hawana tahadhari kabisa wana andaa mikusanyiko hawavai barakoa hawana sanitizer hawana maji ya kunawa yaani hovyo tu. Ipo haja ya wizara ya afya kukaa na tume ya uchaguzi kuweka taratibu na kanuni za afya kipindi hiki cha kampeni.

Napendekeza yafuatayo;

1. Iwe marufuku mtu kuhutubia watu bila kutoa mpango wa afya ya kinga kwa mganga mkuu wa eneo husika, mfano kuwepo kwa ndoo na sabuni za kunawa, washiriki wa misafara wanaozunguka kutoka eneo moja hadi jingine wawe na barakoa, eneo la kuhutubia liwe na nafasi yakuwepo social distancing.

2. Misafara iwe na magari ya huduma ya kwanza ikiwemo mitungi ya oxygen wahudumu wenye sifa na mafunzo stahiki walioidhinishwa na serikali.

3. Wanapovuka mkoa mmoja kwenda mwingine wachukuliwe vipimo vya covid-19 kuhakikisha hawaenezi magonjwa kutoka sehemu moja kwenda nyingine.

4. Wahusika wa hiyo mikusanyiko wavae barakoa na wawe na sanitizer, nimeona mabaunsa wao wakiwa wamejifunga marapurapu midomoni, hapana hatuwezi kukubali mambo ya hovyo namna hiyo, kanuni za afya lazima zizingatiwe, hasa kipindi hiki cha corona.
 
Sasa hayo yote ili kumfurahisha nani na tabu zote hizo za nini?
Kwa sababu maisha yetu kiujumla hayana hizo tahadhari za corona na wala hatufikirii tena suala la uwepo wa corona nchini sasa itakuwa vituko hizo tahadhari zikafanywe kwenye hayo masuala uliyoyaeleza tu halafu mambo mengine yaendelee kama kawaida.
 
Hapo. Umechokoza watawala walioanzisha wimbo:"Korona imekwisha"! Huoni wakati wa kumuaga na kumzika hayati Mkapa, nani alivaa barakoa au kulikuwa na matumizi ya sanitizer?
 
Mungu hajatunusuru bwana. Corona bado ipo. Watu wengi wanaumwa. Ila watu wameaminishwa kisiasa kuwa Corona haipo.
 
Back
Top Bottom