kluger
JF-Expert Member
- Jun 16, 2016
- 2,093
- 1,897
Maisha yamekuwa yenye changamoto nyingi, maumivu mengi yanayosababishwa na kutofikia malengo yetu kama vile ambavyo tumetamani yawe, wanadamu wenzetu wanatufanyia mabaya hawapendi kuona mafanikio, furaha au mazuri yetu.
Lakini tunaendelea kuamini katika mungu na ipo siku moja tutakuwa na furaha tena, wala hatuhitaji kuwa wanyonge zaidi, shetani analeta matatizo kati yetu yaani sasa dunia ni uwanja wa mapambano lakini wenye haki tutakuwa mashujaa.
Hata hivyo tutasonga mbele, kwa maana unatutia moyo, eeh mungu baba ahsante.
Nawapa moyo wale wenzangu wote tunaopitia wakati mgumu kwa namna moja ama nyingine, makazini, biashara, familia zetu, majirani, mahusiano na ndoa. karibuni tupeane moyo, tuamke na kupambana kwa nguvu zote, ushindi upo na ni lazima kwetu!! Usikate tamaa kamwe.Pambana kupata furaha yako.