Pamoja na mashaka tuliyonayo juu ya uhuru wa Mahakama zetu,wapinzani bado hatuitumii Mahakama ipasavyo kupambana na huu unaweza kuwa ni uzembe wetu

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,027
144,382
Ngugu zangu wapenda mabadiliko,leo naomba mtanisamehe kwani wakati mwingine inabidi tuelezane ukweli na ikiwezekana tujisahihishe pale tunapokosea vinginevyo tutabaki kulalamika tu miaka yote.

Ni hivi,wakati tunalalamikia kitendo cha raia mmoja kwenda mahakamani kupinga ukomo wa vipindu viwili vya uraisi,tujiulize sisi wapenda mabadiliko, je, na sisi hatuwezi kwenda mahakamani kupinga tume ya uchaguzi kutokuwa huru kama ibara ya 74(7) ya katiba inavyoagiza?

Je,hatuwezi kwenda mahakamani kujenga hoja kuiomba mahakama iizuei tume hii kuendesha uchaguzi wowote ule mpaka kesi ya msingi tutakayofungua kupinga tume kutokuwa huru itolewe uamuzi na mahakama?

Je, na sisi hatuwezi kwenda mahakamanini na kuiomba mahakama itamke kuwa matokeo ya uraisi kutopingwa mahakamani ni kinyume na matakwa ya katiba yetu inayotambua mahakama kama chombo pekee chenye mamlaka ya kutoa haki(kutafsi sheria)?

Nambo niweke wazi kuwa mimi si mwanasheria na wala si mtaalamu wa mambo ya katiba ila kwa kusoma tu katiba yetu naona bado na sisi tunaweza kwenda mahakamani kupinga au kuhoji baadhi ya ibara za katiba yetu ambazo baadhi ni wazi zina kasoro na zingine hazifai kuendelea kuwepo katka katiba hii inayotambuwa uwepo wa mfumo wa vyama vingi kama vile ibara ya 74(1) inayompa Raisi anaetokana na chama kimojawapo cha siasa kuteua mwenyekiti na watendaji wengine wa tume ya uchaguzi.

Mambo haya nimeyasema sana kupitia hapa JF ila hatushituki hivyo wacheni wenzetu watumie haki yao maana sisi tunajisahau sana.

Na mwisho huwa najiuliza hivi haiwezekani kwenda mahakamani na kuiomba mahakama iagize serikalli kukamilisha mchakato wa kupatikana kwa katiba mpya?

kama tunavyopigania ubunge wa Lissu mahakamanini na kama tunavyopigania mambo mengine kupitia mahakama hizi hizi tulizona na mashaka nazo,basi tufanye hivyo kupigani mambo haya ya msingi yaliyo kikwazo katika swala zima la upinzani kutimiza azima yake ya kushika dola na tukifanya hivi, hata wananchi watuona tuko serious na si watu wa kulalamika tu unless maombi haya ninayoyapendekeza hayawezi kufunguliwa mahakamani(wanasheria mtanisaidia).

Nliowahi kuhoji/kushauri ni haya:



 
kidogo alieka na uthubutu huo alikua ni Dr.slaa hawa wengine kazi kulalamika tu na kwa minajili hiyo mabadiliko tuyasubilie kwanza
 
Laiti kama manyanyaso yote yasiyokua ya kisheria wangekua wanaenda kulalamika mahakamani wala yasinge kuwepo
 
Laiti kama manyanyaso yote yasiyokua ya kisheria wangekua wanaenda kulalamika mahakamani wala yasinge kuwepo
Na usishange wakashinda hiyo kesi ya kuondoa ukomo wa vipindi viwili vya uraisi.

Tukiwa na tume huru,.hata wakiondoa huo ukomo, bado haitawasaidia hivyo na sisi kwa sasa tupiganie tume huru tu.
 
Back
Top Bottom