Pamoja na mapungufu madogo ya Polisi, tuwapongeze wanafanya kazi nzuri sana tusiibeze

britanicca

JF-Expert Member
May 20, 2015
15,647
30,009
Kila nchi ya afrika wanachukia sana polisi wao kisa
1. Kubambikiziwa kesi, unaweza ukakamatwa ukawekewa bangi mfukoni ionekane una makosa,au ukaambiwa unamiliki silaha kinyume cha sheria,

2. Unaweza tozwa faini ya kuzidi kiwango unachotakiwa kutoa hasa kwa nchi majirani, na usiku wanalazimisha uwape rushwa kwa kujifanya wanalinda usalama wanapatikana Kenya hawa kaanjoo,

3. Unaweza pigwa na polisi hata kama huna kesi mambo yatajulikana mbeleni au saa nyingine ukapigwa risasi kabisa wakati uhusiki na uarifu,

4. Wanatumia nguvu kubwa kukamata waharifu badala vya kutumia njia stahiki,

5. Pengine huchukua mali za watu hasa mipakani na askari wa jiji kula chakula Cha mama ntilie,
Hizo ni changamoto ambazo zipo,
Lakin siyo polisi wote wanayapenda hayo, nao wanapitia magumu ambayo raia wa kawaida anapita, wana huruma pia hata ikitokea wakaua bahati mbaya ,uomba nmsamaha kwa familia husika,

Siyo polisi wote ni wabaya wengi wameonekana kutoa ushirikiano katika kulinda raia na usalama wake,

So kila polis anakula rushwa wengine wanaiogopa kama ukoma,

Sio Kila polisi anatumia njia isiyo sahihi kumkabili muarifu wengine wako na adabu,

Tuwapongeze kwa kulinda amani yetu mtaani na kupunguza ujambazi, tuwapongeze kwa ilo
Uarifu na vibaka,utekaji magari, na uvunjaji sheria umepungua kwa kasi, hata polisi wa usalama barabarani wamepunguza sana ajali, pia madawa ya kulevya na vitendo kama hivo vimepungua,

Pia na. sisi tutii sheria bila shuruti

Jioni njema

Britannica
 
hivi kile kituo kikichozinduliwaga pale Biafra kinafanya kazi.ilikiwa kama call center flani hivi au rapid response unit flani.
sijawahi kuisikia wala kusikia ufanisi wake tena.
mkuu tujuze.
 
Polisi wazuri wapo na waovu pia wapo. Ni bora kuwa na jeshi hili la sasa la polisi licha uovu wao kuliko kutakuwa nalo kabisa maana mtaani hakutakalika tutachomana visu na vibaka na majambazi wazi wazi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hivi kile kituo kikichozinduliwaga pale Biafra kinafanya kazi.ilikiwa kama call center flani hivi au rapid response unit flani.
sijawahi kuisikia wala kusikia ufanisi wake tena.
mkuu tujuze.
Siko Tanzania yapata miaka 2 japo nasikia kazi ya polis iko powa na ilo ntalifuatilia,
 
Nakuunga mkono mkono mia kwa mia,
ukitaka kujua umuhimu wao,jiulize mwenyewe
hili swali, "Hivi ikitokea polisi wakagoma,nini kitatokea mitaani?"
Wakigoma na mshahara hawapati familia zao na wait wataishije. Polisi ni mwajiriwa hivyo Ni kazi yake. Wala awaombwi kutulinda. Kama hawataki wagome. Kikubwa wafuate sheria na katiba, wajue hasa mabosi wao wajue katiba inasemaje kuhusu wao. He katiba inaruhusu kuonea watu na kukumbatia chama au katiba inasema walinde raia bila kujali vyama vyao au makabila yao
 
Wakigoma na mshahara hawapati familia zao na wait wataishije. Polisi ni mwajiriwa hivyo Ni kazi yake. Wala awaombwi kutulinda. Kama hawataki wagome. Kikubwa wafuate sheria na katiba, wajue hasa mabosi wao wajue katiba inasemaje kuhusu wao. He katiba inaruhusu kuonea watu na kukumbatia chama au katiba inasema walinde raia bila kujali vyama vyao au makabila yao
Kwani madaktari, wakufunzi na walimu wanaogoma ile siyo ajira?
 
Nakuunga mkono mkono mia kwa mia,
ukitaka kujua umuhimu wao,jiulize mwenyewe
hili swali, "Hivi ikitokea polisi wakagoma,nini kitatokea mitaani?"

Wanataka sana kugoma, ila watakula wapi? Wakiwaza umasikini unaowazunguka hawathubutu. Na watawala kwa kulijua hilo ndio huwatuma hata shughuli zilizo nje ya sheria.
 
Jamani hapa mimi naomba nitoe ushuhuda
kwamba polisi weredi na waadilifu bado
wapo,kuna siku nililetewa zengwe na walinzi
wa benki pale NBC posta ya zamani kwamba
nisipark gari muda wa kupark bado
nikajaribu kujieleza kwamba mimi ni mteja
na nimekuja hapo benki wakakomaa
kwamba nitoe gari maana mabosi wakilikuta wataleta tabu
nikagoma wakasema wanaita break down ilivute
Nikayapiga picha yale magari kama ushahidi
Ndo nikawa nimewasha moto,yule kolokoloni mwenye bunduki akaingilia
kati akaniita mkorofi akaniweka chini ya ulinzi
akaitisha gari likanipeleka central,pale nikakutana
na polisi aliyesomea upolisi,akaelewa hoja yangu
na kuniachia kiroho safi Nikarudi nikadipost hela na kuchukua gari
yangu nikaondoka.Hivyo kuanzia hapo nikaelewa
kuna polisi wanaolichafua jeshi hilo,ila wapo
ambao wanafanya kazi zao kwa weredi mkubwa.
 
Kwani madaktari, wakufunzi na walimu wanaogoma ile siyo ajira?
Ni ajira wanagoma kwa kudai haki yao. Polisi nao wagome Kama haajalipwa haki zao. Unajua Kuna sehemu nyeti tuseme muhimu ambazo wakigoma haichukui hata dakika kumi matatizo yao yanakuwa yametekelezwa. Polisi nao wamo, hivyo unatakiwa ujue kuwa polisi, JESHI siyo rahisi kugoma. Kwa hayo mawazo uliyoandika ukutukiwa kuandika Ni Kama vile ulikuwa ndotoni unaota ukakurupa na kukamata keyboard. Polisi, JESHI hawawezi kugoma. Mafao yao yanalipwa kimya kimya. Kugoma kwao Ni kwamba Magufuli ATAKUWA nje kesho yake.
 
Back
Top Bottom