Gosbertgoodluck
JF-Expert Member
- Mar 3, 2008
- 2,855
- 401
Wakati Kawambwa akiwa Waziri wa Ujenzi ulikuwa unaona kabisa anapwaya kwenye hiyo Wizara, sasa yuko Wizara ya Elimu i guess ndio kabisaa.kawambwa -mbunge wa bagamoyo 2005-2015
kikwete- mbunge wa bagamoyo 1995-2000
Jk mtu wa visasi jaman. Kamwambia magufuli,eti wizara na tanroads ni wazembe wa kutupwa. Jaman kweli?
Wandugu,
Ni swali la kizushi tu. Katika mawaziri waliopwaya wakiwa ujenzi ni Dr. Kawambwa. Ilikuwa kama wizara haina waziri. Ni kama alipokuwa wizara ya maji. Lakini nyakati zote hizo hatujawahi kusikia kikwete akiikemea wizara kwa kufanya mambo hovyo. Leo hii wameingia mawaziri wachapa kazi tunaona jamaa amechachamaa. Inakuwaje hapa? Au ndiyo kumalizana kwenyewe ionekane pombe imeshindwa kazi yake?
Atamfokeaje mshikaji wake. Kazi ambayo ameshaifanya na anaendelea kuifanya Maghufuli inaonyesha kuwa uwezo wa JK ni mdogo kwa hiyo anafanya hivyo ili kumwonyesha kuwa hajafanya kitu. More is needed. Kawambwa hawezi kazi, in fact alishindwa kumuondoa fisadi Mrema TANROAD wakati Kilons Mprogomyi aliuanika ufisadi wa Mrema bungeni. Ila nadhani Maghufuli naye hawezi kukimbia kwa sababu akijiuzulu tu JK atamgeuka katika suala la uuzaji wa nyumba. Serekali isiyokuwa na dira na uwezo wa kusimamia katiba na maslahi ya wananchi wake ndiyo ilivyo. Kwa hiyo tusitegemee kitu cha maana kwenye serekali ya JK. Na JK alivyo bingwa wa kulipiza visasi, nakuambia siku Maghufuli akijiuzulu ndiyo siku hiyo hiyo anashitakiwa. Lakini RA, EL, Vijisent nk kamwe hawatashitakiwa. Hii ndiyo TZ
Kiukweli kabisa mawaziri wanaopwaya Kikwete anawabeba, yupo Sofia Simba, yupo Magembe, yupo Mkulo. Lakini wale wanaochapa kazi wanaonekana kama ma.vi vile, hatujasikia hata siku moja akiongelea vitisho anavyopewa Tibaijuka, wala kumsifia Magufuli kwa kazi nzuri. Kila siku tunasikia vijembe tupu sijui tutaishia wapi
Bruker, suala sio ukabila. Lakini tuangalie kazi ambazo so far Maghufuli amezifanya na uzilinganishe na zile alizofanya Kawambwa. Pia, ujiulize kama kupeana maagizo na kuumbuana mbele ya wananchi ni jambo jema katika uongozi. JK ndiye aliyemteua Maghufuli kuwa waziri wa Miundo mbinu, wizara ambayo hapo nyuma wakati wa Mkapa, Maghufuli aliiongoza vema na wananchi tuliona barabara zikijengwa tena kwa kutumia hela ya watanzania na wala sio misaada. Je, kwani hakuna njia nyingine za kuwasiliana kati ya JK na Mawaziri wake mpaka kuwasiliana mbele ya watu. Kwanini Pinda alitoa matamko ya kumdhalilisha Maghufuli tena jimboni kwa Maghufuli? Wote Maghufuli, JK na Pinda wana mapungufu yao na mema yao. Lakini hili la kumdhalilishwa Maghufuli mbele ya wananchi ambao walikuwa wameshajenga imani kwake kwa sababu mara nyingi akishika wizara mambo yanaenda, sioni kama lilikuwa jema hata kidogo. By the way, JK ili kujoinyesha kuwa yeye ni bora, anasema ufanye kufuata sheria, najiuliza kuwa kwani hapo mwanzo alikuwa hafuati sheria? Na kama alikuwa hafuati kwanini hakukamatwa? Ile ilikuwa kupunguza umaarufu wa Maghufuli ili JK na Pinda waonekane wema wakati wema wao hatuuoni. Basi ngoja tuenjoy folleni za Dar es Salaam in the expense of kuwapaka mafuta Pinda na JK ili wang'are.
Na hao wote uliowataja na aliotaja Ntemi K wameteuliwa na kilaza mkuu mwenyewe!!! Kaazi kweli kweli.Duuh! yaani yupo Jumanne ( Magembe), Mustapha ( Mkullo)!!? Lakini hayupo Steven ( Wasira), William ( Ngeleja) wala Ezekiel ( Maige- ambaye kamati ya Mashirika ya umma iligundua mengi kuhusu kodi za mahoteli kwenye sehemu za hifadhi...Tshs. 19 billion zimepotea serikalini kutokana na Waziri kukataa mapendekezo ya wataalamu)... Lakini ah!! kina Omari na Yahaya ndio wanaopwaya zaidi.
Ila tutafika tu!!! Wacha niangalie nyota zangu hapa kibarazani.
Shkh Yahya,
Magomeni.