Pamoja na maandalizi ya hali ya juu na gharama kubwa zilizotumika, data za sensa 2022 hazitakuwa na ukweli kwa asilimia kubwa

Yawezekana isiwe hivyo, ila takwimu zitakazotoka zitakuwa na walakini kwa kiasi fulani
Kigogo Luhanga nyumba Moja Ina kaya 15 na karani anaambiwa lazima ahesabu nyuma 100. Weeee Kwa malipo ya 40000/= Kwa day wakati Kuna mtu kakaa kwenye kiyoyosi anakuna kende analipwa 300,000/= per day
 
Wote ni mashahidi kuwa Sensa ya mwaka huu ilikuwa na promo sana ukilinganisha na zilizopita, na dhumuni kubwa ni kuongeza hamasa kwa wananchi ili waweze kushiriki.

Ila kama ilivyokuwa kwa post code(anuani ya makazi), sensa inaharibikia mwishoni, na data zitakazokusanywa hazitakuwa na uhalisia, hii inatokana na sababu zifuatazo:

1. Walioomba hizi kazi, walipata msukumo kutoka kwenye hela za malipo bila kupima uzito wa kazi.

2. Makarani wanapika sana hizi data na hawafati misingi ya sensa inavyotaka.

Imagine karani alikuwa anahoji mwanamke ambaye anaishi na watoto wake wawili, ila usiku wa tarehe 22 kuamkia 23, hawa watoto hawakuwepo hapa Dar, wapo likizo kijijini kwa bibi yao.

Ila huyu Mama alimuomba karani watoto wake wahesabiwe hapa Dar, na karani alimkubalia, huko walipo it's obvious watahesabiwa tena .

3. Karani alikuja kwangu, akaniuliza umri, majina, tunaishi wangapi, tuliolala pale 22 kuamkia 23, namba ya nida na bima ya afya. Then after hapo akawa kimya muda mrefu, namuuliza vipi mbona kimya? Akanijibu kuwa taarifa zinazofata zinaeleweka ndio maana anajaza, so nisiwe na wasi. Ila nikahisi kama amemaliza kujaza dodoso, ikabidi nimuulize, mbona taarifa za ninaeishi nae hajachukua hata moja? Maana hakuniuliza umri wake, majina elimu n.k.

Yule karani akanijibu kuwa wanawake taarifa zao zinachukuliwa kwenye kaya za jamii. Nikamuuliza why iwe hivyo wakati anaishi hapa? Akanijibu kuwa taarifa zingine wanaume hatuwezi kuwa nazo, au unakuta ni za siri hivyo inabidi zitolewe na wanawake wenyewe kwenye dodoso za kaya za jamii, akatolea mfano mwanamke anaweza kuwa na mtoto wa nje alaf wewe hajakwambia .

Ilifikia hatua nikamwambia wewe nenda tu, maana sidhani hata kama unakijua unachoongea.


Sasa nikawa najiuliza, why wapike data? Kusave time, wamechoka au nini? Maana kazi ndio kwanza siku ya 3, au ni vile wanahasira/uchungu wa hela ambazo wanahisi wamepigwa?

Maana wanasema hela za chakula walizokatwa, zilikuwa haziendani na chakula wanachopewa. Lakini pia kuna certain amount in cash walitakiwa kupewa, nazo hawajui hatma yake.

Anyway, waendelee kujitahidi kwa hizi siku zilizobaki, ila wawe makini wasije kutoa data zikaonesha tupo wachache kulinganisha na 2012, au la, kukawa na unrealistic changes.

Regards,

Analyse
CCM hawashindwi wakiona wanapata idadi chini ya ile ya 2012, wapika ili iwe juu. Kumbuka tunakadiriwa kuwa tupo Mil 63, tutarajie kupewa majibu ya kuwa tumefikia Mil 66 kwenda juu.

Kwangu hawajaonekana hadi leo, na hadi sasa hakuna matumaini ya kuhesabiwa ingawa mimi binafsi sihesabiwi kabisa maana natoka alfajiri na kurudi usiku kila siku
 
Nakufahamu wewe ni mmoja wa waliobaniwa na mtendaji wa Kata nafasi ya ukarani.
Kwahiyo unakiri kabisa kumbe hizi nafasi walipeana kwa kujuana kama wananchi wengi wanavyolalamika?

Kubaniwa nafasi maana yake kunyimwa kitu ambacho una uwezo nacho na ni haki kukipata.
 
Sitakiwi kuulizwa mwenza wangu anaitwa nani, ana umri gani au anajishughurisha na nini? Nisipoulizwa Mimi, hizo taarifa wao wanazitoa wapi?

Pia ni sahihi kuhesabu watu ambao hawakulala kwenye hiyo kaya?
Ukiona hivyo karani ana connection na mama watoto,data zimeshajazwa,pole sana maswali yako yote ni ya msingi.
 
Jana kuna dada alifika kwangu kwa bahati mbaya sikuwepo. Alivyo mjinga kauliza jina langu kwa mtu ambaye naye alifika tu kunitembelea na hakunikuta. Alijaza jina mengine kakadiria.

Kabla hajaondoka nikawa nimefika nikamwambia karibu akadai anaondoka alishamaliza kazi kajaza taarifa zangu. Nikamuuliza umetoa wapi wakati sikuwepo na umejaza nini?

Alinitajia jina tu mengine kagoma na kukimbia aisee nilimsema sana huyo mtu aliyekuja kunitembelea japo ni ndugu yangu.

Yule mama sensa wala hakuweka tick mlangoni matokeo yake wenzake wanapita tena kwangu kuhesabu.
 
Wenye Akili tuliliona hili Siku nyingi sana. Kuna Census Clerk Mmoja wakati anachukua Taarifa za Mwanakaya Mmoja ( siyo MINOCYCLINE ) akaona Mwanamke mwenye Makalio makubwa ( Inye Ndembendembe ) anapita akaanza Kumkodolea na Kuamka kabisa Kitini Kumfuatilia na aliporejea akamwambia aliyekuwa anamhoji kuwa Mahojiano yameisha aingie tu ndani na Yeye atamjazia anavyojua ( akimaanisha kwa Kubumba ) ili mradi tu amuwahi yule Dada.
 
Wenye Akili tuliliona hili Siku nyingi sana. Kuna Census Clerk Mmoja wakati anachukua Taarifa za Mwanakaya Mmoja ( siyo MINOCYCLINE ) akaona Mwanamke mwenye Makalio makubwa ( Inye Ndembendembe ) anapita akaanza Kumkodolea na Kuamka kabisa Kitini Kumfuatilia na aliporejea akamwambia aliyekuwa anamhoji kuwa Mahojiano yameisha aingie tu ndani na Yeye atamjazia anavyojua ( akimaanisha kwa Kubumba ) ili mradi tu amuwahi yule Dada.
Zoezi la sensa limeyumbishwa sana na makarani
 
Back
Top Bottom