Pamoja Na Changamoto Nyingi, Dar Es Salaam Ndio Sehemu Ambayo Kila Mtu Anaweza Kufanikiwa

Pamoja Na Changamoto Nyingi, Dar Es Salaam Ndio Sehemu Ambayo Kila Mtu Anaweza Kufanikiwa

Makirita Amani

JF-Expert Member
Joined
Jun 6, 2012
Posts
1,914
Reaction score
3,437
Siku chache zilizopita rafiki yangu alinipigia simu akitaka nimshauri kama abaki dar au aende mkoani. Alikuwa njia panda kwa sababu amepata kazi dar na pia amepata kazi mkoani, kazi zote zina maslahi mazuri na ni yeye tu kuchagua. Nilimshauri abaki dar na nikampa sababu kwa nini namshauri hivyo. Nimeona huenda kuna wengine wanapata wakati mgumu kama huu na hivyo nimeona ni vyema nikatoa ushauri wa wazi kwa wote wanaofikiri ni wapi pa kuweza kufanikiwa kimaisha dar es salaam au mikoani.

Kwanza kabisa kufanikiwa kwenye maisha hakutegemei sana eneo mtu alipo ila inategemea na juhudi binafsi na malengo ya kufanikiwa. Ila tunapokuja kwenye mazingira yetu ya kitanzania kwa mtazamo wangu, DAR ES SALAAM NDIO SEHEMU PEKEE TANZANIA AMBAYO KILA MTU ANAWEZA KUFANIKIWA. Nasema kila mtu bila ya kujali kabila, dini, umri, jinsia wala kiwango cha elimu. Nitaeleza vizuri hili.

Mimi nimezaliwa moshi, nimekulia na kusomea moshi mpaka kidato cha nne. Nilikuja dar es salaam kwa mara ya kwanza miaka tisa iliyopita (mwaka 2005) na kwanzia kipindi hiko nimekuwa nikilinganisha maisha ya dar es salaam na maisha ya moshi na kuona tofauti kubwa sana.
Dar es salaam kuna fursa ya kila mtu kuweza kufanya biashara hata kwa kuanza na mtaji kidogo na akatengeneza faida kubwa.

Kwa mikoani, kwa mfano sehemu kama moshi ambapo nipafahamu vizuri ni vigumu sana kuweza kuingia kwenye biashara hasa ukiwa na mtaji kidogo, kuna watu wachache ambao wameshatawala masoko ya biashara na hivyo kuingia na mtaji kidogo ni kujipoteza.

Ni dar es salaam pekee ambapo mtu anaweza kuanzisha biashara kwa mtaji wa chini ya laki moja na akaweza kuikuza na kuwa biashara kubwa sana. Namfahamu mtu aliyeanza kufunga karanga kwa mtaji wa shilingi elfu ishirini ila sasa ameajiri vijana watatu kwenye kazi hiyo. Kuna watu wengi wanaishi dar hapa kwa biashara ndogo sana na maisha yao wanayaendesha vizuri. Watu wanauza maji na wanaishi, wanauza kahawa wanaishi, wanatembeza miwa wanaishi na hata wanaouza chenchi nao wanaishi. Ukienda sehemu kama moshi kuna watu wachache sana wanaofanya biashara za aina hii na tayari wameshatawala soko, hivyo inakuwa vigumu sana kwa mtu mpya kuingia kwenye soko la aina hii.

Ni dar ambapo mtu anaweza kuanzisha biashara bila ya kuwa na mtaji wowote na akatengeneza biashara nzuri kama anamipango mizuri. Biashara za kukusanya na kuuza makopo, vyuma chakavu, pesa mbovu, chenchi, kupiga debe zote hizi kwa mtu ambao anaweza kujipanga vizuri anaweza kufanya kwa muda mfupi na akajipatia mtaji na kuanza biashara nyingine kubwa.

Ni dar es salaam pekee ambapo mtu anaweza kuanzisha biashara ndogo ila akaingiza kipato kikubwa kushinda mshahara wa meneja wa makampuni makubwa. Namfahamu mtu ambaye alianza kuuza supu ya utumbo kwa shilingi elfu moja tu kwa sahani ila kwa miaka kama mitano sasa ameweza kununua nyumba, kutanua biashara yake na hata kuwekeza kwenye biashara nyingi zaidi, hana elimu kubwa ila ana juhudi kubwa. Namfahamu mtu ambaye alianza kuuza chipsi kwa kuchonga viazi mwenyewe, akajituma na hivi sasa ameajiri vijana sita na anabiashara nyingine nyingi zinazotokana na biashara hiyo.

Namfahamu mtu ambaye anazoa takataka mtaani kwetu ila anaishi kwenye nyumba yake na analea familia yake. Mtaji wake ni mkokoteni tu.
Namfahamu mwanaume ambaye huwa anavaa nguo za kike na kuzunguka mtaani kuchekesha na jioni anarudi nyumbani na hela ya kutosha kuendesha familia yake.

Watu wote ninaowataja hapa ni kwenye mtaa mdogo ninaokaa Tabata, hapa hatujenda kinondoni, mwenge, tegeta, mikocheni, temeke, mbagala, gongo la mboto na kwingine kwingi. Tofauti na mikoani dar es salaam hakuna anayemiliki eneo, kama wewe unafikiri unamiliki mtaa wenu mikocheni, sinza kuna watu kibao wanafanya yao, hapo hujaenda manzese, magomeni au ukonga.

Hapa natoa mifano michache sana ila kila ninapopita mitaani naona ni jinsi gani dar imejaa fursa ambazo hata mtu ambaye hajamaliza shule ya msingi anaweza kuzitumia na kuboresha maisha yake.

Kwa nini nasema yote haya?
Siandiki haya kuwashawishi walioko mikoani kukimbila dar es salaam, la hasha, popote ulipo unaweza kutengeneza mafanikio yako. Naandika haya kuwahamasisha wale walioko dar KUAMKA na kuchangamkia fursa hizi zilizopo wazi kwa kila mtu. Kuna watu wako dar hapa lakini wanalalamika maisha magumu, hakuna kazi, hakuna mitaji na kadhalika. Ila kama wakiweza kutumia fursa nyingi zinazopatikana dar wanaweza kutengeneza mafanikio makubwa.

Ni kitu gani unaweza kufanya mikoani?
Sina uzoefu na mikoa mingi ila kwa uzoefu nilionao kwa moshi, biashara ndogo ndogo ni vigumu sana kukua.
Ila kwa mikoa mingi ya kitanzania kilimo ni kizuri sana kufanyika mikoani na hiki unaweza kuanza na mtaji kidogo. Pia unaweza kuangalia mazingira uliyopo na fursa nyingine ambazo unaweza kuanza na mitaji kidogo. Kwa kujifunza vizuri mazingira yako na kufanya kazi kwa juhudi na maarifa unaweza kupata mafanikio makubwa.

Kama upo DAR na unalalamika maisha ni magumu wewe ni mzembe.
Samahani kama nimetumia neno kali na linalokuudhi lakini sina njia nyingine ya kuliremba hilo. Kwa fursa hizi ambazo zinapatikana kwenye kila kona ya jiji hili ni vigumu sana kushindwa kuzitumia.

Tatizo kubwa watu wengi wanachagua sana vitu vya kufanya wakati hawana anasa hiyo ya kuchagua. Waliopata elimu kidogo nao wanaona wana hadhi kubwa hivyo kudharau shughuli ndogo ndogo ambazo zinawaingizia watu wengi kipato kikubwa.

Kuna changamoto nyingi sana dar es salaam, foleni, miundombinu mibovu, hali ya hewa ya joto, wingi wa watu na mengine mengi. Ila ukiweza kutengeneza njia nzuri ya kukabiliana na changamoto hizi unaweza kupata faida kubwa sana ndani ya jiji hili.(Kwa mfano kukabiliana na changamoto ya foleni unaweza kufanya hivi, bonyeza hapa kusoma zaidi.)

Kwa nini wengi hawafanikiwi?
Pamoja na watu wengi niliowataja hapa bado kuna wengi sana ambao wanafanya biashara ndogo ndogo huku mitaani ila bado hawafanyi vizuri. Tatizo kubwa linatokana na kutokuwa na mipango mizuri na kukosa ubunifu. Wengi wanafanya biashara kwa kuiga, mtu anaona mwenzake anauza kahawa na yeye anaenda kuanza kuuza kahawa bila hata ya kuangalia ni jinsi gani anaweza kuitofautisha na kutengeneza soko kubwa zaidi.

Kama upo dar es salaam na unateseka kutengeneza kipato karibu tushauriane njia bora za wewe kuweza kujenga uchumi wako na kufikia mafanikio makubwa. Kwa ushauri zaidi unaweza kuwasiliana na mimi kwa email amakirita@gmail.com au simu 0717396253/0755953887.

Nakutakia kila la kheri kwenye safari yako ya kuboresha maisha yako.

Kumbuka TUKO PAMOJA kwenye safari hii.
 
Good Article Indeed Ila Kumbuka Kuna Survival Of The Fittest Popote Utakapokuwa Haijalishi Upo Dar Es Salaam Au Mkoani!!
 
Naunga mkono andiko hili 100%

Ila pia kuliweza sana hili jiji kiuchumi uwe mzoefu au mwenyeji kiasi chake
La sivyo ukija na ugeni lazma u hustle kwanza kuujua mji vema otherwise uwe mtu unae cop na mazingira fasta.

Usije mjini
 
Good Article Indeed Ila Kumbuka Kuna Survival Of The Fittest Popote Utakapokuwa Haijalishi Upo Dar Es Salaam Au Mkoani!!

Ni kweli kabisa mkuu, survival of the fittest ipo kila mahali na ndio maana hapa nataka kuwasaidia watu wawe fiti ili waweze kusurvive, sio wote watakaoweza ila wale wenye nia ya dhati wataweza.
 
Ni ushauri mzuri ndugu, ila washauri nini wafanye wakiwa mikoani, wilayani na vijijini kwa kutumia changamoto zilizopo ili jiji lisifurike watu na carrying capacity ikawa shida kwao na watu wengine!

Vinginevyo umefanya vizuri kuandika na kuweka mawasiliano yako.
 
Siji dar ng'o....nipo uswailini na mambo yangu yanaenda vizuri.
 
Ni jambo jema Sana uliloliwaza, ingawaje maisha hayana formula. Ilikuwa Ni vyema ukawaambia na watu sehemu uliko nje ya Dar unaweza kufanya mabadikiko ya maisha yako. Hii Ni kwa sababu kwa article yako hii amini Kuna mtu anatafuta nauli aingie Dar.
Wote tukihamia Dar, nani atalima kule vijijini?. All in all Good article
 
mbona ume qoti li habari lote hilo!
 
Naunga Mkono Mada Na Mawazo Ni Mazuri, Asante Mkuu.
 
Makirita Amani-Andiko lako lingekua na maana zaidi kama ungekua umeshafanya maisha walau mikoa 7 kati ya mikoa 30 ya Tanzania.
Umetoka Kilimanjaro Ukaenda Dar kwahiyo ukiacha sehemu hizo mbili hujui chochote kuhusu maeneo mengine.

Kwa ufupi wewe tunakuita umestuka jiji,yaani umetoka migombani kule Moshi ghafla umeona mataa ya jiji unadhani nini kitatokea.

Maisha ya watu wa Dar ni mateso tupu.
Kwanza ungeuliza waliopo Morogoro,Mbeya,Mwanza,Arusha n.k wanaendeshaji maisha na shughuli zao then ufanye comparison na Dar ndipo utoe andiko lako.

Wakati kijana wa Dar anaona kufanikiwa kimaisha ni kumudu kumiliki godoro,kitanda na kupangisha chumba, kijana wa Msange kule Singida anaona kufanikiwa ni kumiliki hekta 7 za shamba la vitunguu avune akauze Kenya.
Usikariri kaka maisha hayana formular.
 
Dar es salaam sio sehemu ya kwenda kuanza maisha kwan asilima kubwa ya vijana wanaoishi dar maisha yao ni magumu wachache hasa waliokwendaa shule na wenye mitaji mikubwa ndo wanaofurahia jiji. wengi huko wanaishi kwa ndoto na kuwasindikiza wenye nazo, kuna gape kubwa sana kati ya tajir na maskini wa dar na hicho ndo kipimo halisi cha maisha,wakat watu wachache wana mahela mpaka wanakosa pa kuyaweka walio wengi sana hawana hata uhakika wa kupata hata mlo mmoja kwa siku kila kitu shida maji usafir hali ya hewa nk!
 
Makirita Amani-Andiko lako lingekua na maana zaidi kama ungekua umeshafanya maisha walau mikoa 7 kati ya mikoa 30 ya Tanzania.
Umetoka Kilimanjaro Ukaenda Dar kwahiyo ukiacha sehemu hizo mbili hujui chochote kuhusu maeneo mengine.

Kwa ufupi wewe tunakuita umestuka jiji,yaani umetoka migombani kule Moshi ghafla umeona mataa ya jiji unadhani nini kitatokea.

Maisha ya watu wa Dar ni mateso tupu.
Kwanza ungeuliza waliopo Morogoro,Mbeya,Mwanza,Arusha n.k wanaendeshaji maisha na shughuli zao then ufanye comparison na Dar ndipo utoe andiko lako.

Wakati kijana wa Dar anaona kufanikiwa kimaisha ni kumudu kumiliki godoro,kitanda na kupangisha chumba, kijana wa Msange kule Singida anaona kufanikiwa ni kumiliki hekta 7 za shamba la vitunguu avune akauze Kenya.
Usikariri kaka maisha hayana formular.

umenena vyema Mkuu. mkoani fursa bado ziko wazi na ukizitumia vizuri unapasua fasta. hatuwezi kujazana Dar ili tufanikiwe. hatuishi kwa mazoea Bali tunaishi kwa kujifunza.
 
Makirita Amani-Andiko lako lingekua na maana zaidi kama ungekua umeshafanya maisha walau mikoa 7 kati ya mikoa 30 ya Tanzania.
Umetoka Kilimanjaro Ukaenda Dar kwahiyo ukiacha sehemu hizo mbili hujui chochote kuhusu maeneo mengine.

Kwa ufupi wewe tunakuita umestuka jiji,yaani umetoka migombani kule Moshi ghafla umeona mataa ya jiji unadhani nini kitatokea.

Maisha ya watu wa Dar ni mateso tupu.
Kwanza ungeuliza waliopo Morogoro,Mbeya,Mwanza,Arusha n.k wanaendeshaji maisha na shughuli zao then ufanye comparison na Dar ndipo utoe andiko lako.

Wakati kijana wa Dar anaona kufanikiwa kimaisha ni kumudu kumiliki godoro,kitanda na kupangisha chumba, kijana wa Msange kule Singida anaona kufanikiwa ni kumiliki hekta 7 za shamba la vitunguu avune akauze Kenya.
Usikariri kaka maisha hayana formular.

Big up mkuu! hiyo inaitwa tembea uone!
 
Waulize wale walio Dar ambao hawana uhakika hata wa mlo mmoja ndo utajua kama kila mtu anaweza kufanikiwa!
 
Makirita Amani-Andiko lako lingekua na maana zaidi kama ungekua umeshafanya maisha walau mikoa 7 kati ya mikoa 30 ya Tanzania.
Umetoka Kilimanjaro Ukaenda Dar kwahiyo ukiacha sehemu hizo mbili hujui chochote kuhusu maeneo mengine.

Kwa ufupi wewe tunakuita umestuka jiji,yaani umetoka migombani kule Moshi ghafla umeona mataa ya jiji unadhani nini kitatokea.

Maisha ya watu wa Dar ni mateso tupu.
Kwanza ungeuliza waliopo Morogoro,Mbeya,Mwanza,Arusha n.k wanaendeshaji maisha na shughuli zao then ufanye comparison na Dar ndipo utoe andiko lako.

Wakati kijana wa Dar anaona kufanikiwa kimaisha ni kumudu kumiliki godoro,kitanda na kupangisha chumba, kijana wa Msange kule Singida anaona kufanikiwa ni kumiliki hekta 7 za shamba la vitunguu avune akauze Kenya.
Usikariri kaka maisha hayana formular.

Umeongea vyema aisee,mikoani nako fursa zipo,nikiwa na million zangu kama 3 nakodi mashamba hekari 25,napanda maharage tu kwa vile ni ya mda mfupi,hapo nishapiga mahesabu ya kuwalipa wanaopalilia na kuandaa shamba,ukija kuvuna unapiga hela isiyopungua million 15 ndani ya miezi 3 au 4.Je kwa mtaji wa 3m niambie dar utapata million 15 ndani ya miezi 4,na ni biashara gani??upige bei ya kupanga chumba maana ni ghali mno,msosi wa kila siku na kama unaenda kazini kwa kulipia daladala inakwaje,kama ni kibanda ujue lazima ulipie jengo na bado unalipia gheto la kuishi.
 
Safi mkuu mimi nilifukuzwa chuo kikuu nikaenda home mzee akanifukuza nikaja dar kidongo chekundu nikajichanganya na madalali kwa juhudi kubwa nikatoka fresh sasa ninamiliki show room yangu mzee tunaelewana na nimechukua digrii yangu...siri....juhudi sala na uaminifu popote utafanikiwa biashara zangu haziko dar tena
 
Ni jambo jema Sana uliloliwaza, ingawaje maisha hayana formula. Ilikuwa Ni vyema ukawaambia na watu sehemu uliko nje ya Dar unaweza kufanya mabadikiko ya maisha yako. Hii Ni kwa sababu kwa article yako hii amini Kuna mtu anatafuta nauli aingie Dar.
Wote tukihamia Dar, nani atalima kule vijijini?. All in all Good article

Kama kilimo dili ,na kama ni muhimu kuwe kuna watu wanaolima mikoani, kwa nini huyo mtu asiwe ni wewe? ? we unataka uendelee kuwepo dar. halafu jamaa waendelee kulima mikoani?

Ni hivi inabd jamaa waje mjin,mashamba yakose wakulima, kisha mikoani kutakuwa na chakula kidogo cha kutosha wao tu Dar itakosa chakula, na kisababisha bei kupanda, watu watataka kucapitalize kwenye ongezeko la Bei za vyakula kwa kurudi mikoani kulima ili wauze Dar ambako vyakula ni bei sana na vina faida.

Na kwa kuwa. watakuwa wamekusanya mitaji yakutosha wakiwa Dar, na ujanja mwingi wa hapa mjini, watafanya kilimo kisasa sana na kwa technolojia
 
Acha masikhara bwana!
Ktk mikoa vijana wanapigika na maisha Dar unaongoza.
Miaka 9 ndo ufanikiwe kukodi chumba Tandale au Mbagala
 
Back
Top Bottom