Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 269,640
- 697,994
Kwanza habari za kifo cha Prof J ni za uongo hivyo zipuuzeni..Imebidi nifanye masahihisho ya haraka kwenye hiki kifungu cha kwanza
Pili nipende mno kumpongeza Mama Samia Suluhu kwa kujitua furushi zito lililomlemea sana tangu alipotwishwa na hao wenye agenda zao. Hatimaye ukweli amekuja kuuona na kwa dhati ya moyo na uthubutu wa hali ya juu kabisa kaamua kufanya ambacho wengi wasingethubutu kukifanya.. Mama yu kwenye mchakato wa maridhiano na chama kikuu pendwa na maarufu Afrika na duniani CHADEMA
Tatu nimpongeze wakili msomi na mwanasiasa machachari Tundu Lissu kwa kazi kubwa aliyofanya akiwa nje uhamishoni kwa muda wote aliokuwa huko .. Kitu kilichopelekea kusababisha na kuchagiza haya yanayotarajiwa kutokea.. Maridhiano na kufungua ukurasa mpya..
Nne nimpongeze kwa dhati ya moyo mwenyekiti shupavu wa CHADEMA kwa kusimama imara hata katika kipindi cha kuumizwa na kutikiswa kisiasa, kiuchumi na kijamii Lakini bado akabaki imara kama chuma cha pua..! Kukichwa hatimaye hupambazuka.. !
Tano niwapongeze wanachama, wapenzi, mashabiki nk wote wa chama kikuu cha upinzani Tanzania kwa kushikamana, kutiana moyo kusaidiana katika kipindi chote cha mapito yote waliyopitia.. Hakika wamekuwa jasiri na shupavu kwa kiwango cha juu kabisa..pongezi hizi ziwaendee na viongozi wote pia
Sita niwapongeze CCM ...!
Mama aliposhika hatamu ilikuwa ni kipindi cha usemi maarufu wa KUUPIGA MWINGI..! Tulimsifu na kumsifia kila upande na kila kona.. Lakini mara ghafla bin vuu akazongwa na kutwishwa furushi zito lililomuelemea kwa kipindi chote hicho.. Muda hauongopi na muda ni hakimu mzuri.. Uongo hupanda lift na kufika haraka bali ukweli hukwea ngazi na kufika baadae!
Tunatambua yote haya mapya yanayotrend sana hayakutokea ghafla bin vuu.. Ni mengi yamefanyika nyuma ya macho ya hadhira.. Tunda lake la kwanza kuonekana likitarajiwa kuwa tar 18.02.2022...Likitokea kama linavyotarajiwa kutokea basi ni mwanzo mwema sana
Natambua kuna kesi zinaweza kufutwa.. Watuhumiwa wakaachiwa huru lakini hapo hapo wakakamatwa tena! Hili tuliweke kiporo
Natambua pia kuna covid 19.. Namna vile homa inavyopanda na kushuka!
Natambua pia hii ni wiki ya RED CLOLOR... Rangi angavu inayoashiria bahati,nguvu na mamlaka kwa baadhi ya tamaduni.. Rangi ya upendo na wapendao. Rangi ya Timu kubwa Afrika SIMBA SPORTS CLUB.. IMEPIGA MTU 3:0, KISHA IKAPIGA MWINGINE 7:0.. Tafuta kiroho tafsiri ya namba 3 na 7 na nguvu zake.. Utajua CHADEMA ni nani.. Na SIMBA ninini..!!!!
Ni hayo tuu..!