Darren2019
JF-Expert Member
- Nov 23, 2019
- 1,112
- 2,379
Uaminifu uko katika mambo mbalimbali ila mimi ntajikita hasa kwenye mambo ya fedha.
Nimekuwa muhanga wa kuumizwa na jamaa zangu mara kwa mara hadi najiona boya sasa, si kwamba nina pesa no ila katika hizihizi senti mbili tatu.
Unamwamini mtu unamwazimisha fedha tena unamwambia si zako, anakuhakikshia hatokuangusha nawe unampa kwa bashasha eti umemsaidia jamaa ako, mwisho wa siku matokeo yake unakuja kulipa mwenyewe na urafiki unakufa.
Visa vipo vingi ila vingne ni hivi vya kurejesha deni nusunusu kinyume na makubaliano, tunavurugiana mipango bhana.
Mtu nimempa elfu 50 January kwa makubaliano arudishe mwisho wa mwezi, ulipofika mwisho wa mwezi akanifuata anaomba nimvumilie atarejesha mwisho wa February, nikakaza roho nkakubali, leo anakuja na elfu 20 eti nimvumilie hadi wiki ijayo kuna hela anasubiri kwa jamaa ake. Nimepokea ila nimefanya somo.
Ukitaka kupoteza marafiki jitie kiherehere wa kukopesha ovyo. Natambua kila mtu ana chance ya kupata shida ila tujitahidi kuthamini wanaotusaidia si kwamba wanazo sana.