Pamba, Korosho Mmeshindwa kununua sasa mnanyang'anya Watu Choroko zao

RockCarnegie

JF-Expert Member
Jan 17, 2019
963
1,927
Habari wana JF

Nimeona taarifa zikimuonesha Mkuu wa Wilaya ya Magu akiwanyang'anya wafanyabiashara shehena za choroko walizonunua kutoka kwa wakulima kwa madai ya kutotumia vyama vya ushirika kununua zao hilo.

Swali la kujiuliza, kwa nini serikali ya Rais Magufuli haitaki kujifunza kuwa Ushirika umeshindwa kufanya biashara na badala yake limekuwa genge la kudhulumu wananchi mali zao. Mfano ni mazao ya korosho na pamba ambayo mpaka sasa wakulima hawajalipwa malipo yao ya msimu uliopita.

Serikali ya CCM itambue kuwa kutaifisha/kunyang'anya mali za watu ni rahisi mno kuliko kufanya biashara yenyewe.

Toka kuwa Serikali ya wanyonge hadi kuwa genge la wanyang'anyi, CCM ni chama mufilisi hakiwezi kamwe kutupa uongozi wa kuendeleza taifa na watu wake.
 
Naona wameichokoza na choroko sasa , hii itawapigw zaidi ya korosho..kikubwa serikali iache mazao yaamue soko lao wenyewe, vyama vya ushirika ndio vimeiua pamba , mkonge


It is never to late to begin. Start now
 
Yule mfanyabiashara ni kama anaonewa, kwanin asipewe mlolongo wa kufuata ili arejeshewe mali yake. Nimejikuta namuonea huruma kwa jinsi alivyojitetea, sasa endapo kakopa Benki ndio baaasi mnada wa nyumba yake unamhusu. Hurumaaa
Huyo jamaa aliyenyaganywa nakaa naye nyumba ya tatu kutoka kwangu ....na aliweka bond mkopo nyumba yake wife kaanguka na preasure yupo hospital na alikuwa kapata soko la kupeleka indian

........hiii ni biahsara huria na ninasikia mwaka huu wanampango hata mpunga vyama vya ushirika vinunue kwa kanda ya ziwa ...kwa mkopo huku si kurudishana nyuma

sent from HUAWEI
 
Back
Top Bottom