Palipotoboka panazidi kuvuja!

Palipotoboka panazidi kuvuja!

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
360,102
Reaction score
828,977
Sidhani kama washauri wao wa kiroho wanawaambia ukweli mambo yanazidi kuharibika na kila uchwao ni afadhali ya jana na ya kwamba hii haina comeback!

All we can say in very very painful feelings it will never be the same again!

Hizi dalili mbili zingetosha/zinatoshq kabisa kuwagutua toka usingizi mzito kwamba hamkani si shwari tena! No longer at ease!
1.
Jaribio la utekaji lililoshindikana nchi jirani na watekaji kujulikana! Hili jambo limezivua nguo
mamlaka na si jepesi kama inavyochukuliwa!

2. Kukamatwa kwa meli yenye bendera na usajili wa Tanzania iliyokuwa imebeba shehena ya maana ya madawa ya kulevya

Kwenye tukio la utekaji wameshindwa kabisa kujitokeza na kusema neno! Lakini kwenye tukio la meli msemaji kajaribu kulitolea ufafanuzi ambao hata hivyo umezidisha maswali na mijadala mitandaoni

Matukio yote mawili yametokea kimataifa na yote ni matukio hasi.. Wengine wameenda mbali na kusema utekaji na biashara ya mihadharati ni lila na fila.
Ziada ya hayo kuna ile kesi ya TAL.. Nayo ni aibu tupu mpaka imefikia UN imetoa tamko zito kwamba TAL mwenyekiti wa CHADEMA aachiwe huru bila masharti na alipwe fidia! Je unadhani bado mambo ni shwari?

La mwisho! Makaburi yaliyozika miili takribani 20 iliyoharibika iliyofungwa kwenye viroba vyeusi

Ardhi imelemewa na sasa inatapika.. Ulimwengu wa roho unajaribu kutuonesha ishara na kujaribu kuwapa tahadhari kwamba sasa enough is enough! wasiendelee tena!
IMG-20260225-WA0016.jpg
 
Back
Top Bottom