Pale Mfalme anapogeuka Watu wake!

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,330
51,836
PALE MFALME ANAPOGEUKA WATU WAKE!

Anaandika, Robert Heriel

Pale Mfalme anapogeuka watu wake, Raia wa nchi yake hugeuka Watumwa wa Wageni. Wananchi hutumikishwa na Wageni, hufanywa vijakazi na vikaragosi,

Pale Mfalme anapogeuka Nchi yake, Raia hugeuzwa vibarua pasipo barua ya Mkataba, ilhali wageni wanapewa mikataba minono ya kujaza kibaba. Huku wananchi wakifa Kwa ufukara.

Pale Mfalme anapogeuka nchi yake, Raia wake hutembea Kwa miguu Kama Wadudu ilhali Wageni hupanda Farasi wenye Kasi, na magari ya kifahari kwa kuwanyonya wenye nchi Yao.

Pale Mfalme anapoigeuka nchi yake, Wageni huwa na umoja kuliko wenyeji, Mfalme atahakikisha wenyeji hawaungani Kwa ajili ya nchi Yao.

Pale Mfalme Anapogeuka nchi yake, huwasamehe Kodi Wageni na kuwakamia Wenye nchi ikiwezekana kuwafunga kabisa Jela.

Pale Mfalme anapoigeuka nchi yake, Wageni ndio huwa matajiri kuliko Wenyeji wa nchi Husika. Moja ya Dalili ya kuwa wafalme wamegeuka nchi zao ni kuangalia matajiri wa nchi husika, ukiona wageni ni matajiri kuliko wenyeji basi elewa nilichokisema.

Pale Mfalme anapoigeuka Nchi yake, Nyenzo, Mashirika na Miradi mikubwa ya uzalishaji katika nchi itashikiliwa na Wageni,

Pale Mfalme anapogeuka nchi yake, Wageni watakuja wakiwa Masikini kisha wataondoka wakiwa matajiri ndani ya nchi. Huku wenyeji WA nchi wakipuuzwa .

Pale Mfalme anapogeuka nchi yake, atashindwa kuunda Propaganda ya kutukuza watu wake na kuwatengenezea falsafa kuwa wao ni bora kuliko wageni, Mfalme atakuwa anawasifia wageni kuliko wenyeji.
Moja ya Jambo la awali la Mfalme au Mtawala basi ni FALSAFA YAKE.

Mtawala yeyote ambaye hana falsafa ya kuona Watu wake ni bora kuliko wageni huyo mi MSALITI.
Na ikiwa ni hivyo, Taikon angeshauri aondolewe mara moja.

Pale Mfalme anapogeuka watu wake, atawapuuza Wanyonge na Masikini na kuwapendelea Matajiri na watu wenye hadhi.

Hali inasema; Usimpendelee Tajiri Kwa Utajiri wake wala usimpendelee masikini Kwa umasikini wake, bali wote wape haki sawa na usiwe na mawe mawili ya kupimia.

Pale Mfalme anapogeuka watu wake, atawapendelea masikini na wanyonge na kuwapuuza matajiri.

Pale Mfalme anapogeuka Watu wake, atakosa maarifa ya kuwakomboa wananchi masikini kutoka katika hali ngumu ya maisha, Ila atakuwa bingwa WA kutafuta sababu za kuhalalisha ugumu huo wa maisha.

Pale Mfalme anapogeuka watu wake, atazalisha Wafanyakazi na watumishi wahuni na washenzi washenzi wasiowaadilifu, ambao hawatatimiza wajibu wao kuwahudumia wananchi wa nchi Yao isipokuwa watakuwa wanatoa upendeleo Kwa Raia wa kigeni.

Ukiona mtumishi au mfanyakazi katika ufalme iwe wajuu au WA chini hatimizi wajibu wake kukuhudumia wewe Kama Raia, jua Huyo ni MSALITI WA NCHI, mwambie wewe ni Msaliti wa nchi. Watu Kama HAO Taikon anawapigaga vibao.

Mfalme Msaliti huzalisha Watumishi Wasaliti. Kisha hufanya wananchi wawe wasaliti wa nchi Yao wenyewe.

Taifa kamwe halitoweza kuendelea ikiwa litaongozwa na Wafalme ambao ni wasaliti, waliogeuka nchi Yao na kugeuka watu wao.

Ulikuwa nami Taikon Master, kutoka Nyota ya Tibeli.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Iringa
 
Back
Top Bottom