Pale maiti inapokuwa ni Bora kuliko Mgonjwa (Ujumbe wangu wa leo)

Matanga

JF-Expert Member
Nov 13, 2019
2,281
3,973
Mazungumzo baina ya Bwana Sixto na Sembela ambao ni marafiki wakubwa sana.

Sixto: Naumwa sana rafiki yangu Sembela nimelazwa wiki ya pili sasa sina pesa kabisa.

Sembela: Unaumwa nini Kaka?

Sixto: Homa imenibana kweli aisee na naona pesa za kugharimia matibabu zinaniishia kabisa.

Sembela: Ningekusaidia bro bahati mbaya kuna kiwanja tulipatana na muuzaji majuzi ndo nataka kesho nikanunue.

Sixto: Sawa Kaka, ila siko vizuri kabisa. Nisaidie walau kidogo ndugu yangu.

Sembela: Iko hivi bajeti zote tunazopanga Mimi na mke wangu, huwa hazivunjwi ndugu yangu. Nimebakiwa na hiyo milioni tano ya kiwanja.

Sixto: Ukinisaidia hata laki mbili tu inatosha. Nikipona nitakulipa, nitazirudisha.

Sembela: Hapo ngumu kidogo na vipi umejaribu kuupigia Uongozi wa Chama chetu cha wafanyabiashara?

Sixto: Ndio, wamenichangia 30000.
Sembela: Anzia hata hiyo bro. Get well soon.

BAADA YA SIXTO KUFARIKI

Sembela:
Sixto alikuwa rafiki yangu tuliyeshirikiana katika mambo mengi sana hivyo Mimi kama rafiki aliyekuwa zaidi ya ndugu natoa mchango Milioni moja.

Chama cha Wafanyabiashara: Tumehuzunishwa sana na taarifa hii, kwani alikuwa mtu muhimu sana katika chama chetu.

Sisi tutagharamia gharama zote za hapa kuanzia chakula, usafiri hadi mazishi.

UJUMBE WANGU KWENU

Naomba ifikie kipindi tu tubadilike kwa kuanza kuthamini mgonjwa kuliko Maiti, yaani Mtu akishafariki.

Maana kuthamini Maiti kuliko Mgonjwa ni unafiki uliopitiliza.

Huenda huyo Mtu angesaidiwa kwa nguvu kubwa kama inayoonekana kwenye mazishi asingekufa.

Kibaya zaidi ni pale ambapo Mtu hakuwahi kwenda hospitali kumjulia hali Mgonjwa makusudi kabisa, lakini anajifanya yeye ndo Mwenyekiti wa Kamati ya Mazishi.

MUNGU atuhurumie. Tujitafakari saana na Tubadilike jamani!
 
Ukweli mchungu.....ila bina adamu wengi hasa wakizazi hiki chaleo(dotcom)kimekua chawatu wabinafsi nawanafiq mnooo.....
 
Kuna grp moja la WhatsApp jamaa alitoa taarifa kuwa anauguliwa na mtt wake wa kumzaa kabisa, members wa grp wakamjibu kuwa katiba yao haipo kwaajili ya kuchangia mgonjwa, kwakua kila mtu atasema anauguliwa kila siku, hivyo katiba imesema kama akifiwa na mtt ndo watachanga
 
Ukweli mchungu.....ila bina adamu wengi hasa wakizazi hiki chaleo(dotcom)kimekua chawatu wabinafsi nawanafiq mnooo.....
Ubinafsi unalipa. Nimesaidia Sana watu tangu 2004 lakini siku unapata tatizo unaenda kuomba msaada kwao. Anakupotezea. Kila mtu ahangaike na shida zake
 
Sitakaa nisahau nilikuwa na shida ya ths 150000 nikampigia rafiki yangu wa karibu sana , nikamweleza shida yangu akanambia angenisaidia ila hela aliyonayo anatengeneza gari zake mbili na shopping ya chakula cha nyumbani , Pia ana Safari ya kwenda Sri Lanka December hawezi toa hela na hatakama angenipa , hawezi kwenda bank kwa ajili ya kutoa USD 70!
 
Sitakaa nisahau nilikuwa na shida ya ths 150000 nikampigia rafiki yangu wa karibu sana , nikamweleza shida yangu akanambia angenisaidia ila hela aliyonayo anatengeneza gari zake mbili na shopping ya chakula cha nyumbani , Pia ana Safari ya kwenda Sri Lanka December hawezi toa hela na hatakama angenipa , hawezi kwenda bank kwa ajili ya kutoa USD 70!
Aiseee
 
Hahaha ujamaa uliishashindwa mgeanza kujaribu ubepari sasa.

Kila mtu awe na bima ya afya yake na familia yake.

Wazazi wawe na life insurance au bima ya maisha.

Kila mtu ajifunze kujitegemea.

Ulizaliwa peke yako utakufa peke yako.

Siasa za kutishiana Mungu kwenye maisha zinaendeleza ujamaa pori, unaouita inafiki.

Anza sasa kuelewa kila mtu atabeba msalaba wake mwenyewe.
 
Ukweli mchungu.....ila bina adamu wengi hasa wakizazi hiki chaleo(dotcom)kimekua chawatu wabinafsi nawanafiq mnooo.....
Shakazulu,usimsahau nyerere,mbele mwekeke Mandela,kwame,chukua maumoja moja yote lada oau,east Africa community acha hii ya Sasa ambayo wengine wanafunga mipaka Corona wengine hawafungi ile ya 70-80 labda ilikuwa na waafrica wa kweli u
 
Back
Top Bottom