Pale kiswahili kinapotamalaki!

Behaviourist, wamelitumia vizuri tu, neno hilo 'kubanduliwa', wakimaanisha 'unseated' kwa kimombo. Tena ndio maana yake kamili na ni kiswahili sanifu, litafute kwenye kamusi yako ya kiswahili. Sema watanzania huwa wanalitumia kiuzinzi zaidi.
Umenikumbusha siku Bujibuji aliposhangaa kusikia kwamba marehemu nchini Kenya huwa anaitwa mwendazake.
 
Umenoa jombaa, nchini Kenya ukizungumza kuhusu kubanduliwa watu watajua unamaanisha maana kamili ya neno kubanduliwa. Wala hamna matumizi mengine ya neno hilo zaidi ya hapo. Sasa hapo utasemaje kwamba wamechemsha?
 
Wazee wa "MBI" MBI" "I" wanavyokinajisi kiswahili mbaya zaidi wanawadanganya mpaka wazungu utakutana na mtalii anajionea fahari kuwa anajua kiswahili kumbe kafundishwa na hayo matapeli
 
Nakuhakikishia kwamba hapo Citizen Tv hakuna anayefahamu kwamba 'kubanduliwa' lina maana nyingine, tofauti na walichonuia kwenye caption yao hiyo. Jombaa ni jambo la kawaida sana kwa lugha yeyote ile kuwa na maneno au matumizi ya maneno yanayotofautiana kwenye maeneo tofauti. Kwa mfano Kiswahili cha visiwani Lamu, Manda na Kiwayuu kinatofautiana na cha Mombasa, Malindi na Kilifi au hata Taveta. Hivyo hivyo kwa kiswahili cha Zenji, Pemba na kile cha Dar, Tanga na Tz bara kwa ujumla.
 
Nadhani umeelewa hoja yangu vizuri tu, sina maelezo mengine ya ziada kuhusu suala hilo. Ila unafaa ufahamu kwamba kwenye kiswahili, sawa na lugha yeyote nyingine, kuna maneno ambayo yana maana zaidi ya moja. Tena nadhani 'kubanduliwa' kama mnavolitumia nyie ni kama 'slang' na maana yake hiyo sio rasmi. Huwezi ukawalaumu Citizen Tv kwa kulitumia neno hilo, kisa eti lina maana nyingine kwa lugha ya mitaa. Kuna mifano mingine mingi tu kwenye kiswahili sanifu. K.m Kupiga pambaja- Kukumbatia, Mwendazake- Marehemu, Nyanya- Bibi n.k, n.k.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…