Palamagamba Kabudi tengeneza Sheria ya Tanzania tuachane na Ukoloni!

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,817
Waziri wetu wa Sheria Palamagamba Kabudi (PhD) wewe ndiye naweza kukuita nguli wa Sheria Tanzania, nilikuwa na pendekezo wewe pmj na manguli wenzako tengenezeni Sheria ya Tanzania ili tuachane na British Common Law ambayo ni Utamaduni wa Muingereza!

Tunaishi mara moja tu Dunia hii hivyo fanyeni kweli, ili mkiondoka muache nyuma vizazi vitakavyojivunia jamii yao, linawezekana kabisa mkiamua!

Nilishangaa kwenye Kampeni za Uchaguzi wa tls Arusha watu walikuwa wanashindana kuongea Kiingereza tu, badala ya hoja, ujinga huu lzm tuuache kama tuna nia ya kwenda mbele na kuwa na nafasi kama Binadamu wa kuheshimika Dunia hii!

Nchi ndogo kama Korea ina watu milioni 24 tu na ukubwa wa km za mraba laki moja na ushee, TZ yetu ni kubwa zaidi ya mara 7, lkn wanaisimamisha Dunia!
Sasa wameweza je? Ni kwa sababu wanajiamini, hivyo hata sisi tukiamua tunaweza!
 
Waziri wetu wa Sheria Palamagamba Kabudi (PhD) wewe ndiye naweza kukuita nguli wa Sheria Tanzania, nilikuwa na pendekezo wewe pmj na manguli wenzako tengenezeni Sheria ya Tanzania ili tuachane na British Common Law ambayo ni Utamaduni wa Muingereza!

Tunaishi mara moja tu Dunia hii hivyo fanyeni kweli, ili mkiondoka muache nyuma vizazi vitakavyojivunia jamii yao, linawezekana kabisa mkiamua!
Ila kumbuka kateuliwa kwa kujua kusoma na kuandika tu. Hivyo usimbebeshe mzigo was was kiprofesa! Napendekeza wanasiasa wote maprof na ma dkt , prof na dkt ziondolewe kwenye politica ID zao! Not needed
 
Back
Top Bottom