Mkuu, it doesn’t pay to be mean, radher than to be practical and diplomatic.
Be smart and simple.
Hao jamaa tuishi nao kwa akili, si kujitamba kuwa mean and menacing, wakati hatuna lolote .
Kama kuna kitu cha kujifunza, ni kama issue ya Saddam Hussein.
Alizidiwa na utajiri wa mafuta na kaanza kutembeza umwamba Middle East.
Saddam kapigana na Iran kwa msaada wa hao hao wazungu, miaka 8.
Umwamba na kujiamini kulipo zidi mara kajenga kinu cha nuclear, mara kavamia Kuwait.
Hao jamaa walipomchoka, wakaamua kuwa na principle ya “give a rogue dog a bad name, and kill it”
Kweli, wakamzulia kuwa ana WMD, Weapons of Mass Destruction, kitu ambacho ni cha kuzua.
Wakasema anaweza kupiga Washington na London kwa missiles ambazo anaweza kuziset up ndani ya dakika 45.
Wakapitisha maazimio ya kumdhibiti, si bunge la Ulaya tu, bali UN Security Council.
Nia ilikuwa kumuua tu na kuangamiza dola ya Iraq.
Pamoja na huo mtego na sifa za kijinga Saddam aliendelea kutukana na kukejeli pamoja na kujigamba kuwa yeyote atakayeshambulia Iraq itakuwa “Mother of all battles”
Saddam alipogundua baadaye kuwa amezungukwa, na jamaa wamedhamiria kumpiga, akawaambia kwa kweli hana silaha za WMD, na hashambulii mtu.
Hakuna aliyemsikiliza, by then, diplomasia ikawa haina nafasi.
Tujifunze na historia, hata matukio kama haya ambayo ni ya karibuni.