Pakistan:Hatutaendelea tena kuwa kibaraka wa Washington

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,992
17,892
Pakistan: Hatutaendelea kuwa kibaraka wa Marekani
Waziri Mkuu wa Pakistan, Imran Khan ameeleza namna nchi hiyo inavyojuta kwa namna ilivyoamiliana vizuri na Marekani huko nyuma, akisisitiza kuwa Islamabad haitaendelea kuwa kibaraka wa Washington.
Khan ameyasema hayo katika mahojiano na gazeti la Washington Post na kufafanua kuwa, "Nisingependa kuwa kwenye uhusiano ambapo Pakistan inatumiwa kama bunduki ya kukodi na kurubuniwa na pesa ili ipigane vita kwa niaba ya wengine."
Waziri Mkuu wa Pakistan amebainisha kuwa, "Iwapo tusingeegemea upande wowote baada ya shambulizi la Septemba 11, naamini tungeliweza kujikwamua kutoka kwenye kinamasi tulichojiingiza. Kutokana na taifa hili kuwa mstari wa mbele katika eti vita dhidi ya ugaidi vya Marekani, tumejisababishia matatizo mengi. Mbali na watu wetu kupoteza maisha, lakini pia kumeibuka mgogoro mkubwa katika maneo yetu ya kikabila na pia tumepoteza hadhi yetu kama taifa."
Mapema mwezi uliopita, Imran Khan alimjia juu Rais Donald Trump wa Marekani baada ya kusema kuwa Pakistan haijafanya chochote katika vita dhidi ya ugaidi, licha ya kupokea misaada ya mabilioni ya dola kutoka Washington. Alsema kuwa nchi hiyo haitapigana tena vita vya kutwishwa ndani ya ardhi yake.
Agosti mwaka huu akitangaza stratijia mpya ya Washington katika kile kinachoitwa ni vita dhidi ya magaidi wa Taleban, Trump aliweka wazi kwamba Pakistan ni ngome ya maficho ya amani ya magaidi, suala ambalo liliibua malalamiko makali kutoka kwa viongozi wa Pakistan.
Kiongozi wa chama cha Awami National Party (ANP) nchini Pakistan, Asfandyar Wali Khan hivi karibuni alisema kile kinachotajwa kama stratijia mpya ya Washington kuhusiana na Pakistan na Afghanistan imesababisha kudhoofika serikali za mataifa hayo na kwamba, Trump anahusika na uchochezi wa mgogoro wa nchi hizo.
 
Kimsboy mmarekani ni kama maji utayanywa tu na ndio maana juzi kati hapa ulikuwa unalia lia dola kupanda, kama vipi tumia hela ya ayatollah
 
Hii serikali ya huyo mcheza Cricket ni ya kinafiki sana, wao ndio wanaleya magaidi hadi kuna waziri wao mkuu aliyeuawa na hao magaidi na hata Osama walimuhifadhi wao.

Pakistan hawawezi kuaminika kwani ni pango la magaidi na kamwe hawawezi kupiga vita ugaidi. Trump yuko sahihi by 100%.
 
Pakistan daima iko kote kote inawapa hifadhi Taliban wakati huo huo inawapiga Vita ili ipate mabilioni ya fedha kutoka Washington.
 
Naona huyo waziri hajipendi, sazingine us hawahitajiruhusa kufanya wanachotaka maslahi yao yakiguswa.
 
Back
Top Bottom