Pafyumu: Unajuaje....

bora puliza yenye harufu isiyo kali na pia iwapo mwenzio akikwambia kama harufu yako inakera basi jaribu kujirekebisha,mwenzetu hapa kazini tulimwambi akasema mnanionea gere wakati perfume yake inanuka majani ya muarubaini wakuchemsha, na chakukera zaid kila baada ya saa anajipulizia ndio inazidi harufu mbaya....
 
Kuna moja nilienda kwenye msiba nikaisikia, alikuwa amepuliziwa marehemu. Siku moja nikiwa mtaani nikamsikia mtu ananukia vile, nikapata picha ya marehemu
 
Tumia pafyumu kulingana na mazingira, kwa mfano unapokuwa ofisini pafyumu kali sio mahali pake, unaweza kuta Mkuu wako wa kazi hapendi hiyo pafyumu, kitakachofuata ni wewe kufanyiwa uhamisho wa kawaida ili kuboresha utendaji wako. Iila ukiwa viwanjani kama Coco Beach, tumia chupa nzima ya paffyumu kuogea maana hapo ni mahali pake.
 
hahahahaaaaa...hii imenikumbusha kuna siku niliumwa siku mbili kisa nilikaa na jamaa kwa muda usiozidi nusu saa tu kwenye daladala alikuwa 'AMEOGA' perfume yaani ni inakwangua koo vibaya mnooo...yaani mpaka nashuka home koo lote linauma..kesho yake naamka asubuhi kifua si kifua, sauti haitoki na koo linawaka moto..shati nililovaa ilibidi nilivyofika tu nilivue lifuliwe maana haikuwa kawaida...dah...sio siri nilishangaa sana ile siku..

Kuna jamaa mwingine nae huyu mpaka leo...yaani anavyokuwa anakuja tu home utajua (hata kama hajakupa taarifa) yaani akiwa nje huko unasikia harufu ya perume unajua huyooooo anakuja ...utafkiri anatembea na atmospere yake...lol.

:focus:
mimi mwenyewe natumia perfume lakini ni mpaka mtu anikaribie sna ndo anasikia harufu..isitoshe karibu 90% ya watu waliowahi sikia harufu ya perfum hii wanaisifia kuwa harufu yake imetulia na sijawahi pata malalamiko yoyote kutoka kwa mtu yoyote kuwa inamkera..hapo kabla nilikuwa natumia perfum flani hivi ila kuna watu wachache walishawahi kusema harufu yake ilikuwa inawasumbua so nikashit..
So , pamoja na mapenzi ya kitu nadhani ni vyema kwa mtu pia kutilia maanani jamii inayokuzunguka wanasema nini juu ya hilo as long as you are in it..si lazima kukubali au kukataa kila kinachosemwa lakini vingine muhimu kujichek...
 
Mi nikitumia perfumes kali najitesa mwenyewe, na nilizowah kuletewa ambazo ni kali nagawa. Nnaemgaia humpa masharti asije kwangu wakiwa amejipaka hio perfume coz nna sainus kali sana. Me mwenyewe nachagua za kupaka napenda ziwe mild hata km itanicost sana kuzinunua. Na hio ni hata kwa sabuni, lotion na hata mafuta ya nywele
 
Kuna siku nilikua pale DSE kumuulizia Broker mmoja (wakiume) nikaambiwa hayupo,,mara mdada mmoja akadakia kwa kusema,,"afadhali leo hakuja kwani pafyume yake huwa inakera.

Leo nimeingia ofisi moja kuna wadada na wanaume wanajadili mdada mmoja ambaye ni secretary,jinsi ya kumwambia, kwani pafyumu yake huwa inawakera pindi anapokatizakatiza kwenye makoridor.

Kama mjuavyo kuna brand tofautitofauti za pafyumu:-

-Sasa wakuu, hiyo pafyumu uliyotumia unajuaje kuwa haiwakeri wenzako?
-Ivi unapaka pafyumu kwasababu unaipenda au wenzako wataifurahia manukato yake?
-Unauhakika gani kuwa hujadiliwi kuhusu pafyumu unayotumia?

Kiukweli mimi huwa situmii kabisa pafyumu wala lotion,na mafuta ninayotumia ni yale yasio na harufu kabisa kama Vaseline na Nivea, yote haya kuepuka kumkwera mtu yeyote.


Mkuu angalia then usijekuwa unawakera kwa harufu asilia maana binadamu huwa hatuishi visa.
Mi perfume yangu nishagongewa like kama mara 7 hivi na wadada, mwingine ilikuwa kwenye daladala alinambia kaka naipenda perfumu yako. So I'm sure me yangu haiwakeri watu.
 
Mkuu angalia then usijekuwa unawakera kwa harufu asilia maana binadamu huwa hatuishi visa.
Mi perfume yangu nishagongewa like kama mara 7 hivi na wadada, mwingine ilikuwa kwenye daladala alinambia kaka naipenda perfumu yako. So I'm sure me yangu haiwakeri watu.

Mkuu embu itaje tuweze kukupa live za uso.
 
Back
Top Bottom