Padri na mthambi kwenye maungamo

MPAMBANAJI.COM

JF-Expert Member
Mar 2, 2011
713
331
-------- Ni kweli Mungu anasamehe lakini unapomueleza binadamu mwenzio ubaya huu unategemea ataogopa................???????????? Padri amekaa katika ki-box cha kuungamisha, kanisani hakuna mtu. Mara muumini mmoja akaingia, akapiga magoti upande wa pili na kufanya ishara ya msalaba akaanza kuungama. "padri naungama dhambi zangu, leo nimefanya dhambi kubwa sana " "endelea" "bosi wangu aliniita nyumbani kwake akaniambia amegundua nimeiba shilingi milioni 50, akasema nisipotoa maelezo ya kutosha atanipeleka polisi. Sasa ukweli mimi naogopa kufungwa, nikatazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke yetu, nikachomoa bastola nikamuua. MUNGU atanisamehe?" "utasamehewa" "Basi wakati nataka kuondoka nikasikia mlango unafunguliwa, kutazama loh, mke wa bosi. Akaniuliza nimemfanya nini mume wake. Kutazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke yetu, nikamuua na yeye. MUNGU atanisamehe na hiyo?" "utasamehewa" "nikatoka nje, nikawasha gari niondoke lakini mlinzi akakataa kufungua geti akasema amesikia kama kishindo hivi! Nikaona ananiwekea kiwingu. Kutazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke yetu nikamuua. MUNGU atanisamehe?" "utasamehewa" "nikajifungulia geti mwenyewe nikaenda nyumbani, wakati napanga kuja kuungama mtoto wa bosi akabisha hodi nikawaza mambo gani tena. Akasema amerudi nyumbani na kukuta yaloyotokea, lakini akanionyesha diary ya baba yake inayoonesha kuwa nilikuwa na appointment naye kabla hajafa. Nikamuuliza nani mwingine anajua, akasema ameanzia kwangu kisha atakwenda polisi. Nikatazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke yetu nikamuua. Diary nikaichoma moto. MUNGU atanisamehe na hilo ?" - kimya........ "padri, MUNGU atanisamehe kwa hilo ?" - kimya......... Jamaa kutazama kwenye kibox padri hayupo. Lakini kwenye kona moja akaona kabati la nguo za mapadri kama linatikisika. Kufungua akamuona padri kajificha katikati ya majoho anatetemeka. "sasa baba mbona umenikimbia?" padri kwa taabu akajibu "nilitazama huku na huku nikagundua kuwa tuko wawili peke yetu........"Kama umeipenda just ckik 'like'
 

mseseve

JF-Expert Member
Apr 3, 2011
511
88
duuuh kwelii ni nomaa hata ningekuwa mimi ningemuwahi kabla haja fanya kitendo
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

3 Reactions
Reply
Top Bottom