Padri Karugendo; Umeona Wabunge wa CCM Wanavyojipiga Mtama?

KAMBOTA

Senior Member
Mar 21, 2011
176
103

Na Nova Kambota,
Akiandika kupitia gazeti maarufu la uchambuzi nchini Raia Mwema mwandishi nguli na mwanaharakati wa siku nyingi Padri Privatus Karugendo kwenye toleo namba 196 la tarehe 27 julai 2011 Karugendo anahoji "Kwa nini tupoteze fedha nyingi kujadili "ndiyo" bungeni?".

Niliposoma makala ile nilimwelewa vilivyo padri Karugendo labda niseme kuwa ingawaje makala yake ilichota nukuu kutoka kwenye Biblia takatifu ""UKISEMA, ‘ndiyo', basi, iwe ‘ndiyo', ukisema ‘siyo', basi iwe kweli ‘siyo'. Chochote kinachozidi hayo hutoka kwa yule Mwovu" (Mathayo 5:37)" lakini acha niseme ukweli kuwa Karugendo alifanikiwa kuweka mambo hadharani bila kificho, aliweza kuonyesha jinsi taifa linavyopoteza fedha nyingi kwa vikao vya Bunge ambavyo vimetamalaki kwa unafiki wa wabunge hususani wa CCM kwa kuendesha sarakasi za chama chao ndani ya bunge.

Padri Karugendo alitoa pendekezo la kupunguza muda wa kukaa Dodoma kwa wabunge wetu na akashauri wabunge wa upinzani waanze kusambaza taarifa za kimaandishi juu ya michango yao kwenye maswala ya kitaifa kuliko kuendeleza mijadala ambayo mwisho wake huzaa NDIYO kutokana na tabia ya wabunge wa CCM kutetea chama chao na kusahau taifa, Karugendo anajenga hoja yake kwa mtindo wa swali anapohoji "yanini kwenda kujadili mambo yaliyokwishaariwa"

Naam! hakika Padri Karugendo ameibua mjadala mkubwa iwapo kweli tunahitaji bunge hili la sasa? ambalo limemezwa na hoja za ndiyo hata panapostahili siyo?

Ni ukweli usiopingika kuwa kilio cha Karugendo ni cha watanzania wengi ambao wanaamini kuwa vikao vya bunge vinavyoendeshwa kwa mazoea ya kujibu ndiyo havina maana kwa sababu hata Mungu hapendi unafiki huu!

Labda nirudi nyuma kidogo kwa kuhoji, je wabunge wa CCM wanapotetea chama chao bungeni wana maana gani? je wanamaizi kwa kiasi gani wanatukera? watafanya hivyo mpaka lini?

Huku watanzania tukiendelea kusota kwenye lindi la umasikini? hakika wanajidanganya, kwa mbali naona wabunge wa CCM wanajipiga mtama wenyewe wao na chama chao, ni swala la muda tu kama si leo basi kesho wataanguka tu, kwani mtu akijipiga mtama anategemea nini? kama si kuanguka?

Tafakari!

Nova Kambota Mwanaharakati,
+255717 709618
novakambota@gmail.com
Nova Tzdream -

Tanzania, East Africa
Agosti 10, 2011.

Mimi pia ni mmoja kati ya wapenzi wa kubwa wa mkala za ndg Karugendo na hiyo makala yake niliisoma zaidi ya mara mbili.Nakubaliana na mwandishi na kwa kuogezea tu kidogo, kwakuwa hao wabunge wa Ccm hawawezi kukubaliana na wazo la kuondoa hivyo vikao kwaajili yaposho basi nani-heri wakaacha kuwa wanachangi miswaada kwani hakuna haja kubwabwaja maneno mengi ya kukataa alfu mwisho wanakubali kwa asimia mia.

Ukweli wabunge wa CCM wamepoteza maana ya Ubunge wao kwani wamekuwa sehemu y serikali so hawawezi kujenga hoja ya kujenga nchi zaidi ni kuvaa magamba

wee acha tuu adhabu yao yaja lazima tuwaadhibu katika chaguzi zijazo bila masihara

Huyu Padri ya amma ni mshabiki wa cdm ama hajui kinachoendelea bungeni. Ni hivi majuzi tu tumeona wabunge wa CCM wakikataa (hapana) waziwazi makadirio ya wizara mbili, mpaka waziri mkuu ikabidi, moja aiombee wiki tatu ikajipange upya na moja ikaongezewa bajeti. Na pia tumeona wabunge wa CCM wakiitisha hoja ya dharura ya kuitaka Serikali itoe maamuzi ya dharura na yakakubalika na kambi zote na wabunge wote wakaunga mkono hoja na Serikali ikafanya maamuzi waliyoyataka wabunge.

Sasa hizo ndio ndio ziko wapi?

Watanzania inatakiwa tujichunge sana katika kuwasikiliza hawa mapadri kwenye mambo ya siasa, wasitufikishe walipoifikisha Rwanda na Burundi kwa chokochoko zao.

Huyu Padri ya amma ni mshabiki wa cdm ama hajui kinachoendelea bungeni. Ni hivi majuzi tu tumeona wabunge wa CCM wakikataa (hapana) waziwazi makadirio ya wizara mbili, mpaka waziri mkuu ikabidi, moja aiombee wiki tatu ikajipange upya na moja ikaongezewa bajeti. Na pia tumeona wabunge wa CCM wakiitisha hoja ya dharura ya kuitaka Serikali itoe maamuzi ya dharura na yakakubalika na kambi zote na wabunge wote wakaunga mkono hoja na Serikali ikafanya maamuzi waliyoyataka wabunge.

Sasa hizo ndio ndio ziko wapi?

Watanzania inatakiwa tujichunge sana katika kuwasikiliza hawa mapadri kwenye mambo ya siasa, wasitufikishe walipoifikisha Rwanda na Burundi kwa chokochoko zao.

Unijibu bila kukosa tafadhali, je walipiga kura au muswada uliombewa muda ukapangwe upya!

I wish wabunge at least 30% wasiwe affiliated na vyama vyovyote vya siasa! Hii ingesaidia sana kupunguza ushabiki wa vyama na kuanza kuangalia maswala ya wananchi!

I also adimire Karugendo's ways of thinking n thinking aloud!

Ni muda muafaka kwa Watanzania wote wenye uzalendo wa hii Nchi kutoa Elimu kwa Umma kuhakikisha Bunge linabalance kwamba Watanzania wasikubali kuchagua Wabunge wa Chama kimoja kutawala Bunge matokeo yake ndo haya,Bunge likibalance nguvu ya Hoja ndo itashinda otherwise tutakuwa tunatwanga maji kwenye kinu.

Back
Top Bottom