Padri amekaa katika chumba cha kuungamisha, kanisani hakuna mtu. Mara muumini mmoja

akaingia, akapiga magoti upande wa pili wa meza na kufanya ishara ya msalaba

akaanza kuungama.

Akisema "Padri naungama dhambi zangu, leo nimefanya dhambi kubwa sana"

Padri "endelea"

"Bosi wangu aliniita nyumbani kwake akaniambia amegundua nimeiba shilingi milioni

50, akasema nisipotoa maelezo ya kutosha atanipeleka polisi , ukweli mimi naogopa

kufungwa, nikatazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke yetu, nikachomoa

bastola nikamuua.

Je ! Yesu atanisamehe?"

Padri "utasamehewa"

"Basi wakati nataka kuondoka nikasikia mlango unafunguliwa, kutazama loh, mke wa

bosi. Akaniuliza nimemfanya nini mume wake. Kutazama huku na huku nikagundua tuko

wawili peke yetu, nikamuua na yeye.

Je ! Yesu atanisamehe na hiyo?"

Padri "utasamehewa"

"nikatoka nje, nikawasha gari niondoke lakini mlinzi akakataa kufungua geti akasema

amesikia kama kishindo hivi! Nikaona ananiwekea kiwingu. Kutazama huku na huku

nikagundua tuko wawili peke yetu nikamuua.

Je ! Yesu atanisamehe?"

Padri "utasamehewa"

"nikajifungulia geti mwenyewe nikaenda nyumbani, wakati napanga kuja kanisani

kuungama dhambi mtoto wa bosi akabisha hodi nikawaza mambo gani tena ! Akasema

amefika nyumbani na kukuta yaloyotokea, lakini akanionyesha diary ya baba yake

inayoonesha kuwa nilikuwa na appointment naye kabla hajafa. Nikamuuliza nani

mwingine anajua? akasema ameanzia kwangu kisha atakwenda polisi. Nikatazama huku na

huku nikagundua tuko wawili peke yetu nikamuua. Diary nikaichoma moto.

Je ! Yesu atanisamehe na hilo?"

Padri - kimya.......................................

"Padriiii, Je Yesu atanisamehe kwa hilo?"

- kimya..................................

Jamaa kutazama kwenye box la maungamo padri hayupo.

Lakini kwenye kona moja akaona kabati la nguo za mapadri kama linatikisika!

Kufungua akamuona padri kajificha katikati ya majoho anatetemeka sana.

"Sasa baba Paroko mbona umenikimbia?"

Padri kwa taabu akajibu ;

"nilitazama huku na huku nikagundua kuwa tuko wawili peke yetu........"