Padre Mapunda: Dk Slaa mwiba unaowatesa wanasiasa wengine

FreedomTZ

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2012
Posts
1,104
Reaction score
251
Amesema Yesu Kristo aliandamwa na uongozi wa Kiyahudi siyo kwa sababu alikuwa gaidi au jambazi, bali kwa sababu alikuwa ni tishio kwa mamlaka na vyeo vyao. Amesisitiza Dr. Slaa anaandamwa na CCM kwa sababu ni mwiba kwao na vyama vyenye mrengo wa CCM vinavyoamini katika siasa zisizo na faida. Kama kiongozi wa chama cha upinzani (Chadema) Dk Slaa ana mvuto wa pekee kwa Watanzania bila kujali dini, itikadi, kabila, vyeo wala tabaka la watu.
=================

Chanzo: Mwananchi
 
Huyu Bwana ni nguzo muhimu sana kwa CHADEMA na UKAWA. Endapo ataidhinishwa kuwania Uraisi mchuano utakua mkubwa sana na MaCCM ambao mpasuko wa wazi unanukia tayari katikati yao, kama hautatokea kabla utatokea baada ya uchaguzi kutokana na uhasama na kutovumiliana kunakokua sana ndani yao (wenye macho wanajua sana hili).

Iwe isiwe tuendendako alama za kuimba nyimbo mpya za ukombozi wa pili zinaonekana kwa uwazi zaidi kuliko kipicho chochote cha awali.

Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Africa.
 
Huyu padre ni mwiba mkali sana kwa CCM, anatoa elimi nzuri sana ya uraia.

Hongera Father Baptist Mapunda
 
Huyu Padre nasikia atagombea ubunge kupitia Chadema.

Padre Mapunda kwenye makala yake amesema Dr. Slaa alishaondolewa mamlaka ya kipadre na uongozi wa juu wa Kanisa Katoliki baada ya yeye kuomba. Hivyo kwa maoni ya padri Mapunda si sawa kuendelea kumwita Dr Slaa padri;hizo ni propaganda.
 
Siku hizi makanisa yamevamiwa mpaka wahuni wa vijiwenu wanajiita mapadri bure kabisa tutaanza kuwatia bakora wakileta mambo yao ya siasa kwenye nyumba za ibada.

IV UNAJUA MA PADRE WANAVYOPATIKANA AU UNAJISEMEA TU kuna TOFAUTI KUBWA KATIKA KUWAPATA MAPADRE na WACHUNGAJI. USIKURUPUKE
 
Huyu Padre sasa anaenda too far,angepaswa awe tu mpigania haki na usawa katika jamii ila kuingia kabisa hivi anakosea maana Wakatoliki anawasalisha jambo wote wanapaswa wawe na matendo mema na wapiganie usawa na haki lakin wana maono tofauti juu ya viongozi wa siasa.

Hakupaswa kwenda this far
 
Huyu Padre nasikia atagombea ubunge kupitia Chadema.

Ritz,

Usipende sana kujitoa ufahamu.Katika Miaka 15 aliyokua Mbunge ameonyesha kuwa mbunge anapaswa kufanya nini

Tatizo la nchi yetu ni mfumo mbovu wa CCM na tunahitaji overhaul na mtu wa kusimamia hili

Kwa namna ambavyo Dr.Slaa amekua akisimamia maswala ya msingi na kuonyesha weledi wa kiwango cha juu na uzalendo ndiye anayeweza kusimamia haya

Sisemi hivi kwa sababu ni kiongozi wangu kiutendaji isipokua wakati mwingine tuwe realistic

Taifa hili limepoteza mwelekeo kisera na kiitikadi


Yote yaliyosemwa na Father Mapunda ni ukweli mtupu

Na mwaka huu tumejipanga kukabiliana na wale watawala wenye hila katika zoezi zima na kilichotokea kwa wale waliochakachua matokeo ya serikali za mtaa ni rasharasha tu.

Tutawakabili kwa nguvu na kila mbinu ambazo hamjawahi kushuhudia tangu tupate uhuru na tutatoa fundisho kwa mamlaka nyingine Afrika

Haki za kiraia na Demokrasia haziwezi kuhujumiwa kisha wahusika wakapona hivihivi
 
Last edited by a moderator:

ILA KUMBUKA KAMA KWELI UNA MCHA MUNGU HUWEZI KUWA au KUIPENDA CCM, INAENDA KINYUME NA MAAMRISHO MENGI YA MWENYEZI MUNGU
 
Kwa hiyo kama Slaa ana matendo kama ya Yesu basi panapo mfaa ni kanisani zaidi kuliko Ikulu!

Lakini si shangai Mapadri kupigiana chapuo...nasubiri mpambano kati ya CUF na Chadema!

Nchi hii haito ongozwa na kiongozi wa dini!
 
Huyu Padri ataleta ugomvi kati ya CUF na Chadema.
 
Ni ngumu sana kutofautisha Kanisa na Chadema.

Huo udini utakufikisha wapi? Tuna waislam na hata wasiokua na Dini ndani ya Chadema

Mlisema Chadema ni cha wakristo kisha CUF ya Waislamu sasa CUF na CHADEMA vyama vya wakristu na Waislam wameungana ina maana CCM ni chama cha wapagani?

Achana na siasa hizi kaka.Nigeria hali tete kwa sababu ya ujinga huu
 

tatizo ccm hawapendi ukweli, hongera father b mapunda
 
Kwa hiyo kama Slaa ana matendo kama ya Yesu basi panapo mfaa ni kanisani zaidi kuliko Ikulu!

Lakini si shangai Mapadri kupigiana chapuo...nasubiri mpambano kati ya CUF na Chadema!

Nchi hii haito ongozwa na kiongozi wa dini!

Badala ya kujenga hoja unaombea UKAWA mabaya
 

Mngekuwa hamuendekezi njaa na kuhongwa kirahisi maneno yako ningeyaamini
 
Last edited by a moderator:
Siku hizi makanisa yamevamiwa mpaka wahuni wa vijiwenu wanajiita mapadri bure kabisa tutaanza kuwatia bakora wakileta mambo yao ya siasa kwenye nyumba za ibada.

Mbona nlishindwa kuchapa viboko wale wachungaji njaa waliokuwa kwenye binge maalum la katiba?Au ni kwa kuwa ni vibaraka wa ccm?
 
mkiona neno dr. Slaa makalio yanatikisika...

hauoni safu ya viongozi wa kanisa mkuu.

1) padre mapunda

2) padre slaa

3) mchungaji msigwa

4) mchungaji israel natse

na wengine wengi.

mungu yupi kamanda? Huyo mungu wa chadema amekubali kabisa chadema kiwe chama cha upinzani.

mkuu kumbe chadema hakuna masheikh.

huyu padri ataleta ugomvi kati ya cuf na chadema.

hivi ccm imewatuma kutetea dini gani? Ccm imewatuma kupinga dini gani? Hivi ccm inapigania dini gani? Mnataka kusema chochote kinachofanywa ndani ya ccm tukiangalie kwa jicho la kidini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…