Mauaji yoyote hayafutiki. Ndiyo maana mpaka leo, tunaendelea kwa nyakati tofauti kukumbuka maujibyaliyofanywa na Hitler, Musolin, Stallin.
Kwa bahati, nchi yetu kabla ya utawala huu wa sasa, hakuna utawala uliowahi kufanya mauaji ya kutisha kama haya yaliyotokea. Amekuwa wa kwanza rais mwanamke, amekuwa wa kwanza kuua watu kwa maelfu, amekuwa wa kwanza kufuguliwa kesi ICC. Ni rekodi mbaya kabisa kwake mwenyewe, familia yake, uko wake, kwa Zanzibar na kwa taifa zima.
Ni muhimu sana kwa taifa, kutafakari kwa umakini mkubwa wa haya yaliyotokea ili kamwe yasitokee tena, wala kiongozi au wakuu wa vyombo vya ulinzi wenye kuruhusu haya, kamwe wasitokee tena.
Nchi imetiwa doa, familia zimepewa majeraha yasiyofutika, taifa limepakazwa damu, hii ni laana kubwa ambayo kama taifa tunatakiwa kuondokana nayo kwa hekima: kwanza kwa kuukiri uovu uliotokea, kisha kuujutia na hatimaye kuweka dhamira ya kutoruhusu utokee tena.