Padre amwagiwa Tindikali huko Zanzibar

Padre amwagiwa Tindikali huko Zanzibar

Status
Not open for further replies.

Informer

Platinum Member
Joined
Jul 29, 2006
Posts
1,611
Reaction score
6,720
Wana JF,

Nina habari mbaya za Padre Mwang'amba wa Kanisa Katoliki Zanzibar kumwagiwa tindikali huko Mlandege katika cafe ya Sun Shine.

More info to follow.

--------------------------------------
attachment.php

1236877_576695175709486_940245755_n.jpg


6126722_orig.jpg


Sept 14, 2013:
Padri wa Kanisa la Romani Katoliki Parokia ya Machui, Joseph Monesmo Magamba amemwagiwa tindikali na watu wasiojulikana katika Mtaa wa Mlandege jana jioni, Mkoa wa Mjini Magharibi, Zanzibar.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Haji Hana alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba kiongozi huyo wa dini amelazwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja, akiendelea na matibabu baada ya kujeruhiwa usoni, kifuani na mikononi.

Hana alisema kwamba Padri Magamba (60) alikuwa akitokea katika duka la huduma za mawasiliano ya mtandao la Shine Shine saa 10.15 jioni na watu waliommwagia walimtega mlangoni kabla ya kufanya uhalifu huo na kutoweka kwenye vichochoro vya Mitaa ya Mtendeni na Mchangani.

Alisema polisi wamestushwa na tukio hilo kwa vile limetanguliwa na matukio matatu ya kumwagiwa tindikali kwa viongozi wa dini na kuwataka wananchi kutoa ushirikiano wa kufanikisha kuwakamata watu wanaojihusisha na vitendo hivyo.

"Tumeanza kufanya uchunguzi ikiwemo kuchukua maelezo ya majeruhi, tungependa zaidi kupata msaada wa kitaarifa kwa watu walioona na wanaojua mahali walipo watu wanaofanya vitendo hivyo," alisema Hana.

Mfanyakazi wa Duka la Huduma za Mawasiliano ya Mtandao, Rukia Yahya Abass alisema anamtambua Padri Magamba kama mteja wake wa muda mrefu na huja dukani hapo nyakati za asubuhi au jioni kwa ajili kupata huduma za mawasiliano.

Rukia alisema ameshtushwa kuona padri huyo baada ya kumaliza kupata huduma na kutoka nje akipiga mayowe ya kujeruhiwa.

"Nimezoea kumwita father au babu, ni mteja wangu kwa kweli, nilimwona akirudi tena ndani huku akiomba msaada, watu waliokuwa katika mtandao harakahara wakammwagia maji, alikuwa akilalamika kwa ukali wa maumivu," alisema Rukia akiwa na huzuni.

Alisema wasamaria wema ndiyo waliomchukua na kumpeleka hospitali. Kabla ya tukio hilo alilipa gharama za huduma ambazo zilikuwa ni Sh2,000 na kurudishiwa chenji yake baada ya kutoa noti ya Sh10,000.

Daktari Jamal Adam ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Mnazi Mmoja alisema kwamba Padri Magamba amepatiwa huduma ya kwanza na anaonekana amejeruhiwa usoni, mikononi na kifuani.

"Ni mapema mno kusema ameathirika kwa kiasi gani kutokana na tukio hilo, tunaendelea na juhudi za kumtibu, "alisema Dk Jamal.

Huu ni mfululizo wa visa vipatavyo vinne vya kikatili ambavyo vimefanyika Zanzibar, vikiwalenga watu maalumu katika kipindi cha miezi 10 iliyopita.

Desemba mwaka jana, watu ambao bado hawajafahamika wamlipiga risasi Padri Ambros Mkenda wa Kanisa Katoliki la Mpendae mjini Zanzibar na kumjeruhi vibaya.

Februari mwaka huu aliuawa kwa kupigwa risasi kichwani, Padri Evarist Mushi wa Kanisa Katoliki katika eneo la Mtoni, Mkoa wa Mjini Magharibi.

Agosti mwaka huu wasichana wawili, raia wa Uingereza waliokuwa walimu wa kujitolea, walimwagiwa tindikali na kujeruhiwa kifuani, shingo na uso.
 
Du tuendako cpati picha, na tukifika cjui tutakuwa na Hali gani.
 
Hayo mambo yanafanywa na waislamu,dalili zote ni wao.
Huku bara hatumwagii mapadri tindikali wala shehe.HAO WAISLAMU WANAOFANYA HAYO hawawezi kulazimisha kueneza uislamu kwa njia za kipuuzi kama hizi.
 
Wana JF,

Nina habari mbaya za Padre mmoja wa Kanisa Katoliki kumwagiwa tindikali huko Mlandege katika cafe ya Sun Shine.

More information to follow


Muungano uvunjwe, machogo hamtakiwiiiiiiii
 
Tunalea ujinga na Kanisa linaendelea kuomba serikali dhaifu kuchukua hatua!! Kanisa lichukue hatua ngumu kidogo kukomesha hili! Nikisema hatua ngumu kidogo najua jinsi Kanisa linachoweza kufanya ktk mazingira hatarishi kuinjilisha au hata imani za waamini kuwa mashakani na hofu kuu.
 
anaitwa Ancelmo Mwang'amba wa parokia ya Chelu.
 
breaking news ITV. padri ancelomu mwang'ambwa wa parokia ya cheju zanzibar amemwagiwa tindi kali. kwa habari zaidi stay tuned on ITV news
 
Mpaka wawamalize au muwachie wapumuweeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee! bila shaka wanaagiza tindikali kwa mameli, na wanayo nyingi wala haiishi, mtakwisha nyinyi.
1371450_10200746553170104_445747008_n.jpg
 
Padri wa kanisa
Katoliki Parokia ya Cheju
Zanzibar,Joseph Mwangamba
amemwagiwa tindikali na kujeruhiwa
usoni na kifuani
source..East Africa Radio.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom