Package ya ndoa

Package ya ndoa

Artifact Collector

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2019
Posts
6,622
Reaction score
10,254
UPENDO
Ndoa lazima iwe na upendo usio na mipaka Kwa pande zote mbili, (unconditional love) ukiingia kwenye ndoa Kwa kumpendea mtu kitu fulani siku hiko kitu kikiwa hakipo upendo utaota mbawa

TENDO LA NDOA
Hakuna kitu kizur kufanya tendo LA ndoa na mtu ambaye unampenda, na sehemu zenu za siri kiwa zinafit na sio zinapwaya hamuwez chokana

KUSITIRIANA
Wanadamu wote tuna mapungufu na huwez ondoa mapungufu ya mwenzako bali unaweza yasitiri, ili ndoa idumu ni lazima kila mmoja a-handle mapungufu ya mwenzake. Na sio kwenda kuwatangazia marafiki zako mapungufu ya Mme/mke wako hilo ni kosa kubwa ambalo watu wengi wanafanya

KUENDANA KAULI
Kwenye ndoa mkiwa watu wa kupishana kauli hakika hio ndoa haitadumu kamwe, jitihid kuoa au kuolewa na MTU ambaye hamtapishana kauli mara Kwa mara

KUJISHUSHA
Mwanaume unampomkosea mke wako jitaidi ujishushe na kumuomba msamaha, hivyo hivyo Kwa mwanamke hii nayo pia itasaidia ndoa kudumu


KUVUMILIANA
Kama nilivyosema kwenye kusitiriana, hakuna ndoa isiyo na matatizo hata moja, na hii ni kutokana na ukweli kwamba wanavumiliana

USIRI
Kwenye ndoa lazima kuwe na usiri, ni hatari sana kila kinachotokea kwenye ndoa unaenda kushare na marafiki zako, au wengine wanaenda mbali wanashare siri zao za ndoa kwenye mitandao ya kijamii hill ni kosa kubwa sana.

KUWA NA MTIZAMO MMOJA WA MAENDELEO
Kama kila mtu akiwa na mtizamo tofaut wa maendeleo itakua in ngumu sana kuleta maendeleo katika familia

KUACHA KUIGA MAISHA YA NDOA YA WATU WENGINE
Mfano kuna watu wakimuona Michele na Obama wanataman ndoa zao ziwe vile, hilo ni kosa kubwa ishi na make au Mme wako jinsi alivyo
 
Ndoa ni wito,kama huna wito ukilazimisha lazima itavunjika tu.
 
Back
Top Bottom