Oysterbay na wanamazingira feki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Oysterbay na wanamazingira feki

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Macos, Mar 9, 2010.

 1. Macos

  Macos JF-Expert Member

  #1
  Mar 9, 2010
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 1,831
  Likes Received: 1,004
  Trophy Points: 280
  WANAMAZINGIRA FEKI” NA UENDELEZWAJI WA VIWANJA VYA UFUKWENI ENEO LA MASAKI
  Hivi karibuni Halmashauri ya Kinondoni kwa ushauri wa Rais Kikwete, kuhusu umuhimu wa kuviendeleza viwanja vya wazi eneo la Masaki waliligawa eneo hilo kwa ajili ya kuendelezwa, na makampuni 6 yalipewa kazi ya kufanya hivyo.
  Cha kushangaza kampeni chafu ‘ati’ ujenzi huu utaharibu mazingira ya eneo hilo ? hivi ni kweli ? na ‘ati’ waswahili watakosa sehemu ya kukoga??? Huu ni uongo kwani sehemu ile iko juu ya usawa bahari, eneo lote kutoka Seacliff mpaka Golden tulip kuna bonde kuteremkia bahari na hakuna mswahili wala mzungu anaeogelea sehemu ile!!!! Pale wapo wavuta unga na bangi na vibaka ndio mafichio yao .Hawa “wanamazingira’ feki wanamdanganya Mkuu wa Mkoa ati waswahili watakosa sehemu ya kuogelea SIKU ZA SIKUKUU!!

  Ukweli wa mambo fukwe yoyote isipoendelezwa basi mmomonyoko wake ni wa kasi zaidi.hii ipo wazi tangu wakati ule Sumaye apige marufuku kupumzika eneo la Oysterbay basi sasa hivi ile minazi ilobaki ipo ndani ya bahari!!!! Si ajabu miaka kama 10 ijao bahari hio itapiga hodi kwenye barabara .
  hebu tuchukue mfano wa wazi…kuna mazingira gani yaloathirika na uwepo wa Police mess pale Oystebay/Masaki ?? Ipo pale zaidi ya miaka 40 watumabie…mazingira gani yameatirika zaidi ya kuizuia erosion ? kama isingekuwepo basi bahari ingekula ile eneo.
  Kuna sea cliff hotel na golden tulip ubaya gani na mazingira gani yameathirika? Bali eneo limependeza na serikali pamoja na halmashari zetu zinapata kodi.
  Lipo eneo ambalo mimi nadhani kweli linaharibu mazingira…nalo ni Coco beach…huyu kajenga banda lake bila kuzingatia uharibifu wa mazingira lakini hawa watu kimya!!! Kuna tahadhari gani pale imechukuliwa? MACHUPA YA ULEVI NA CONDOMS ZIMEZAGAA SEHEMU YA COCO BEACH !!!!!!!!!
  Mbali na kuharibu mazingira ni eneo maarufu kwa uvutaji bangi na kubwia unga….lakini hawa watu wa mazingira kimyaaaaa
  Unajua serikali ya awamu ya tatu iliuza nyumba za serikali na nyngi zipo Masaki na Oystebay na haw ndio wanaopiga kelele , kisa nyumba nyingi hizi zimegeuzwa store za pombe..tena nje..na hawa watu wamazingira hapa sio ishu….leo ukipita maenea haya utadhani upo maeneo uwanja wa fisi..pita tu usiku utajionea….hawa wanaogopa kuanguka biashara zao za pombe ….
  Tuangalie mfano wa mji wa zanzibar sio mbali”

  Zaidi ya miaka 300 ndio hapa palijengwa Zanzibar !!! mji unapendeza na bahari inapendeza…..hakuna mazingira yalioathirika..
  Na tuangalie London….Thames River ilivojengwa??? Unafikiri kama hawakuendeleza fukwe hizi leo london yote ingemegwa na maji…
  Angalieni Zanzibar,Manahattan pale nenda Hongokong….Dubai….na sehemu nyingi…amabazo miji yao imejengwa maeneo ya bahari…hakuna hii sheria ya kutojenga mita 60 kutoka ufukweni….watalaam wetu wamesoma lakini wanatia aibu kutunga sheria pofu kama hii…Mungu ametupenda kutupa bahari….lakini uchoyo umetupofua….  Angalia chini jinsi Zanzibar walivoendeleza Beach area yao?? Hapa sio ulaya ni Forodhani park Zanzibar.  Mambo mengi ya nchi hii hayendi kwa kuwasikiliza watu ambao wana uchoyo na wabinafsi..hawajali maslahi ya nchi…watu hawa huwa na visingizio kibao wanapo pinga kitu cha maendeleo …..
  Huu mji unahitaji maeneo kama haya ya forodhani ya zanzibar pale Oysterbay….ili watoto wapate sehemu ya kweli kupumzika wakati wa sikukuu…NA SIO SEHEMU ISOKUA NA MIPANGILIO ZAIDI YA KUWEKA ULEVI KILA SEHEMU .lakini pia serikali itapata kodi ……
  Mimi nampa 5 Mzee Mwinyi…watu wanasema alikua mpole lakini alifanya maamuzi ya kweli na busara ..na yanayozingatia maslai ya nchi alipo ruhusu ujenzi wa hotel ya Sheraton wakati ule ,sasa Movernpick ..Walikuwepo watu kama hawa wa Masaki….kupinga na kila sababu za kijinga..chambilicho Nyerere watu kama hawa hakusita kuwaita ‘wajinga wajinga’
  Cha kushangaza hata gazeti la daily news limeingia katika mtego huu wa kupinga kuendeleza mji…
  Pia alitoa kibali ujenzi wa Golden tulip..ipo pale na watu wanaoshi Masaki kama yupo aloathirika aseme…..pia aliruhusu Seacliff kujengwa….mbali maeneo mengi ya Kawe najamngwani beach..Whitesands,Water world, Kunduchi water park ..
  Walipinga sana watu hawa…lakini hakuwasikiliza…..alijua wanasumbuliwa na choyo.sio wakweli…hawana utafiti wa kitaalaam unaonesha uharibifu utao tokea…


  Point yangu ni kwamba faida kwa taifa ni kubwa zaidi kama maeneo yale yataendelezwa..yakichwa basi hakuna zaidi ya kutumiwa na wabwia unga….
  Na ni wakati wa Rais kutoa kibali na amri kuendeleza hayo maeneo…na utaratibu ufanywe eneo la oysterbay mpaka cocobeach ligeuzwe Park kama forodhani Zanzibar hapa chini jionee

  Hii ni beach ya forodhani sio….pengine


  Hata sehemu ya watoto ipo beach!!!..hapa ni zanzibar…

   

  Attached Files:

 2. RRONDO

  RRONDO JF-Expert Member

  #2
  Mar 10, 2010
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 25,825
  Likes Received: 20,813
  Trophy Points: 280
  nimeipenda hio forodhani beach,kama eneo lile kuanzia SEA CLIFF HOTEL-GOLDEN TULIP litaendelezwa kwa mfano wa forodhani ni wazo zuri kwani kutabaki kuwa open space kwa public, lakini kukijengwa hotel tena watu watakosa sehemu za wazi kupumzika kama tunavyojua open spaces ni chache sana hapa DAR
   
 3. M

  Mchili JF-Expert Member

  #3
  Mar 10, 2010
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Watu walitaka kutumia ushauri wa raisi vibaya. Raisi alishauri yale maeneo yaendelezwe lakini yabakie kuwa accessible kwa public. Anaeendeleza alitakiwa kufuata utaratibu, atoe mpango wake na ramani na uchambuzi yakinifu kuelezea jinsi atakavyofanya bila kuharibu mazingira kwa vyombo husika. Sio kukurupuka kinyemela kupima viwanja, kugawana kinyemela na kuanza ujenzi. Hiyo sio sahihi na wala sitegemei kama tungepata kitu kinachofanana na forodhani.

  Mfano mzuri nenda Mbezi beach barabara ya africana uone kilichojengwa ufukweni. Ni ufisadi mttupu. Badala ya kutengeneza mandhari ya kupumzika ya beach yamejengwa maghorofa ya hotel za kitalii na access ya kuingia baharini imezibwa mpaka upitie kwenye hizo hotel kwa kiingilio.

  Bado wazo la raisi linaweza kutekelezwa kwa uwazi zaidi na umakini na likawa na manufaa yaliyokusudiwa. Hata eneo la Masaki lililozuiwa linaweza kuendelezwa kama wahusika wakiweka hila pembeni na kufuata utaratibu.

  Acheni hujuma na ubinafsi na sio msingizie ati kuna kampeign chafu.
   
Loading...