Over drive button

hii topic kila kukicha inanzishwa, halaf natoka kappa

sasa correct me if am wrong: Ile taa kwenye dashbod haitakiwi iwepo ili u-save mafuta, sawa au sio sawa?
Naommba jibu liwe tu sawa au sio sawa ili musiendeleee kunichanganya
sawa kabisa
 
Jitahidi hapo kwa upande wa kulia usiwe unavuka vuka sana hadi namba tatu kwa safari ya mbali, vinginevyo utakuwa unatumia mafuta mengi sana kwa kilomita,maili chache

kumbe ila nikifanya hivyo si hata Alteza zinanipita na kunidharau BMW X5 ?? :shocked:
 
Asanteni kwa kutuelimisha matumizi ya over drive. Je hii D2 inatumika wakati gani? Na unavyotumia hiyo D2 over drive iwe OFF au ON?
Naomba kuwakilisha hoja.
 
kwa kuongezea hapo kuna D,2,L je niwakat gan natakiwa kutmia 2 na L?

L ni low utaitumia hii kama unavuta gari au trailer,utaanza na low gari ikitembea kidogo unaweka 2 then ikichanya kidogo unaweka D. unaweza pia kutumia hii kushuka au kupanda mlima mkali

2 hii inaruhusu gear kubadilika 1-2 only unaweza kuitumia kuvuta gari au kushuka/kupanda mlima mkali ili usitegemee sana brake,baadae unaweka D safari inaendelea.

kuna gari nyingine zina L,3,4,D huwa natumia 3 badala ya D nikiwa namfundisha mtu kuendesha kwa sababu hata akanyage vipi gear zitaishia namba 3
 
kumbe ila nikifanya hivyo si hata Alteza zinanipita na kunidharau BMW X5 ?? :shocked:

Kama unapenda mibio kamua baba, ila hapo nilipotaja mimi spidi 120 ndio ya kiusalama zaidi, kama unajali maisha yako, familia n.k

Sawa kiafya gonga hadi kwenye (4) au zaidi ya hapo kidogo sio mbaya

Na hiyo x5 nina uhakika kila ukikanyaga unaona hamna kitu, ila ukiangalia kisahani ndio utajua unatambaa

Kama kistarehe labda kutembelea familia au vekesheni basi mdogo mdogo raha sana halafu uwe na mwenzio

Lakini kama una dharulula kamua baba
 
Hii topic kila kukicha inanzishwa, halaf natoka kappa

Sasa correct me if am wrong: ILE TAA KWENYE DASHBOD HAITAKIWI IWEPO ILI U-SAVE MAFUTA, sawa au sio sawa?
Naommba jibu liwe tu SAWA aU SIO SAWA ili musiendeleee kunichanganya

Kwa maneno rahisi ni kwamba unapoona ile sign ya OD/OFF kwenye dashboard yako manake inakuelekeza kwamba unaendesha gari yako kwenye OD na kama hutumii hiyo OD you just put if OFF kwa kubonyeza kitufe cha OD na hiyo taa iliyokuwa inawaka kwenye Dashborad itazima kuashiria kwamba hutumii hiyo OD.Kwa hiyo hayo maneno OD/OFF ni agizo la kukutaka kutoa OD kama huitumii.Hiyo unaweza kuifananishA na taa ya OIL au FUEL inapowaka manake ni kwamba oil au Fuel imepungua,na dawa pekee ya kuondoa hiyo taa isiwake kwenye Dashbord ni kuongeza Oil au Fuel
 
hapa naona watu wengi wanachangaya.naomba unisome kwa makini.

ukibonyeza OD button maandishi mekundu OD OFF yanatokea maanake umezima OVER DRIVE.je nini kinatokea? tuanze na maana na kazi ya OD

OD kwa maelezo mafupi ni mfumo unaofanya gear box ku-override engine,maanake ni kuwa gari inabadili gear kabla engine haijafika maximum revolution per minute na kwa kufanya hivi unasave mafuta nastrain kwenye engine.kwa hali ya kawaida tunaendesha gari ikiwa OD ON ndio maana unaweza kufika gear namba tano ukiwa 60km/h na rpm 1500/2000 kutegemea na gari.

kwa upande mwingine ukibonyeza ile OD button OD inakuwa OFF kwahio utapata max power kwa sababu gear box haita-OVERRIDE ENGINE na gear hazitabadilika mpaka ufikie max engine rpm for particular gear hence max power as well as max fuel use.

kwahio kama unataka more speed in short time switch off the OD by pressing that botton and OD OFF will appear on your dashboard. but for normal drive leave it ON hence no sign on your dashboard.
 
Kama unapenda mibio kamua baba, ila hapo nilipotaja mimi spidi 120 ndio ya kiusalama zaidi, kama unajali maisha yako, familia n.k

Sawa kiafya gonga hadi kwenye (4) au zaidi ya hapo kidogo sio mbaya

Na hiyo x5 nina uhakika kila ukikanyaga unaona hamna kitu, ila ukiangalia kisahani ndio utajua unatambaa

Kama kistarehe labda kutembelea familia au vekesheni basi mdogo mdogo raha sana halafu uwe na mwenzio

Lakini kama una dharulula kamua baba

wacha niwe nakamua hivyo hivyo washike adabu wa vigari vidogo japo maumivu yake ya spear na mafuta najua mwenyewe rohoni kwangu. :tinfoil3:
 
wacha niwe nakamua hivyo hivyo washike adabu wa vigari vidogo japo maumivu yake ya spear na mafuta najua mwenyewe rohoni kwangu. :tinfoil3:

Umenichekesha sana Mkuu. Eti bwana, gari yako mwenyewe, maumivu ya mafuta na spea ni yako mwenyewe! KAMUA tu. Mie nina ka X-Trail kenye Turbo, kanakula mafuta hako, lakini mwendo acha kabisa! Nami nakamua tu!
 
Nilikuwa nimeshaanza kuelewa sasa mmenichanganya tena.........niendeshe taa ikiwaka O/D off au isiwepo hiyo taa.......?

endesha gari yako TAA IKIWA IMEZIMA........ndio inavyotakiwa ile taa kuwaka waachie wanaopenda mashindano barabarani.

make sure U DONT SEE O/D OFF on your dashboard.
 
Hii topic kila kukicha inanzishwa, halaf natoka kappa

Sasa correct me if am wrong: ILE TAA KWENYE DASHBOD HAITAKIWI IWEPO ILI U-SAVE MAFUTA, sawa au sio sawa?
Naommba jibu liwe tu SAWA aU SIO SAWA ili musiendeleee kunichanganya

SAWA.

uliza lingine nikufahamishe.
 
Kwa jinsi nilivyowaelewa wadau hapo juu ni kwamba ukiwa unaendesha ktk mazingira ya kawaida taa HAITAKIWI kuwepo (i.e hapo ndipo OD inakuwa ON - to save fuel) ila kama unataka ku-overtake au kupanda mlima taa INATAKIWA kuwepo (i.e hapo ndipo OD inakuwa OFF - fuel consumption inakuwa kubwa na unapata rpm kubwa, mwendo wa gari unaongezeka).

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums

correct.
 
button ya OD mm ninavyoelewa inafanya kaz kwa approach sawa na magari yenye turbo ambapo kwa magar ya turbo huwa yanafungua yenyewe automatically gari inapofikia speed limit flani na na mwendeshaji anahitaji mwendo zaidi hii husave mafuta na speed huongezeka na nguvu pia. ninavyoona tofauti ya turbo na hiyo button ya OD ni kwamba turbo inafunguka automatic na OD unapress manually.
 
ndugu,hivyo ni vitu viwili tofauti,turbo iko kwenye engine na OD iko kwenye gearbox
 
ndugu,hivyo ni vitu viwili tofauti,turbo iko kwenye engine na OD iko kwenye gearbox

naweza kukubali kwamba ni vitu viwili tofauti lakini vinafanya kaz inayofanana tofauti ni location vilipowekwa ndugu. naomba pia nikuulize swali dogo tu, kwani kinachoongeza speed ya gari ni injini ya gari au ni gear box? ninavyoelewa gear box inategemea rotation ya injini kaz ya gear ni kuamplify au kureduce mwendo wa gari kulingana na rotation ya injini ndio maana rpm imesetiwa kwenye injini na sio kwenye gear box ndugu
 
Back
Top Bottom