Ulitegemea nini kipya kutoka kwa Mh. Waziri, wakati JK mwenyewe alisaula bungeni kwa kusema wabunge wameongeza ajira za MAHAUSIGELI ?
Wakati wa bajeti alisema kuwa serikali ilikuwa imetengeneza ajira laki nne unusu tu. Ina maana kati ya Julai mwaka jana na sasa zimetengenezwa ajira takriban laki nane... najihisi niko nchi ya KUFIKIRIKA
Ndio inaweza kuwa hiyo figure ni kweli but wengi waliopata hiyo ajira ni
Walimu wa CRUSH PROGRAM-miezi 3
Askari POLISI
Askari JWTZ & JKT
Askari MAGEREZA
Mkuu Bello, Waziri amesema walipata kazi ni kwenye sekta binafsi ni 1,233,747 sawa na 97% siyo upolisi wala uwalimi Mkuu! watu millioni 1 si mchezo mwanangu.
wakati mwingine..mawaziri wa kikwete na yeye mwenyewe wanatia kinyaa kujaribu kutuambia mafanikio ambayo hayaonekani na ni ya kufikirika....mimi ningefurahi sana kama jk kwenye hii kampeni ya kuuelezea mafanikio yake angeweka zile taarifa za kweli tu..kuliko hesabu za kupika......sasa angalia anasema asilimia 97% sekta binafsi...kwani angesema wamepata ajira laki 5..ambapo inakaribia na ukweli...na miongoni mwao askari na walimu laki moja ...ingekuwaje.............
mahesabu ya kapuya ni kaama ya yule mama waziri wa utumishi aliyesema ameokoa bilioni 3 za watumishi hewa bila justifications...
mbona wakati wa utawala wa mkapa hakuwa na haja ya kuandika mafanikio kwenye magazeti kama haya ya kupapasa.......aaache kupiga makelele ,aache watu waone wenyewe!
Mkuu Bello, Waziri amesema walipata kazi ni kwenye sekta binafsi ni 1,233,747 sawa na 97% siyo upolisi wala uwalimi Mkuu! watu millioni 1 si mchezo mwanangu.