Our real problem is not our strength today | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Our real problem is not our strength today

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Recta, Feb 27, 2009.

 1. Recta

  Recta JF-Expert Member

  #1
  Feb 27, 2009
  Joined: Dec 8, 2006
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  "Our real problem is not our strength today, it is rather the vital necessity of action today to ensure our strength tomorrow."

  Niliwahi kuombwa na ndugu Amani Noni kufafanua maneno hayo hapo juu. Hii hapa chini ni quote yake.

  Kama alivyosema Amani hapo juu, ni kweli kuwa quote hiyo (Our real problem is not our strength today, it is rather the vital necessity of action today to ensure our strength tomorrow) inaweza kuandika kitabu kama ikitakiwa kutolewa maelezo. Ila naamini pia kuwa inajitosheleza kwa kiasi kikubwa. Kwa kuwa ameniomba nielezee, mimi nitafanya hivyo kwa maneno machache, nikiamini pia kuwa wachangiaji wengine watajitokeza kuongezea zaidi.

  Wakuu, We have problems, we have always had problems. Our problems lies not in what we cannot do, but rather in what we do not want to do. Wapo waliowahi kusema, "unachokula leo ndio kitakachokujenga kesho".

  Watu wengi huogopa kujaribu, wakidhani kuwa hawana uwezo wa kufanya mambo makubwa (usipojiamini mwenyewe kwanza, si rahisi kuaminiwa), na wakati mwingine hukosa nia thabiti ya kufanya mambo makubwa yanayoweza kusababisha mambo mazuri zaidi kwao wenyewe na kwa jamii zao na hata kwa Taifa lao.

  Mara nyingi tumesikia watu wakilalamikia hali ngumu ya maisha, uhaba wa hiki na kile, ubovu wa miundo mbinu, matendo yasiyokubalika yanayofanywa na watu mbalimbali katika jamii, mifumuko ya maradhi, madawa ya kulevya, vifo vinavyoweza kuzuilika, ukosefu wa haki na mambo mengi mengine. Ukiangalia hatua zinazochukuliwa kukabiliana na mambo hayo yanayowakera/kuwasumbua watu, utagundua kuwa hakuna jitihada za maana zinazochukuliwa au kufanyika. Hali inazidi kuwa mbaya, na kadiri watu wanavyoongezeka, ndivyo matatizo yanavyoongezeka pia. Imani yangu ni kuwa, "ukiahirisha tatizo, basi utakapoamua kulitatua, litakuwa limeshakuwa tatizo kubwa zaidi kuliko wakati ulipoliahirisha".

  Kila mtu ana uwezo wa kipekee wa kuleta mabadiliko chanya katika jamii yake, endapo atakusudia kufanya hivyo. Hata kama mtu ana matatizo kiasi gani, anao uwezo wa kuamua kuyakabili matatizo yake, na kuwa na hali bora zaidi. Kuamua kushindwa kabla hujashindwa ndio kushindwa kwenyewe.

  Even drugs addicts, if they decide to quit however hard it is to do so, they should know that some people have accomplished it before them. Mafanikio huleta faraja kubwa katika maisha. Kila mtu anayo stahili ya kufurahia maisha kwa kuamua kufanikiwa. Anachotakiwa kufanya ni kuamua kufanikiwa, kuweka mipango thabiti ya kufanikiwa, na kuchukua hatua za kufikia malengo yake. Perseverance towards set goals and to pursue the goals diligently is a way to success.

  Optimism, self-leadership and action plans can help in focusing efforts and get anything accomplished on time, in desired quality and cost. By directing thoughts to find solutions and accomplishing them, you will not only increase performance, but also rid yourself from unnecessary stress.
   
 2. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #2
  Feb 27, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  tatizo ni kuwa ni vigumu kuanza kufikiria kuhusu tomorrow, na jinsi ya kuishughulikia 'today' wakati 'today' tuna matatizo ambayo yanahitaji ufumbuzi wa haraka na tunashindwa kuyatatua. Kwamba, even today, we are weak
   
 3. Recta

  Recta JF-Expert Member

  #3
  Feb 27, 2009
  Joined: Dec 8, 2006
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Ni kweli Mpita Njia kwamba, leo tuna matatizo mengi. Ila si kweli kuwa hatuwezi kuyashughulikia. Nia hatuna, ila uwezo tunao. Kinachotakiwa sasa, ni kuanza kushughulikia matatizo tuliyonayo bila kuogopa ukubwa wa matatizo yenyewe na pia bila kuogopa wingi wake.

  Mkuu siamini kuwa tuko weak kiasi hicho. Naamini weakness yetu pekee ni kuamua kuamka baada ya kuanguka. Unajua mkuu, ukiamua kufikiri kuwa unaumwa, ukaamini kuwa u-mgonjwa, ni dhahiri kuwa utakuwa mgonjwa. Ni maswala ya psychology zaidi ya hali halisi. Kuna mataifa amabayo yalikuwa weak kuliko sisi wakaamua kujikwamua kutoka kwenye weakness zao na sasa ni strong wa kuigwa na kutamaniwa.

  Matatizo yote yana solution.
   
 4. M

  Mkandara Verified User

  #4
  Feb 27, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Recta,
  Mkuu labda niongezee kwa mifano hai kulingana na mazingira yetu..lakini sina hakika kama nami nipo ktk fungu la wananchi ambao hawakufahamu maana ya maneno hayo..Isije kuwa asiyejua maana haambiwi maana! heee heee hee!

  Kifupi mtu anapo ku bully kila siku shuleni au mtaani ni dalili za unyonge wako lakini sio kipimo cha nguvu zako kwa sababu hupigani kujibu mashambulizi ukitumia nguvu zako..Kwa hiyo, vitendo vya kuwa taunted, teased, pushed na hata kupigwa ni ukweli unaokubalika kudhihirisha unyonge, lakini fikra za unyonge huo utumike kama kiamsho (vital necessity) cha fikra mpya za kutafuta dawa ya kukomesha mchezo huo wa kuonewa kila siku..

  Katika maisha yetu ya kila siku, tunawaambia watoto zetu usikubali kuonewa tena, jikaze wewe mwanamme, kabiriana naye, hakushindi kwani yeye ana mikono mingapi?.. na kadhalika..
  Nadhani usemi huu ndipo uliposimama yaani katikati ya matatizo na solution.
  Huu ni ujumbe mzuri sana kwani unatazama unyonge kisha unakupa nguvu na fikra za kukabiliana na tatizo lililopo mbele yako..
  Tatizo la usemi huu ni katika utekelezaji..Nchi kama Tanzania badala ya kukabiriana na matatizo yetu sisi hutafuta mtu mwingne (mnyonge) wa kum bully..nikiwa na maana strength yetu tunaihesabu jinsi tunavyowasumbua wengine -in the case of our economy - tunajishughulisha ktk matatizo yasiyokuwepo..
   
 5. Recta

  Recta JF-Expert Member

  #5
  Feb 28, 2009
  Joined: Dec 8, 2006
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mkuu Mkandara, what you said is absolutely correct.

  Matatizo mengi tunayokumbana nayo mara nyingi tunayaogopa na kuyaweka kando na hivyo kuendelea kutusumbua, ama tunatafuta wa kumlaumu badala ya kutafuta solution(s).

  Tanzania ni nchi yenye rasilimali nyingi sana. Kuna mito na chemchem, Maziwa na Bahari (zaidi ya 1440km), kuna milima na mabonde, kuna almasi, dhahabu, Tanzanite, na vito vingine vingi. Kuna ardhi nzuri kubwa na yenye rutuba. Kuna hali nzuri ya hewa mwaka mzima. Hakuna dhoruba, vimbunga wala catastrophes zozote miaka yote. Kuna vivutio vingi vya utalii na kumbukumbu za kihistoria. Ila kwa kuwa hatujaamua kuvitumia ipasavyo, matatizo yetu mengi yanaendelea kutusumbua.

  Tanzania ina watu zaidi ya 35 million. Baadhi ya watu hao wana uwezo mkubwa wa kiutaalam, wana exposure, wana elimu nzuri tu, ila haitumiki vizuri au hawatumiki kabisa (inawezekana hawajulikani kabisa) katika kuleta hali bora za maisha ya waTanzania. Badala yake watu hao wamekuwa wakitumiwa vizuri na majirani zetu kuendesha miradi mizuri na yenye manufaa kwa majirani hao. Sisi tunabaki kuogopa kuanza. Hatujui kila tunapoahirisha kuanza kutumia rasilimali zetu, ndipo mahitaji mapya yanapojitokeza, na nguvu zetu zinapoyoyoma na kutotosha.

  Ili tuendelee, tunahitaji kuamka, kuaminiana, kushirikiana na kufanya yote yanayofaa kwa ustawi wa taifa letu. Tufanye leo na si kesho. Maana tusipofanya leo, kesho tutakuwa weak zaidi.
   
Loading...