Mkapa anashitakika - Dk. Slaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkapa anashitakika - Dk. Slaa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Feb 17, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Feb 17, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,572
  Likes Received: 82,060
  Trophy Points: 280
  Mkapa anashitakika - Dk. Slaa

  na Edward Kinabo
  Tanzania Daima~Sauti ya Watu

  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeendelea kumshinikiza Rais Jakaya Kikwete kumchukulia hatua za kisheria Rais wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, kwa kutumia vibaya madaraka yake wakati wa kipindi chake cha uongozi.

  Chama hicho kimewataka Watanzania kutokubali kuendelea kupotoshwa na baadhi ya watu wanaokuwa wanadai kuwa Mkapa hawezi kushitakiwa hadi Bunge limwondolee kinga.

  CHADEMA imesisitiza kuwa Rais Mkapa, sawa na rais yeyote mstaafu, hana kinga kikatiba inayozuia asishitakiwe dhidi ya makosa aliyoyafanya akiwa madarakani kama mtu binafsi.


  Hayo yalisemwa na Katibu Mkuu wa CHADEMA na Mbunge wa Karatu, Dk. Wilbrod Slaa, katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Sokoni, Kawe, Dar es Salaam, juzi, ikiwa ni mfululizo wa mikutano ya kuimarisha chama hicho iliyopewa jina la Operesheni Sangara.

  Alisema katiba ya sasa pamoja na kuwa na upungufu, haijatamka kuwa rais mstaafu hawezi kushitakiwa kwa makosa aliyofanya akiwa madarakani kama aliyoyafanya Rais Mkapa wakati wa kipindi chake cha uongozi.

  “Watanzania mpende kusoma. Mmekuwa mkipotoshwa kwamba Mkapa hawezi kushitakiwa kwa sababu ana kinga ya kikatiba. Tunasema kwa katiba yetu hii hii pamoja na upungufu wake, bado anaweza kushitakiwa kwa makosa aliyofanya akiwa madarakani…

  “Ibara ya 46 ya katiba yetu inafafanua wazi kuwa iwapo kutakuwa na haja ya rais mstaafu kufunguliwa mashitaka kwa makosa aliyofanya, ataandikiwa notisi ya siku 60 kuhusu kusudio la kumfungulia mashitaka kabla ya shauri hilo kupelekwa mahakamani.

  “Watu wanapotosha kuwa hawezi kushitakiwa hadi aondolewe kinga bungeni. Kinga gani? Katiba yetu haizungumzii chochote kuhusu kinga dhidi ya mtu aliyetenda mambo binafsi wakati akiwa madarakani,” alisema Dk. Slaa.


  Akifafanua zaidi suala hilo, alisema matendo ambayo rais mstaafu hawezi kufunguliwa kesi hadi aondolewe kinga ni yale tu aliyoyafanya kama rais, katika madaraka yake kisheria kama kuwaachia huru wafungwa, kuidhinisha sheria na masuala mengine yaliyoainishwa kwenye katiba ya nchi.

  Masuala kama ya Rais Mkapa kufanya biashara akiwa Ikulu hayahitaji kuondolewa kinga ili ashitakiwe, kwani aliyafanya nje ya mamlaka ya rais aliyopewa.

  Rais Mkapa anapaswa kushitakiwa kama watu wengine kwa kutumia Ikulu kujimilikisha hisa katika mgodi wa makaa ya mawe, kupitia kampuni aliyoiunda ya Tan Power Resources Limited na kuiingiza nchi katika hasara.

  Dk. Slaa alitoa msimamo huo kupinga kauli za baadhi ya wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) hususan kauli ya Mbunge wa Singida, Lazaro Nyalandu, ambaye hivi karibuni kupitia kipindi cha Jambo Tanzania kinachorushwa na kituo cha TBC1, alisema Mkapa aachwe ampumzike, kwani amelitendea taifa mambo mengi mazuri badala ya kuendelea kuandamwa na wanasiasa.

  Akielezea kushangazwa kwake na kauli hiyo, alisema hakutarajia mtu kama mbunge huyo kutoa kauli kama hiyo.

  “Sikutarajia kumsikia mbunge akitoa kauli kama hiyo. Hivi mtu akifanya mambo mema mia moja lakini akafanya kosa moja, polisi haimkamati”? alihoji Dk. Slaa.

  Alisema kwa sababu ya Mkapa, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) lililazimika kuilipa Tan Power Resources Limited sh milioni 300 kwa siku, kiasi alichosema ni kikubwa kuliko kile kilichokuwa kikilipwa kwa kampuni ya kufua umeme wa dharura ya Richmond ya Marekani.


  Mkataba wa TANESCO na Richmond kabla ya kuvunjwa ulikuwa ukililazimisha shirika hilo kuilipa Richmond na mrithi wake, Dowans, sh milioni 152 kila siku hata kama hazikuzalisha umeme.

  Aliwaambia wananchi hao kuwa familia ya Mkapa na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini katika serikali ya awamu ya tatu, Daniel Yona, walijimilikisha hisa za asilimia 85 za mgodi wa Kiwira.

  Kutokana na Mkapa kuhusika kwa kiasi kikubwa na ufisadi, hatua zinazochukuliwa na serikali za kuwashitaki watuhumiwa wa ufisadi bado haziridhishi, hadi hapo Mkapa na watuhumiwa wengine walioachwa watakapokamatwa na kushitakiwa.

  Kama serikali ingesimamia vizuri rasilimali za taifa, Tanzania isingehitaji hata senti moja kutoka nchi wahisani. Ameishutumu serikali ya Rais Kikwete kwa kushindwa kukusanya kodi.


  Alisema kama serikali ingekusanya vizuri mapato yatokanayo na sekta ya mifugo na uvuvi, ingeweza kupata mapato ambayo ni karibu mara tatu ya mapato yatokanayo na dhahabu.

  Dk. Slaa aliwataka wananchi hao kuiunga mkono CHADEMA na kukiimarisha chama hicho katika maeneo yao, ili kuipatia viongozi wa serikali za mitaa katika uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika Novemba mwaka huu.

  Kwa muda mrefu sasa baadhi ya watu wamekuwa wakidai kuwa Rais Mkapa hawezi kushitakiwa kwa makosa anayodaiwa kufanya akiwa madarakani, kwa sababu ana kinga ya kikatiba ya kutoshitakiwa kwa makosa aliyotenda akiwa rais.

  Watu hao ambao baadhi yao ni wasomi, wamekuwa wakipendekeza kuwa ikiwa kuna haja ya rais huyo mstaafu kushitakiwa, basi kinachopaswa kufanywa ni Bunge kuondoa kinga hiyo.
   
 2. I

  Interested Observer JF-Expert Member

  #2
  Feb 17, 2009
  Joined: Mar 27, 2006
  Messages: 1,401
  Likes Received: 433
  Trophy Points: 180
  Dr. Slaa For presidency!
   
 3. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #3
  Feb 17, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Bravo Dr. Slaa! go go go dr. for our new ukombozi from mikononi mwa FISADI'S
   
 4. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #4
  Feb 17, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Na huyo Dr. Slaa, Mkapa ndio silaha yake sio? Akumbuke kuwa chini ya CCM hizo kelele zake hazitafika popote.
   
 5. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #5
  Feb 17, 2009
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Je kama wanakula chungu kimoja na Kikwete?

   
 6. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #6
  Feb 17, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Ni yale yale ya kusema kwamba mikataba yetu ya madini ni siri kati ya serikali na wawekezaji. Of course Mkapa anashtakika. Of course bunge lina haki ya kuiona mikabata hiyo. Tuachane kabisa na hisia hizi za woga woga.
   
 7. w

  wajinga Senior Member

  #7
  Feb 17, 2009
  Joined: Jun 25, 2008
  Messages: 148
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Slaa is right and all Tanzanians should wake up from their slumber party and do the right thing join him to libarate the country from Fisadis. Not yet Uhuru my friends.
   
 8. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #8
  Feb 17, 2009
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Kama serikali haimshitaki, na kama Dr. Slaa ana vielelezo vyote vya kutosha, kwa nini yeye asichukuwe jukumu la kumshitaki? anangoja nini?
   
 9. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #9
  Feb 17, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Slaa atafanya kazi ngapi? Awe mbunge, afichue mafisadi, halafu tena mnataka amfungulie Mkapa kesi mahakamani? Kwa kusema tu kwamba Mkapa anashtakika Slaa ameshatimiza wajibu wake. Kuna vyombo vya dola. Vinaogopa nini?
   
 10. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #10
  Feb 17, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Hili ni tatizo la jamii ya akina Slaa kuogopa kuitwika lawama Serikali ya CCM inayoongozwa na Kikwete ,Dr Willbroad Sla ni mwoga anaogopa kuitonesha serikali iliyopo madarakani ,Slaa hakupaswa kumuandama Mkapa ,kwani Mkapa hivi sasa yupo Uraiani ,aliyeko madarakani ni Kikwete ,Kikwete ameshawahi kusema Mkapa aachwe kama alivyo ,sasa kurudia rudia kuhusu kinga au hana kinga ,wananchi wanalielewa na wameshaeleweshwa kitambo ,ninachomshauri Dr Slaa ni kuikalia kooni Serikali ni kuiponda serikali ni kuidharau serikali CCM chini ya Kikwete kuwa inashindwa imeshindwa haijiamini.Hivyo haifai kuwepo madarakani.

  Kama nilivyosema katika topiki fulani kuwa jamii ya akina Slaa inabana mtu mmoja mmoja na inakuwa rahisi kwa serikali kufanya au kutimiza yale yanayodaiwa na Slaa na mifano ipo ,na kumfanya mwananchi wa kawaida aone serikali imefanya ,lakini kwa ukweli ni kuisema serikali na hawa akina Mkapa kuwa kama dondoo ili kutilia nguvu hoja ya kuiponda serikali.Ili kushinda ni lazima wananchi waikane serikali kuwa sio makini na haifai na sio kumuona Mkapa ni fisadi hafai kuachiwa kuzurura.Haya ni mambo mawili tofauti na inafaa yaeleweke upinzani ni kuipinga serikali na sio kumuingia mtu mmoja mmoja na kumuandama ,haya kesho Kikwete akiamua Mkapa afikishwe mahakamani kutakuwepo na jingine la kusema ,maana serikali kuyatimiza haya ni kuwakwamisha akina Slaa ,lakini ukishaiponda serikali mbele ya macho ya wananchi ni vigumu wananchi kuikubali serikali hata ikiwakamata mafisadi wote ,ni vigumu sana kwani mwananchi atakuwa ameshajenga msimamo kuwa serikali na Chama chake haifai hivyo waondoke.
   
 11. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #11
  Feb 17, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,572
  Likes Received: 82,060
  Trophy Points: 280
  Tunataka kuona utawala bora ambapo yeyote yule ambaye anajipatia utajiri kwa njia za haramu anachunguzwa na akinekana na hatia basi apandishwe Kizimbani. Dr wala Watanzania tunaounga mkono kuchunguzwa kwa Mkapa hatuna chuki binafsi dhidi ya Mkapa bali tunataka kuona haki inatendeka na kama Mkapa kaiba mali ya Watanzania basi sheria iachwe ifuate mkondo wake na mali hizo zirudishwe chini ya miliki ya Watanzania.
   
 12. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #12
  Feb 17, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Je Dar Es Salaam, una habari kuwa kuna watu wanalipwa mishahara mikubwa inayotokana na kodi zetu kuchunguza, kukamata, kushitaki na kutoa kuhukumu ? Je una habari kuwa Dr. Slaa kama raia ameishawasaidia hao watu kwa kuwaamsha kama walikuwa wamelala, kuwakumbusha kama walikuwa wamesahau, kuwafundisha kama walikuwa hawajui, na kuwaonyesha njia kama walikuwa wamepotea - kuwa yawezekana kumbana Mkapa. Kweli hata nafsi yako haikusuti unapotumia jukwaa kama JF kutoa kauli kama uliyoitoa ? - kazi kweli kweli.
   
 13. Recta

  Recta JF-Expert Member

  #13
  Feb 17, 2009
  Joined: Dec 8, 2006
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Dr. Slaa anayo haki kabisa kufungua mashitaka juu ya ukosefu wowote aliofanya Mkapa. Nguvu na haki ya kufanya hivyo anayo. Ila anajua akifanya hivyo, atakuwa katika matatizo ya kiKatiba na ili yeye asiwemo, anataka Rais achukue jukumu hilo, halafu yeye akae pembeni akishuhudia sinema ya Kikatiba. Jamani, kwanini hatutendi tunayoongea?

  Mimi namshauri Dr. Slaa akafungue kesi hiyo. Kwa maana Rais hataifungua (hana ushahidi alionao yeye, Dr. Slaa). Aache kutaka wenzake watangulie yeye afuate nyuma. Yeye si kiongozi, aende mbele. Hapo ndipo tunakapoona ushujaa wake.
   
 14. A

  Amani Nyoni Member

  #14
  Feb 17, 2009
  Joined: Feb 17, 2009
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  "Our real problem is not our strength today, it is rather the vital necessity of action today to ensure our strength tomorrow."

  This statement is too sweat, but it is difficult to be understood by common mwanachi. You can write a book about it. I wish it could be explained or be expounded more then just leaving it hanging like that. May you do that sr?
  Thanks.
  Amani Nyoni.
   
 15. Andrew Nyerere

  Andrew Nyerere Verified User

  #15
  Feb 17, 2009
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 3,025
  Likes Received: 1,203
  Trophy Points: 280
  Nimemtazama Mkapajuzi alipokuwa Stadium,he did not look very well. He looked like he was sick.
  Mtu yeyote akitaka kumshtaki Mkapa,I think we can just call him a ""dawg."
  Rais hawezi kushtakiwa kwa mambo madogo kama haya.Ama sivyo Tanzania itaitwa Banana Republic.
   
 16. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #16
  Feb 17, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,572
  Likes Received: 82,060
  Trophy Points: 280
  Watu wengine bwana!!!! Mgodi ulifanyiwa tathmini na Wataalamu na kuonekana una thamani ya shilingi bilioni 7. Mkapa akaamua kuupora kwa njia za kifisadi kwa shilingi milioni 700 tu ambayo ni sawa na 10% ya thamani ya mgodi na mpaka sasa hivi amelipa shilingi 70 millioni tu. Hili unaliita ni jambo dogo!!!? :confused: Kazi kweli kweli!!!!!! Baadhi ya waafrika.....
   
 17. K

  Kidatu JF-Expert Member

  #17
  Feb 18, 2009
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 1,491
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Suala la kumfungulia mashitaka Mkapa ni muhimu kuliko kifo na halikwepeki. Mkapa na kundi lake (The Fisadis) ambalo kwa sasa linafikishwa mahakamani (Yona, Mramba nk) wametufikisha mahali pabaya. Huwezi kuzungumzia ama kusoma kuhusu yai bila ya kumuhusisha kuku. Yona aliiba na Mkapa kuhusu kiwira, leo hii Yona (yai) amepandishwa kizimbani, Mkapa (kuku) anangoja nini?.
   
 18. M

  Mtarajiwa JF-Expert Member

  #18
  Feb 18, 2009
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 440
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hapa mkuu kama tulikuwa tunawaza pamoja vile!
  dr. slaa umeshaongea vya kutosha,tumekusikia,tumekuelewa.ndiyo dr.,unasema mkapa haitaji kuondolewa kinga na ushahidi wote unao kuhusu ufisadi wake kitu ambacho hao wengine unaowapigia kelele wamshitaki labda hawana au hawakielewi vizuri kama wewe.
  sasa dr,nenda mahakamani,kafungue kesi tuuone ujasiri wako.mbona mwenzako mtikila huwa hapigi kelele sana.akishakijua kipengele cha sheria kilichovunjwa basi anakisimamia na anaiburuza serikali mahakamani,sasa nawe si ufanye kama yeye tu
   
 19. P

  Plotinus Member

  #19
  Feb 18, 2009
  Joined: Jan 28, 2009
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  In this post, I am going to be a little incoherent, naombeni mnisamehe!

  Unajua kuna watu wanaboa sana, wanakaa kwenye computer zao halafu kazi ni kutoa ushauri na saa nyingine kubwatuka tu -

  Yaani Dr. Slaa ajitoe mhanga peke yake tu! Wewe unayesema unashauri afungue kesi, toka Dr. Slaa ameanza vita na mafisadi, umeshafanya nini? Umemuunga mkona kiasi gani? Umechanga shillingi ngapi za kusaidia hizo harakati; Uta-support vipi financing ya hizo kesi unazotaka afungue kwa nguvu zake? Kuna maswali milioni kidogo yanajitokeza. Huko kujitoa anakofanya mpaka sasa, hata hamuoni anachofanya...always asking someone else to go a step further! WEWE JE? WHY DONT YOU?

  This is why siku zote Tanzania haikomboleki, because at all times its about someone else doing something for the country, never mimi nafanya, hapana, NEVER! Kazi kulalamika na kubwatuka behind anonymity ya fake names in the forum! Mkimaliza mnaenda kufanya kazi za kujinufaisha nyinyi na familia zenu, peaceful! Kuna watu, Mikutano hawaendi (wanasubiri news because wananchi wa kawaida ndio wakukaa kusubiri hotuba za wanasiasa-wenyewe hapana, kura hawapigi (kwasababu CCM itashinda anyway, so why bother), activism hawafanyi (wako busy na professions nk. but pia hawana guts wala patriotism ya ku-sacrifice), contribution ya ku-support movements hatoi -(kisa, watanzania wote wezi tu, hela zitaliwa, buy and large ni ubinafsi tu) in all these things, anasubiri mwingine afanye!

  Mtikila amefungua ma-kesi mengi tu dhidi ya serikali, mlikuwa wapi, mbona hamkisaidia?!

  Hebu tuwe fair na tuwe tunafanya tathmini kama watu wenye hekima! Huo uwezo tu wakusoma katiba na kuzunguka nchi nzima-ku-counter statement za viongozi wa serikali mnadhani ni kitu kidogo...mnataka afanye zaidi!

  Saa nyingine ndio maana watu wakiingia madarakani wanawasahau wananchi, they just give so much, sacrifice so much, ili wewe u-relax akufanyie kila kitu!
  Change inahitaji kufanyiwa kazi, inahitaji commitment inahitaji watu-tena wengi but it starts with an individual ku-participate!

  Ningeonelea bora ukosoe content ya alichokisema Dr. Slaa, technically or otherwise, but sio kusema afungue, kesi anangoja nini? ooh, chini ya CCM hayafiki popote! Impact ya kelele zake imefanya hata watu wazito wapande makarandinga, which was unthinkable-unprecedented kwa Tanzania, and its a start...pressure, participation, increasing political consiousness and participation in various ways and by all of us, ndio itafanya hata hizo kesi ziendelee na nyingine zifunguliwa na walioko maofisini waanze kuwa makini nk nk nk!

  Watanzania - Do something-toka kwenye comfort zone yako---acha ku-expect wengine tu ndio wafanye!
   
 20. M

  Mtarajiwa JF-Expert Member

  #20
  Feb 18, 2009
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 440
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  duh hivi kuna watu wanaamini kwamba kelele za dr slaa ndizo zilizowapeleka kina mramba kisutu??
   
Loading...