Orodha ya wasanii wenye majina makubwa lakini kiuhalisia hawana vipaji

Mh temba hauna uwezo wowote kimuziki ...aliotea zamani enz zile wasanii ni wachache
Kama ni msanii mkali atengeneze hit song sahv kama mwenzie chege
Chege ana hit song gani hivi sasa!? Maana kuna kutoa wimbo na kutoa hit song. Nisaidie hiyo hit song ya Chege.
 
Tajiri unakaza fuvu tuu , vitu vyepesi kama hivi havihitaji kutumia nguvu kubwa kivielewa
Hit song ni moja ya vigezo lakini pia nje ya hit song hao nliowataja ukiangalia nyimbo zao nyingi zilibebwa either na chorus au bit tuu
Unahamisha magoli. Mara hawana kipaji, mara hit song , mara nyimbo zilibebwa na nini sijui. Ungefanya wewe basi ili sisi wengine tu_judge. Maana hata ukiulizwa kipaji ni nini, hauna unachojibu.
 
Ila we jamaa unachekesha Sana bou nako ana Ngoma yake moja inaitwa MBIO ZA VIJITI...
Siku ukifika Musoma mjini halafu useme Bou Nako Hana kipaji walahi nakuapia kichwa chako kitakatwa mchana kweupeeeeeeeeee wapewe zawadi sangara wa ziwa Victoria...

Huyo Dudubaya unayesema Hana kipaji huenda wewe ndo hujui nyimbo zake na balaa zilizofanya mwanzoni mwa miaka ya 2000...

Hivi ulibahatika kusikiliza hizi ngoma Kwanza..
1. Nakupenda mpenzi
2. Nimeondoka
3. Mashaka
4. Nakupenda tu
5. Manundu
Aisee hiyo namba 4 uswahilini kwenye harusi moja wahuni wali_bang sana. 2004 hiyo kama sikosei. Mkono wa MJ nakumbuka huo.
 
Kuna watu wengi hawajui wanachokizungumza. Na wengine hawajui muziki. Usanii una mambo mengi. Usanii wa muziki pia unaambo mengi kuna utunzi/uandishi, uimbaji, ualimu wa sauti, kurap, au kufanya mziki ktk style fulani au utamaduni fulani. Mfano Saida Karoli, wanne star, mpoto nk.

Hao na wengine wengi tunawaita wasanii wa muziki kwa kuwa muziki au wanachokifanya (uimbaji ni zao la sanaa).

Sasa kuwakubali au kutokuwakubali lazima uweke vigezo vyako au mkubaliane ktk vigezo ili tuelewane. Mfano kuna msanii Mimi naweza kumfahamu lakini mtoa mada au mchangiajiwingine asimfahamu. Mfano Naomisia msanii wa muziki lakini na uhakika wengi hawamfahamu. Sasa kama kigezo ni kufahamika na watu je huyo hatoweza kuwa msanii???

Kuna inshu ya kutoa hitkali. Hiti Kali kwa nani?
Juzi hapa kuna tunzo za hip-hop na kila mtu kazibeza. Maana yake waliozotoa waliona zinastahilo lakini wengi wameona hazistahili. Maana yake unaweza kumuona Ray-Van mkali mi nikakwambia Aslay ni mkali kwa Hawa vijana wabana pua. Mwingine akamkubali Harmonize kwa kuwa amepambana na system akatoboa yaani kipaji na upambani vinaweza kutumika kama kigezo, ila kwa nani?

Mi ntamkubali Suma mnazareti kwa Flow...we utamkubali Roma kwa ujumbe lakini mwingine atasema Roma hawezi badilika beat ni sawa tempo moja...

Kikubwa mkubaliane ktk vigezo. The means justifies the end...hivyo yaani...
 
Jina la Kisanii alikua anaitwa Mr. II au Mr. 2 before hajaitwa Sugu alikua anaitwa Mr. II aka Sugu alipotoa 'wananiita Sugu' na Stala Thomas akafuta Mr. II akajiita Sugu km Sugu, sasa tafuta hio ngoma inaitwa "Wananiita Sugu" uisikilize ukimaliza rudi hapa Ila kabla haujarudi fanya paaaaap bonyeza dude moja linaitwa Mambo ya Fedha Sugu ft. Lady Jay Dee ukimaliza kusikiliza njoo hapa

Tatizo vijana wa 2000 wanawezaje kumjua Sugu wasamehee tu
 
Back
Top Bottom